Ukigundua Mke ama Mume wa rafiki yako anacheat utafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukigundua Mke ama Mume wa rafiki yako anacheat utafanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Wakumwitu, Feb 3, 2011.

 1. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana jamvi, hii tabia imekuwa ikinikera hata sijui cha kufanya "is kind off" niko kwenye "dilemma". Nina rafiki yangu mpenzi ambaye hivi siku za karibuni nimegundua kuwa wife wake anacheat na sehemu anayofanyia huo mchezo naifahamu. Rohoni najiuliza kumwambia mme wake ndoa yao inaweza vunjika, na itakuwa mm ndiye niliyesababisha kuvunjika kwa kutoa siri hiyo. Lakini naumia sana rohoni maana, utakuta rafiki yangu anakwama kufanya shughuli zake zingine akidhani wife wake yuko kazini na gari kumbe amebana sehemu na jamaa yake. Wakati mwingine ananiomba niende kumpeleka sehemu anayotaka kwenda. of course kwa kuwa ni rafiki yangu naenda huku rohoni naumia nikiwaza kama hivi ingekuwa mm rafiki yangu ananiambia wife wako anacheat sehemu furani ninge react namna gani. Kinachosikitisha huyo mama kila wakati ananilalamikia jinsi mume wake anavyocheat. Najiuliza hivi huwa haoni aibu kulalamika na yeye ndiyo mchezo wake? Naomba ushauri wenu nimwambie????
   
 2. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mi binafsi, nikimuona demu/wife wa best wangu anacheat ni lazima nimwambie mwenyewe......kwa sababu hata mimi ningependa niambiwe kiburudisho changu kikiwa kinakunwa na njemba ingine.

  kama ye alikuwa hataki ndoa ivunjike asingecheat.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Inabidi umkanye mhusika anayefanya cheating aachane na hiyo tabia na si kwenda kuharibu mahusiano kati yake kwa mke/mme wake
   
 4. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Thanks FL1 ila pia yataka moyo maana wadada nao balaa, unaweza ukamwambia wewe acha hiyo tabia ukasikia kesho kwa mume wake rafiki yako amenitongoza nimemkataa eti anasema natembea na furani ili tuu ajihami akijua unaweza mwambia mumewe.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Bravo shem langu!
  Mwite huyo mama na umwambie ushajua janja zake, na umpe ushahidi ili asikufanyie bifu!
  Japokuwa akina mama wengine anaweza akakulengesha hadi na wewe ukaingia kingi na kugonga, ili kuziba soo hilo!..ha ha haaaa!
  Akiendelea then mpe live bwanake bila kukwepesha macho, ni bora hao watu waachane, maana hawapendani kidhati!
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mi nadhani mficha dhambi nae kashiriki dhambi hiyo.Hivi utajisikiaje siku ukija kuambiwa wana ngoma wkt wewe ulijua wazi mchezo wake?? utafurahi sana kuona watoto wake wanataabika kwa kukosa wazazi?? jaribu kufanya fumanizi ambalo litakuwa la kiintelijensia.unawez kumchukua jamaa bila kumwambia lolote ukapita nae hayo maeneo mkewe anakobanjuliwa ukamshtua """enheee kama vile naona gari la shemeji pale""" lazima jamaa atashuka achungulie hapo fumaninzi litakuwa limekamilika na hatakulaumu kwa kuwa nawe unajifanya hukujua kama yupo hapnk au ukatumia mbinu ingine yoyote.hakuna kitu kibaya kama kuficha dhambi eti kuokoa ndoa wkt ndo unachangia kuiuwa kabisa.Msema kwlei ni mpenzi wa Mungi na pia Ukweli utakuweka huru daima.
   
 7. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa ndugu yangu Lokissa nimekusikia..hili jambo linanisumbua sana na njia pekee ya kuacha kuniumiza ni kulitafutia ufumbuzi.
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yataka moyo kama shem ni bomba nitamfata ili anizibe mdomo alafu nitamwambia ucrudie tena na nitamtafuta yule jamaa aliyekuwa anachakachua nae nitampa onyo la sivyo nitamkamatisha
   
 9. M

  Msindima JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kabisa, nakubaliana na wewe, anaweza kwenda kumwambia baadae wenyewe wakija-kumaliza tofauti zao ataonekana mchonganishi.
   
 10. B

  BeNoir Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku huyo shemeji yako akikuletea tena lalamiko kuhusu mumewe, chukua nafasi hiyo kumuonya yeye kwa mifano mingi tu. Kama anajidai haelewi basi mpe la wazi kuhusu hiyo tabia yake ambayo unahisi anafanya. Rafiki yako akielezwa basi utachukua jukumu la kumueleza lililokuwa linaendelea na hatua uliyochukua kusave ndoa yao, ila mama yeye kaamua kuitibua jumla. Huwezi kuwa mwema kote.
   
 11. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,668
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  He! hiyo kali sasa si utamuongezea namba ya michito jamani, sasa hiyo siku utakayotoka naye wewe ndio jamaa atawabamba.. au sijakuelewa?
   
 12. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #12
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  siku hizi mbona simple tu. nenda na cha kurekodia maongezi, ongea naye. then akiyapeleka kwa mumewe sasa wewe nenda na evidence ya mazungumzo yenu
   
 13. semango

  semango JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kama jamaa ni RAFIKI YAKO KIPENZI then la msingi ni kuhakikisha ujumbe unamfikia haraka iwezekanavyo.yani iwe kwa majungu, fitna, bunduki au mshale lazima jamaa ajue.lakini kama jamaa ni mshkaji tu wa kukutana kwenye vijiwe then kula ganzi na upotezee tu.
   
 14. GATS

  GATS JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 240
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni hatari nakwambia ogopa sana mke wa mtu. Je wewe ungafanyiwa hivyo ingekuwaje? we mueleze ukweli huyo rafiki yako na mke wake kwa moyo mweupe tu. Usigone kabisa. achana na ushauri huo.
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  we utakuwa wa mwisho kwani unampa onyo uwezi kukamatwa coz ufanyi matangazo ujue ucpofanya nae na ukamkanya tayari umemjengea hofu kwamba utakwenda kumsemea japo umemwambia na kumwapia utomweleza my husband wake kila siku atakuwa na wasiwasi yaliwai kunikuta nikamkanya akakubali lakini akawa na wasiwasi baada ya miezi 3 alinifata akaniambie kweli shem sijawai kuona mwanaume kama ww mana kweli nimedadisi nimegundua my husband wangu ajui so ukiduu nae inakuwa kama kiapo cha utii
   
 16. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Jamani acheni masihara haya mambo hayo uyasikie tu humu kwenye mtandao usiombe kukutana nayo!!Yanasononesha sana,Kufumania au kufumaniwa siyo jambo jema kabisa katika maisha ya ndoa!!Na hakuna baya linalojenga jema,Ila jema lina kawaida ya kujenga ubaya. Nia nzuri ya kuokoa ndoa ya mwenzio yaweza kukuponza wewe wakati mwingine hata huo urafiki wenu ukawa shubiri.
   
 17. loveness love

  loveness love Senior Member

  #17
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umewaeleza ipasavyo kama mie na cheating na flani itahusu vipi ukamuambie my honey?
   
 18. loveness love

  loveness love Senior Member

  #18
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bravo wowwwww bravo wwww
   
 19. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mimi ningemwambia tu huyo rafiki yangu cause akija kujua wewe ulikuwa unajua siku zote halafu humwambii atakushangaa sana. na atakukasirikia hatar ila pia unaweza kujaribu kumwambia shem wako kwanza ukiona analeta za kuleta umwambie rafiki yako
   
 20. GATS

  GATS JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 240
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii nimeipenda afanye hivyo
   
Loading...