Ukifuata life style ya Hayati Magufuli au Nyerere, kwa karne hii huwezi kuishi maisha marefu

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,014
35,777
Hii ni kwa wote uwe Kiongozi kwa ngazi ya kitaifa au chini yake.

Kuna wimbo wa Orchestra Safari Sound unaitwa Dunia Msongamano, kuna sehemu wanaimba¶¶kufa kwa binadamu hupangwa na Mungu nakuomba mwenyezi anipe maisha¶¶

Pamoja na hayo kuna other factors contributed by the bearer. Usiwe mzalendo kupitiliza,hii nchi ni kubwa sana na ina wahuni wengi sana. Nyerere na Magufuli walipitiliza.

Ishi viziri na wazungu, huwezi kushindana na wazungu, Mzee Ruksa na JK walilijua hili. Usiwe mnoko sana kazini. Chunga mdomo wako, fanya mambo yako kimya kimya, ongea inapobidi.

Nchi sio ya baba yako utaondoka utaiacha, play your party, utakapokomea waachie wengine wamalizie.

Usiponde watangulizi wako. Kula bata, maisha ndio haya haya, Nyerere alikuwa anashindia mihogo, JPM alivyoingia Ikulu tu akatimua wapishi binafsi eti atapikiwa na mama yetu kipenzi mama Janeth.

Kiongozi yeyote ukifuata haya huenda ukaongeza siku mbili tatu za kuishi kinyume chake hutoboi.

Mandela mwenyewe alilijua hili, alipotoka jela wala hakujenga bifu na wazungu japo walimfunga mbuzi wale ila aliwasamehe, na alikula bata sana uzeeni. Miundombinu unayoiona South Africa mingi ilijengwa kipindi cha Kaburu.

Mwisho kabisa, usiwe mkweli sana, have some sort of hypocrites
 
aka 2016 mpaka 2020 Tanzania iligubikwa na makelele ya Tundu Lisu aloyejiona yeye tu ndiyo mwenye haki ya kumshauri rais wa nchi wa wakati huo na ni lazima ushauri wake ufuatwe!
Hata hivyo hayati Magufuli alisimama imara na kupuuza makelele yote ya wakala wa mabeberu Tundu Lisu.

Kama hayati raisi Magufuli asingekuwa imara na akasikiliza makelele ya Lisu, haya hapa yangetokea Tanzania.

1. Tanzania tusingekuwa na bwawa la kufua umeme ambalo ni moja ya mabwawa makubwa barani Afrika. Urefu wa bwawa la Nyerere ni km100 yani sawa na urefu wa kutoka Dar mpaka Chalinze.
Tundu Lisu kwa kutumiwa na mbabeberu kwa ahadi ya kumlisha yeye na familia yake pamoja na kumpa hifadhi Ubelgiji alipinga sana ujenzi wa bwawa hili kwa kisingizio kwamba litasababisha uharibifu wa mazingira na mvua hazitanyesha tena Tanzania!. Leo mwaka 2023 bwawa linajazwa maji na Tanzania imegubikwa na mafuriko kila sehemu kwani mvua zinanyesha sana kinyume na utabiri wa Tundu Lisu.

2. Tanzania isingekuwa na ujenzi wa SGR .
Tundu Lisu alipinga sana ujenzi wa reli hii ya umeme na yenye kasi zaidi Afrika yote.

3. Serikali isingehamia Dodoma.
Tundu Lisu na Mbowe walipinga sana serikali kuhamia Dodoma wakisema huko ni kutesa watumishi na kwamba serikali ibaki tu Dares salaam kwa ndoto za mwl Nyerere zimepotwa na wakati. Hayati Magufuli aliziba masikio na leo serikali yote ipo Dodoma.

4. Kampuni ya madini ya Acacia ingekuwepo.
Licha ya kwamba Lisu amesoma kwa kodi za watanzania lakini aligeuka kuwa mwanasheria wa Acacia na akasema ataisaidia kutushitaki MIGA ,kama tukiendelea kuwadai hela za wizi wa makinikia. Hayati Magufuli aliendelea mbele hadi kampuni ya Acacia ikafutwa na kuzaliwa kampuni mpya ya Twiga ambayo watanzania wapo kwenye management na Tanzania yakafunguliwa masoko ya madini kila sehemu, na watanzania wakanufaika na madini yao.

5. Kenya na India zingeendelea kuongoza kwenye uuzaji wa madini ya Tanzanite .
Kutokana na ukweli madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu. Hayati Magufuli alichukua hatua kali sana za kudhibiti madini ya Tanzanite ikiwemo kujenga ukuta wa kuzunguka mgodi huo, hatua hizo zilipingwa mno na Lisu na akaita ni udikteta mkubwa kufanya hivy
 
Kumuweka mwalim jk sambamba na magufuli sio sawa, kwanza ktk hili wapo tofaut san. Mwalim alijua kuishi na wazungu!! Mzungu kuleteana nae ubabe hutoboi hasa ukizingatia still unamtegema mpaka budget yako!!!

Tutakuwa tegemezi mpaka lini?!

Kisa kuogopa kufa….kufa kupo…kila mtu ana sababu yake kuwepo hapa duniani…akishatimiza anasepa

Tanzania tunahitaji mapinduzi ya kiuchumi ilitutoboe…tunahitaji kiongozi jasiri kupitiliza Magufuli…na watanzania tukubali maumivu…tatizo tunataka kujenga nyumba huku tunakula bia…haiwezekani…
 
Hii ni kwa wote uwe Kiongozi kwa ngazi ya kitaifa au chini yake.

Kuna wimbo wa Orchestra Safari Sound unaitwa Dunia Msongamano, kuna sehemu wanaimba¶¶kufa kwa binadamu hupangwa na Mungu nakuomba mwenyezi anipe maisha¶¶

Pamoja na hayo kuna other factors contributed by the bearer. Usiwe mzalendo kupitiliza,hii nchi ni kubwa sana na ina wahuni wengi sana. Nyerere na Magufuli walipitiliza.

Ishi viziri na wazungu, huwezi kushindana na wazungu, Mzee Ruksa na JK walilijua hili. Usiwe mnoko sana kazini. Chunga mdomo wako, fanya mambo yako kimya kimya, ongea inapobidi.

Nchi sio ya baba yako utaondoka utaiacha, play your party, utakapokomea waachie wengine wamalizie.

Usiponde watangulizi wako. Kula bata, maisha ndio haya haya, Nyerere alikuwa anashindia mihogo, JPM alivyoingia Ikulu tu akatimua wapishi binafsi eti atapikiwa na mama yetu kipenzi mama Janeth.

Kiongozi yeyote ukifuata haya huenda ukaongeza siku mbili tatu za kuishi kinyume chake hutoboi.

Mandela mwenyewe alilijua hili, alipotoka jela wala hakujenga bifu na wazungu japo walimfunga mbuzi wale ila aliwasamehe, na alikula bata sana uzeeni. Miundombinu unayoiona South Africa mingi ilijengwa kipindi cha Kaburu.

Mwisho kabisa, usiwe mkweli sana, have some sort of hypocrites
Wewe jamaa una masihara sana, yaani unamweka Nyerere kundi moja na ujinga?
Jiwe ni kaliba ya akina Bashite, Saambaya na Mnyeto. Acha kumuabisha baba wa Taifa
 
Back
Top Bottom