Ukifikiri kama nyundo,kila kitu kinaonekana kama msumari

udongo

Member
Oct 28, 2010
14
0
Suala lililotokea mbeya siku mbili zilizopita ni kitu hatari sana ambalo viongozi wetu tulionao naona kama wanafanyakazi kwa mazoea tuuu. Yaani nitaamka dereva atakuja kunichukua nitaenda ofisini, secretary ataniletea chai na vitumbua tutaingia kwenye kikao tutafanya maamuzi bila kufikiri matokeo yake tutalipana posho ya kikao, lunch, semina, saa tisa dereva atanipeleka bar. Hivi kweli uongozi wa mkoa wa mbeya ulishindwa kufikiri jibu zuri zaidi ya kushughulikia tatizo la wamachinga, hivi hawa sio ndio vijana tunaopita majukwaani tukisema ajira zinaongezeka? waliwafukuza waende wapi? Warudi kijijini? Au kwa sababu tunafikiri kama nyundo basi kila kitu ni msumari? Hivi angetokea mwanasiasa wa kihuni akahamasisha kuwe na uvunjifu wa amani polisi na dola wangeua watu wangapi? Halafu je tatizo lingeisha baada ya kuua? Hivi kweli kiongozi anafanya mambo ya kijinga halafu analaumu mambo ya siasa hivi Sugu asingeenda Mbeya Kandoro angeweza kuwatuliza ule umati wa watu? Jamani viongozi hamuwezi ku think out of the box?
 
Back
Top Bottom