Ukifanya kienyeji, utakuwa wa kienyeji

EddoLexus

Member
Jul 21, 2019
16
25
Dunia ya leo inataka watu wanaoweza kuishi ndani yake, nikimaanisha kama wewe ni mjasiriamali na unataka kufanikiwa katika shughulizako za kijasiriamali lazima uichunguze dunia ya leo inataka ufanye nini kuhakikisha unafanikiwa katika shughuli zako. Usipowekeza ufahamu wako katika mahitaji ya dunia ya leo katika shughuli zako au huduma unayotoa au unayotaka kutoa basi kuwa na uhakika wa kuishia njiani maana watakaotoa huduma kama yako na wamegundua dunia inachotaka watakupa stress sanaa.
Nakupa mfano ambao kila mtu anaweza kuwa shuhuda kwa watua ambao hawakuweza kubadilika kutokana na mahitaji ya dunia ya leo wenyewe walibaki kuwa wa kienyeji,,,,Kwa wale waliozaliwa miaka ya 80 mpaka 90, utakuta kipindi unakua miaka ile ulikuta mtu ana duka na kijiji kizima anajulikana kuwa ana duka maana watu wanategemea huduma kutoka kwake, muda mwingine anafunga duka anaenda shambani mpaka akirudi ndipo mpate huduma.Mtu huyo huyo utakuta mpaka mwaka huu duka analo lakini haja move kabisa katika biashara yake na tangu miaka ya 80 mpaka leo ilikuwa awe mbali sana lakini yuko pale pale na ukimuuliza mafanikio yake ni kama vile ndo kwanzaa anaanza maisha ya duka kumbe ndio kajua kanazamaa..... Kwa dunia ya leo funga duka hafu nenda shambani mpaka jioni subutuuu hizo bdhaa utakula na familia yako wateja wa miaka hii ukiwaroga kienyeji hawarogeki,we waroge kisasa tu utafurahi mwenyewe.

Afrika kuna mahali tunakwama
1.Hatufanyi vitu kulingana na mahitaji ya dunia ya sasa
2.Hatufanyi vitu kulingana na mahitaji ya customers,tunafanya kulingana na mahitaji yetu
3.Tunatanguliza wazo la biashara sio huduma,,Huduma bora inapelekea biashara yako kunawiri
4.Hatuna haja ya kutafuta utaalamu au kutafuta ushauri wa kitaalamu katika shughuli zetu na tunachokwepa hapa ni garama tu,, yaani mtu hata kuunga kifurushi cha 1000 aperuzi mtandaoni hakunaaaa.
5.Tunapenda kupata taarifa kwa mtu wa tatu.Huu ni ugonjwa tena wa kuombewa kabisa.Utakuta mtu anataka kufungu biashara anaanza kumuulizia mtu habari za lesni ya biashara sijui TRA,mikopo ya benk atapataje sasaaa kama sio ugonjwa ni nini,,,hayo maelezo nenda TRA,NMB,CRDB na taassisi mbalimbali husika ukapate maelezo sio kuulizia kwa mtu,waswahili wanasema atakulisha matango pori mwisho wa siku utaogopa utaacha na hapo utadhihirisha kuwa dunia ya kisasa haikuwezi wewe ni wa kienyeji tuuu
.
.
Namna pekee ya kufanikiwa ktk dunia ya leo ni kuwa wa kisasa.Kila siku fikiria namna ya kuboresha jana yako,usipoiboresha wewe wenzako wataboresha na watakupa stress tu
 
Kweli wewe ni mchumi wa vitendo..maana dunia inabadilika kwa kasi sana hivyo uking'ang'ania mfumo uliouzoea unajikuta umefeli
 
Mkuu hivi vitu sana sana wanavyo watu ambao hawajaenda shule. Ila wasomi walio wengi hatuna hii package kabisa. Ndo maana tunapigika sana mtaani.
Na kama hatutachukua hatua mapema,tunakoelekea wasomi africa watakuwa ni watu wenye maisha duni sanaaa,,, tunaishi ki madaftari sana ila nguvu ya uthubutu hatuna wengi wetu
 
Dunia ya leo inataka watu wanaoweza kuishi ndani yake, nikimaanisha kama wewe ni mjasiriamali na unataka kufanikiwa katika shughulizako za kijasiriamali lazima uichunguze dunia ya leo inataka ufanye nini kuhakikisha unafanikiwa katika shughuli zako. Usipowekeza ufahamu wako katika mahitaji ya dunia ya leo katika shughuli zako au huduma unayotoa au unayotaka kutoa basi kuwa na uhakika wa kuishia njiani maana watakaotoa huduma kama yako na wamegundua dunia inachotaka watakupa stress sanaa.
Nakupa mfano ambao kila mtu anaweza kuwa shuhuda kwa watua ambao hawakuweza kubadilika kutokana na mahitaji ya dunia ya leo wenyewe walibaki kuwa wa kienyeji,,,,Kwa wale waliozaliwa miaka ya 80 mpaka 90, utakuta kipindi unakua miaka ile ulikuta mtu ana duka na kijiji kizima anajulikana kuwa ana duka maana watu wanategemea huduma kutoka kwake, muda mwingine anafunga duka anaenda shambani mpaka akirudi ndipo mpate huduma.Mtu huyo huyo utakuta mpaka mwaka huu duka analo lakini haja move kabisa katika biashara yake na tangu miaka ya 80 mpaka leo ilikuwa awe mbali sana lakini yuko pale pale na ukimuuliza mafanikio yake ni kama vile ndo kwanzaa anaanza maisha ya duka kumbe ndio kajua kanazamaa..... Kwa dunia ya leo funga duka hafu nenda shambani mpaka jioni subutuuu hizo bdhaa utakula na familia yako wateja wa miaka hii ukiwaroga kienyeji hawarogeki,we waroge kisasa tu utafurahi mwenyewe.

Afrika kuna mahali tunakwama
1.Hatufanyi vitu kulingana na mahitaji ya dunia ya sasa
2.Hatufanyi vitu kulingana na mahitaji ya customers,tunafanya kulingana na mahitaji yetu
3.Tunatanguliza wazo la biashara sio huduma,,Huduma bora inapelekea biashara yako kunawiri
4.Hatuna haja ya kutafuta utaalamu au kutafuta ushauri wa kitaalamu katika shughuli zetu na tunachokwepa hapa ni garama tu,, yaani mtu hata kuunga kifurushi cha 1000 aperuzi mtandaoni hakunaaaa.
5.Tunapenda kupata taarifa kwa mtu wa tatu.Huu ni ugonjwa tena wa kuombewa kabisa.Utakuta mtu anataka kufungu biashara anaanza kumuulizia mtu habari za lesni ya biashara sijui TRA,mikopo ya benk atapataje sasaaa kama sio ugonjwa ni nini,,,hayo maelezo nenda TRA,NMB,CRDB na taassisi mbalimbali husika ukapate maelezo sio kuulizia kwa mtu,waswahili wanasema atakulisha matango pori mwisho wa siku utaogopa utaacha na hapo utadhihirisha kuwa dunia ya kisasa haikuwezi wewe ni wa kienyeji tuuu
.
.
Namna pekee ya kufanikiwa ktk dunia ya leo ni kuwa wa kisasa.Kila siku fikiria namna ya kuboresha jana yako,usipoiboresha wewe wenzako wataboresha na watakupa stress tu
asante mkuu nmejifunza kitu pia safi sana
 
Back
Top Bottom