Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 65,797
- 156,922
Habari za wakati huu waungwana.
Leo natamani kuwashirikisha jambo ambalo limekuwa likinitatiza kwa muda mrefu katika jamii yetu ya Kitanzania zaidi kuliko mataifa mengine.
Mara nyingi nimepata kusikia maneno mabaya hasa yakiwatuhumu watu wenye mafanikio au wenye mwelekeo wa kufanikiwa au kufikia ndoto zao.
Kwa mfano;
1. Utakuta mtu alikuwa mfanyabiashara
mdogo, ukafika wakati akakuza mtaji
akawa na biashara kubwa na kufikia
hatua ya kujitanua kibiashara au hata
kuanza kwenda nje ya nchi kununua
bidhaa na kuleta nchini.
ndipo maneno huanza..ooh huyu sio
mtu mzuri, mchawi au free m.
2. Au mwajiriwa akianza kufanikiwa tu
utaanza kusikia anatumia ndumba
au hana lolote ni mikopo tu.
3. Wana muziki na kada zingine hawa
jaachwa salama nao wametuhumiwa
kwa mambo kibao.
4. wanasiasa wakipata uteuzi hasa wana
wake...mnajua tuhuma zao pia.
Nimejaribu sana kufanya utafiti wa hizi tuhuma na
mwisho wa siku nimejiridhisha kwa 80%
pasi na shaka kuwa ujinga, umasikini na roho mbaya za kuhalalisha umasikini ndizo chanzo.
Tafsri yake ni kuwa hao waliofanikiwa si chochote sababu sio juhudi binafsi.
Tubadilike, wanapofanikiwa wenzetu iwe ni chachu kwetu ili kufikia hatua waliofikia.
muwe na wakati mwema wote.