Ukielimika aidha kwa kujiongoza mwenyewe au kwa kuongozwa na mtu basi utapata maarifa

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Tukumbushane kwa hili.

Ukielimika aidha kwa kujiongoza mwenyewe au kwa kuongozwa na mtu basi utapata maarifa.

Maarifa huzaa amani, ujuzi, fikra fikirishi na huepuka maangamizo ya kuonekana au kutoonekana kwa mambo maovu kwa yajao au kwa yaliyokwisha kutokea.

Msisitize rafiki, ndugu, jamaa, familia au mwanao kuwa elimu sio tu ni taa ya maisha bali elimu ndio nuru iletayo mwanga duniani.

"Apendaye mafundisho, hupenda maarifa."

Kataa kuwa mtumwa.
 
Back
Top Bottom