denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,511
- 68,141
Wazungu wanasema; The Sky is the Limit.
Hii kauli itatimia kwa mchezaji wa mpira wa miguu yeyote atakayejitahidi aichezee klabu ya Simba ya Tanzania.
Alianza Samatta, kutoka Simba SC akaenda Mazembe, baada ya hapo akawa mfungaji bora na kuitangaza nchi kimataifa mwishowe akaenda zake Ulaya.
Jana usiku mchezaji kutoka Senegal, Pape O. Sakho, ametambulishwa kwenye ulimwengu wa soka duniani kupitia Simba SC, nina hakika huyu Sakho kuna raia wa Senegal waliokuwa hawamfahamu kabisa.
Lakini nguvu ya mashabiki wa Simba SC mitandaoni, hawa wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba kwa umoja wao wakiungana kusimamia jambo lao, hakuna yeyote wa kuwazuia, sio tu hapa Tanzania, au Afrika Mashariki na kati, bali ni kwa bara zima la Afrika.
Naandika haya sio kwa kusifia bila sababu, hapana, yeyote anayeona sina sababu aende akaangalie idadi ya followers ya mashabiki wa Simba SC kwenye mitandao, aanzie FB, aende twitter, kisha akamalizie na Instagram halafu alete majibu hapa.
Hata huyu jamaa yao aliyepigwa "rungu la utosini" jana na Kamati ya Maadili TFF, sehemu kubwa ya followers wake anaotamba nao leo, aliwapata akiwa Simba SC, this is the truth, usirushe ngumi mtani!