Ukichelewa kuoa/kuolewa au mahusiano strong mpaka 30s una possibilities kubwa ya kulamba garasa

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
Habari wadau,

Je hii tetesi ni kweli.

Wengi wanasema mtu anaechelewa kuoa au kuolewa au kuwa na mahusiano ya kueleweka mpaka anafika 30s ana possibilities kubwa ya kuolewa au kuoa mtu ambaye hana upendo nae sababu ya desperation.

Eti sisi ambao mpaka 30s bado tuna mingle kusaka mahusiano mapya tuna possibilities kubwa ya kuoa au kuolewa na vimeo mabaki ya wachaguzi waliowahi na inasemekana ndoa nyingi za utu uzima azijengwi na upendo bali ni kuvumiliana tu upate wa kuzikana nae maana tunaowapenda wengi wanakuwa wameshawahiwa.
 
muda muafaka ukifika inabidi kuoa/kuolewa... swala la umri sio kiashilia sahihi!!!

upo tiari!?? unauwezo wa kuishi katika ndoa!?? then hata miaka 19 unakaribishwa ndoani
 
Kwa upande wa kike ni hatari sana. Kwa sababu kumpata mwanaume ambae ajawa na Family yenye watoto inakuwa ishu sana. Kwa mwanaume unakula ujana tuuu
 
Vijana wengi wanaooana kuanzia umri wa miaka 30 na kuendelea kunauwezokano mkubwa kwa ndoa zao kudumu kwa kipindi kirefu zaidi pengina hata mwisho wa maisha yao. Ila ndoa za vijana below 30yrs ndoa zao zinakumbwa misukosuko hata kufikia kubwagana na hata kutuona roho.

Nb; Upendo hutengenezwa na kuimarishwa kama vile mkulima apandapo zao lako na kulihidumia ikiwa anataka mazao bora .
 
Kama ilivyo kwenye ujenzi, ujenzi bora na imara huendana na ununuzi wa vifaa bora, kuajiri mafundi stadi na wenye weledi ambao ni was min of I, usimamizi mzuri n.k.

Vivyo hivyo kwenye mapenzi. Kuna mapenzi ambayo ni "natural" na mapenzi ya kutengeneza. Unampata mtu unajitoa kwa ajili yake huku ukijitahidi kuwa "faraja na furaha yake". Unajifunza "udhaifu na uimara" wake lengo ni kumfanya aone fahari na si karaha kuwa na wewe.

Jaribu kusoma kitabu kinachoitwa "BIKIRA YANGU" kilichoandikwa na Privatus Karugendo.
 
Ndoa ni muunganiko wa kimwili uliojengwa kwa upendo wa dhati kwenye nyoyo ya wanandoa....upendo huo unawafanya wanandoa wote wawe kama ni mwili mmoja.......
Katika ndoa iliyojengwa kwa upendo ndani yake msamiati wa taraka haupo kabisa kwani kutokana na upendo kati yao kila mmoja najitahidi kwa kadri ya uwezo wake kukabiliana na changamoto zinazowakabili ili kuiimarisha ndoa kwani kwao ni furaha kuwa pamoja na huzuni na vilio kutengana........

Kuishi na mtu kwa kipindi chote cha miasha yako huku mkishare vitu vingi kwenye maisha yenu sio jambo jepesi.....ni jambo linalowezeshwa na nguvu kubwa ya upendo kati yenu....ambayo ni upendo wa dhati baina yenu........

Ni upendo pekee utakaowafanya mvumiliane kwenye shida na raha...
Ni upendo pekee utakaowafanya kila mmoja aumie pindi awapo mbali na mwenzie........
Ni upendo pekee utakaokufanya umuone mkeo au mumeo kuwa ni mtanashati au mrembo kuliko wote chini ya jua............

LOVE TAKES TIME.....
 
Yaani mtu hujatimiza malengo yako hata 1/2 halafu ukimbilie kuoa kisa you are at 30's?

Huo ni ukichaa no.1

Unakimbilia kuoa kwa sifa au? Jipange mkuu tengeneza pesa kwanza.
 
Kiukweli watu weny umri wa kuanzia miaka 28 hasa kwa wanawake, wengi huwa hawana mapenz ya kweli. Wameolewa kwa sbb ya kuona umri umeenda na akipata mtu anayempenda kuisaliti ndoa yake huwa ni rahic sana.
Ila kwa mwanaume age kuanzia 30 huwa mara nying ni wale waliochoka starehe za papuch kwahiy anaamua kuoa ili atulie. Ila uwezekano wa kumuoa mtu usiyempenda upo pia sbb umri wa huu huwa kunashinikizo kubwa la watu wa nje kukulazimisha uoe na pia wanawake weng huwa wanajilengesha na pia kunakutegeshewa mimba kwahiyo unajikuta umemuoa mwanamke usiye mpenda.
 
Habari wadau,

Je hii tetesi ni kweli.

Wengi wanasema mtu anaechelewa kuoa au kuolewa au kuwa na mahusiano ya kueleweka mpaka anafika 30s ana possibilities kubwa ya kuolewa au kuoa mtu ambaye hana upendo nae sababu ya desperation.

Eti sisi ambao mpaka 30s bado tuna mingle kusaka mahusiano mapya tuna possibilities kubwa ya kuoa au kuolewa na vimeo mabaki ya wachaguzi waliowahi na inasemekana ndoa nyingi za utu uzima azijengwi na upendo bali ni kuvumiliana tu upate wa kuzikana nae maana tunaowapenda wengi wanakuwa wameshawahiwa.
kwani hizo ndoa za wenye 20 ndo hazina vimeo?mtu wako anatoka kwa bwana regardless umewahi au kuchelewa no guarantee ktk ndoa kuna waliowahi sasa hawaishi pamoja kuna waliochelewa vilevile so ni uamuz tuu
 
Back
Top Bottom