Ukichelewa kuoa hadi miaka 40 utapata shida kumpata mwanamke utayendana naye

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Kuna imani flani imejengeka kwa vijana wenye umri kuanzia 25-35 kwamba mwanaume umri wowote anaweza kuoa hata akichelewa hamna shida ataoa it's true kuoa mwanaume lakini kupata mwanamke wa ndoto yake ni ngumu sana

1. At the Age of 40 Kama atapata mwanamke mwenye umri kuanzia 29 hadi 39 hapo lazima apate singo mazaa

2. At the Age of 40 Kama atapata mwanamke mwenye Age kuanzia 24-28 bado wana akili za kula ujana hawa wengi watakupendea pesa zako alafu wanaliwa na vijana wenzao maana wee wanakuona ushakuwa babu mzee

3. Ukipata mwanamke mwenye Age kuanzia 18-24 hawa wengi bado wana childhood age hivyo ukiwa nae kimawazo hamuwezi kufanana maana yee utoto mwingi bado ana akili ya kushinda kwenye vigodoro

4. At this Age of 40 Kama maisha yatakuwa yamekupiga chenga hata ukipata mwanamke mwenye Age of 28-35 ambaye hana mtoto atakula vihela vyako kisha atakukimbia kwa sababu huna maisha

5. At the Age of 40 Kama utabahatika kupendwa na mwanamke basi huyo mwanamke ni Aina ya wale wanawake ambao walikuwa wanajiuza sasa amechoka anafuta kijana mzee wa kumweka ndani

6. At the Age 40 ukiamua kutafuta mke mtandaoni baada ya umri kwenda utaishia kuwatumia hela ya nauli wadada wa mitandaoni na kukimbiwa na wadada

Finally vijana wenzangu kama una binti unapenda naye funga naye ndoa tuu wakati ndo huu ukichelewa chelewa huku mbeleni kuna complications kumpata mwanamke wa ndoto yako au utayeendana naye
 
Hizo ni assumptions zenu tuu kwa vijana wa sasa ambao mnadhani ndoa ni kwa ajili ya mbususu tuu.

Enzi zetu tulioa kwa ajili ya watoto na kuendeleza ukoo. Ndio maana mwanamke kutozaa ilikuwa ni ticket ya kuachwa ASAP!

Sasa endeleeni na ujinga wenu wa kuambizana "Life Starts at 40" muone life litakavyowafanya mkifika miaka 60.
 
Yani katika uzi wa kipumbavu nliowahi kusoma huku JF ni huo upuuzi umeandika hapo juu... unayawekea mapenzi fomula? ... nani amekwambia mapenzi yanakanuni kama hizo unazopotosha nazo jamii?... nimeshuhudia miaka 50 wanaoa, na wanafurahia maisha itakuwa miaka 40?...nmeshuhudia wadada wanaolewa miaka 40+ na wanaume miaka 30 na wanaheshimiana na kupendana vizuri kabisa... fanya utafiti sio unakurupuka kuandika tu vile unajiskia, hii ni Forum ya jamii usipotoshe umma.
 
Kama wewe sio mwanamke acha kuvaa sketi.

Wewe unafahamu vipi sababu za maamuzi ya mwanamke kuchagua kuolewa na mwanaume wa aina na umri fulani?

Ukijisikia kuoa kuolewa na ukapata mtu sahihi unafanya hivyo, hakuna njia maalum ya kupita katika maisha.
 
Napata shida sana kuona vijana mnashindwaje kupata wanawake bora mbona wapo wengi sana na ushahidi wa mabinti wawili tupo nao kazini ni mabinti wazuri, bright na wanayajua maisha, watiifu kweli wanachapa kazi haswa, wanajiheshimu haswa.

Najua wanaweza kuwa na kasoro zao lakini za kinadamu.

Mimi nafikiri vijana mna hofu sana kuliko hofu yenyewe, pia mnasikiliza sana maneno ya mtaani
 
Napatashida sana kuona vijana mnashindwaje kupata wanawake bora mbona wapo wengi sana, na ushahidi wa mabinti wawili tupo nao kazini ni mabinti wazuri, bright na wanayajua maisha, watiifu kweli wanachapa kazi haswa, wanajiheshimu haswa.

Najua wanaweza kuwa na kasoro zao lakini za kinadamu.

Mimi nafikiri vijana mna hofu sana kuliko hofu yenyewe, pia mnasikiliza sana maneno ya mtaani
☝☝ ni dm number mmoja wao ni mpongeze kwa kuwa na tabia nzuri.
 
Napatashida sana kuona vijana mnashindwaje kupata wanawake bora mbona wapo wengi sana, na ushahidi wa mabinti wawili tupo nao kazini ni mabinti wazuri, bright na wanayajua maisha, watiifu kweli wanachapa kazi haswa, wanajiheshimu haswa.

Najua wanaweza kuwa na kasoro zao lakini za kinadamu.

Mimi nafikiri vijana mna hofu sana kuliko hofu yenyewe, pia mnasikiliza sana maneno ya mtaani

Umewahi kujiuliza ni kwa nini hao mabinti wapo tu wenyewe?
 
Kuna imani flani imejengeka kwa vijana wenye umri kuanzia 25-35 kwamba mwanaume umri wowote anaweza kuoa hata akichelewa hamna shida ataoa it's true kuoa mwanaume lakini kupata mwanamke wa ndoto yake ni ngumu sana
Kuoa au kuolewa ni jambo linalozingatia mambo mengi sana na sio umri peke yake.

Unapojikuta umri unakulazimisha kuoa au kuolewa jichunguze zaidi kama una uwezo wa kubeba jukumu la ndoa

Ndoa sio lelemama, ni jukumu zito. Mbali na swala la kumpenda mtu na kutamani kuishi nae pia usisahau kutafuta wewe ni nani? Una karama gani? Uliumbwa na Mungu uje ufanye nini duniani?

Na je, huyo unayempenda anachochea kipawa na karama yako au anaiua?
 
Back
Top Bottom