Ukichaa ni nafsi au akili?

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Katika pitapita zangu nmekuja jua kuwa katika mtu kuna mambo makuu matatu, yaani nafsi, akili na mwili.

Nafsi ndio mtu mwenye kwa maana yu hai hata ukitoka mwili(kufa).

Leo nataka mwenye kujua anijuze; Ni ipi nafasi ya nafsi kwa kichaa katika maisha yake, baada ya akili kwenda mrama. Ni kweli kichaa ni akili au nafsi?.

Pia naomba kujua kichaa usingizini huota akiwa safi au huwa katika ukichaa uleule? Vipi akifa atabakia kuwa kichaa katika ulimwengu wa giza?.

Wajuvi wa mambo haya karibuni.
 
Tungempata Kichaa ambae alipona ingependeza zaidi.

Ila Muumba mwenyewe katika kitabu cha Qur'an kichaa hana dhambi na katika sheria zote za nchi mbalimbali Duniani kichaa ahukumiwi hii inamaanisha ukichaa ni AKILI iliyotoka nafsi inakuwepo palepale ndio maana anaweza kufanya mambo mengine ya msingi especially kula, kuvaa na kulala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kuna vichaa wanazini na kupata watoto bila kufunga ndoa
 
Katika pitapita zangu nmekuja jua kuwa katika mtu kuna mambo makuu matatu, yaani nafsi, akili na mwili.
Nafsi ndio mtu mwenye kwa maana yu hai hata ukitoka mwili(kufa).
Leo nataka mwenye kujua anijuze; Ni ipi nafasi ya nafsi kwa kichaa katika maisha yake, baada ya akili kwenda mrama. Ni kweli kichaa ni akili au nafsi?.
Pia naomba kujua kichaa usingizini huota akiwa safi au huwa katika ukichaa uleule? Vipi akifa atabakia kuwa kichaa katika ulimwengu wa giza?.
Wajuvi wa mambo haya karibuni.

Mimi mchango wangu hautojibu moja kwa moja, isipokuwa utashauri namna bora ya kujibu hoja zako.Ninachoshauri ni kuwa swali lako halitokuwa na jibu moja, maana itategemea linajibiwa kwa mtazamo gani.Kwa mfano:

1.Je, anaejibu anatumia sayansi asilia, mfano, Baiolojia ?
Ikiwa atatumia mtazamo huu kwa dhati yake,basi itabidi masuala ya maisha baada ya kifo kifo tuyaondoe kwenye swali lako. Pia, sidhani kama Baiolojia inaamini dhana ya nafsi.

2.Je, anaejibu anatumia Saikolojia? Hapa maisha baada ya kifo yanaweza kuingia, japo si lazima yatumike kama ukweli, maana itategemea na fikra za mtu na jinsi anavyotafsiri. Mengi ya haya hujitengenezwa kwenye vichwa vyetu kadiri tunavyofundishwa na mazoea katika jamii.Masuala kama kulogwa yanapatikana hapa.

3.Je, anaejibu anatumia imani na vitu vya kufikirika zaidi, yani metafizikia? Hapa sasa vingi vinawezekana. Hivyo, mitazamo miwili tajwa hapo juu, inaweza kuwepo hapa lakini kwa mtazamo tofauti kidogo. Wakati Baiolojia inamtazama mwanadamu kama umbo fulani linaloweza kuteketea sasa hivi na kuwa mbolea, metafizikia inakwenda mbali zaidi, kwamba ukiacha umbo tulionalo , pia kuna upande wa kiroho. Sote tunafahamu katika dini au imani fulani chochote kinawezekana maana hapa maumbile na zaidi ya maumbile (metaphyisics) hukubalika. Hapa maisha baada ya kifo yapo.

Hii ni baadhi ya mikabala inayoweza kutumika kutoa majibu, sidhani kama ni rahisi kuongea kijumlajumla hivyo. Ukijaribu kuongea kiujumla utajikuta unapata maswali mengi ukakosa majibu.
 
Ni kweli mtu yupo katika hali tatu, lakini natofautiana na wewe katika kuzitambua hizi hali. Binadamu ni Roho, Nafsi na Mwili.

Roho:

Mwanzo 1:26-27 (na tufanye mtu kwa mfano wetu...), andiko hili linaonesha jinsi ambavyo Roho iliumbwa, ndiyo maana imeandikwa kuwa wote, mwanamume na mwanamke waliumba siku moja, hii kwa sababu uumbaji wa roho ulifanywa siku moja. Wengi wamekuwa wakipotosha kuhusu andiko hili wakidai kuwa huyu mwanamke aliyeumbwa hapa si Hawa ila kulikuwa na mwanamke mwingine jambo ambalo si kweli. Kwa mwanadamu, Roho (au ulimwengu wa roho) ni sawa na soft copy (Roho), ambayo huandaliwa kabla ya priting (kuumbwa kwa mwili), ambapo ndipo utapata hard copy (Mwili).

Roho husimamia mambo yote ya ndani ya mtu kama ya ibada iwe za Kimungu au kishetani, mapokeo ya karama na vipaji mbalimbali, kuandaa mawazo, ndoto, udadisi, ufahamu, tafsiri mbalimbali n.k. Roho haiwezi kufa, kwani ndiyo nguvu na mfano wa Mungu (Uungu) na hurudi kwa Mungu baada ya mwili huu kufa.

Nafsi:

Mwanzo 2:7 inaonesha jinsi ambavyo Nafsi ya mtu iliumbwa. Nafsi husimamia mambo 3. (1) Hisia (kuchukia, kufurahi, kusikitika, kupenda n.k.); (2) Nia (namna tunavyofikiri); (3) Utashi (namna tunavyoamua).

Mwanadamu mmoja anahusiana na mwingine kwa nafsi yake, unapokuwa kwenye uhusiano na mtu hisia zako, nia yako na utashi wako huunganishwa na mtu huyo. Ndiyo maana ukishaingia kwenye uhusiano basi hata kufikiri au kuamua kwako hubadilika... Ndiyo maana ukiingia kwenhe uhusiano usio sahihi basi hata kufikiri kwako, kuhisi na kuamua kwako kunavurugwa, wakati mwingine utatamani usifikiri au usiamue namna unavyoenenda lakini unakuwa hujui utajinasuaje.

Hata hivyo, nafsi ndiyo mfasiri (interpreter) wa yaliyopo rohoni kwenda kwenye mwili au ya mwilini kwenda rohoni. Nafsi inaweza kufa.

Mwili:

Mwanzo 2:7 (Mungu akamuumba mtu kwa mavumbi). Mwili huhusisha mambo yote ya nje (ya ulimwengu). Mwili pia husimamia mambo 3: (1) Utambuzi (hali ya kibinadamu ya kupokea habari kwa njia ya ufahamu); (2) Urejeshi "reaction" (hali ya kutenda kutokana na kutendewa, iwe kwa maneno au matendo; (3) Udhihirisho (hali ya mwili kutoa habari za ulimwengu kwa mawazo, kujisikia au maamuzi ya nafsi. Mwili unakufa na kurudi mavumbini ulikotoka.

Sasa swali la kujiuliza, mtu anapopata matatizo ya kiakili (ukichaa, msongo wa mawazo n.k.) ni nini kinachokuwa kimepata shida? Kwa maelezo yangu nadhani jibu lipo wazi kabisa...

Ahsante mkuu nimeongeza ki2, God bless u
 
Tungempata Kichaa ambae alipona ingependeza zaidi.

Ila Muumba mwenyewe katika kitabu cha Qur'an kichaa hana dhambi na katika sheria zote za nchi mbalimbali Duniani kichaa ahukumiwi hii inamaanisha ukichaa ni AKILI iliyotoka nafsi inakuwepo palepale ndio maana anaweza kufanya mambo mengine ya msingi especially kula, kuvaa na kulala

Sent using Jamii Forums mobile app
It means nafsi na roho ndizo zinazoathiriwa
 
Mimi mchango wangu hautojibu moja kwa moja, isipokuwa utashauri namna bora ya kujibu hoja zako.Ninachoshauri ni kuwa swali lako halitokuwa na jibu moja, maana itategemea linajibiwa kwa mtazamo gani.Kwa mfano:

1.Je, anaejibu anatumia sayansi asilia, mfano, Baiolojia ?
Ikiwa atatumia mtazamo huu kwa dhati yake,basi itabidi masuala ya maisha baada ya kifo kifo tuyaondoe kwenye swali lako. Pia, sidhani kama Baiolojia inaamini dhana ya nafsi.

2.Je, anaejibu anatumia Saikolojia? Hapa maisha baada ya kifo yanaweza kuingia, japo si lazima yatumike kama ukweli, maana itategemea na fikra za mtu na jinsi anavyotafsiri. Mengi ya haya hujitengenezwa kwenye vichwa vyetu kadiri tunavyofundishwa na mazoea katika jamii.Masuala kama kulogwa yanapatikana hapa.

3.Je, anaejibu anatumia imani na vitu vya kufikirika zaidi, yani metafizikia? Hapa sasa vingi vinawezekana. Hivyo, mitazamo miwili tajwa hapo juu, inaweza kuwepo hapa lakini kwa mtazamo tofauti kidogo. Wakati Baiolojia inamtazama mwanadamu kama umbo fulani linaloweza kuteketea sasa hivi na kuwa mbolea, metafizikia inakwenda mbali zaidi, kwamba ukiacha umbo tulionalo , pia kuna upande wa kiroho. Sote tunafahamu katika dini au imani fulani chochote kinawezekana maana hapa maumbile na zaidi ya maumbile (metaphyisics) hukubalika. Hapa maisha baada ya kifo yapo.

Hii ni baadhi ya mikabala inayoweza kutumika kutoa majibu, sidhani kama ni rahisi kuongea kijumlajumla hivyo. Ukijaribu kuongea kiujumla utajikuta unapata maswali mengi ukakosa majibu.
Ahsante mkuu, ubarikiwe
 
Kuna ukichaa unaotokana na mwili (ubongo) na unaotokana nafsi. Ukichaa wa mwili unasababishwa na hitilafu mbalimbali kwenye ubongo na external factors (environmental) nyingine.
Ukichaa wa nafsi unasababishwa na mambo yanayo husiana zaidi na conscious na sub conscious. Kama mtu alifanya kitu kibaya sana lazma aanze kusutwa na nafsi na hivyo hupatwa na ukichaa. Au hata kama mtu aliwahi kuexperience mambo mabaya sana akasahau, bado sub conscious yake itakuwa imehifadhi na ataanza kupata ukichaa.
 
Ahsante mku japo you're explaining is too short
 
Katika pitapita zangu nmekuja jua kuwa katika mtu kuna mambo makuu matatu, yaani nafsi, akili na mwili.
Nafsi ndio mtu mwenye kwa maana yu hai hata ukitoka mwili(kufa).
Leo nataka mwenye kujua anijuze; Ni ipi nafasi ya nafsi kwa kichaa katika maisha yake, baada ya akili kwenda mrama. Ni kweli kichaa ni akili au nafsi?.
Pia naomba kujua kichaa usingizini huota akiwa safi au huwa katika ukichaa uleule? Vipi akifa atabakia kuwa kichaa katika ulimwengu wa giza?.
Wajuvi wa mambo haya karibuni.
Ukichaa ni hali ya ubongo kubadilisha au kuwa na frequency tofauti na binadamu wa kawaida. Mfano akili zinaweza kuwa na frequency za mbwa hapo utakuta muhusika anazunguka tu majalalani, ndio maana vichaa hutofautiana kulingana na frequency walizobadolishiwa.
 
Mkuu kwa faida tueleze kiundani kdogo
 
Kisayansi zaidi ukichaa ni akili..hakuna cha nafsi wala nini
Mtu kuwa kichaa nati zinakuwa zimelegea tu kichwani..

na kuhusu ndoto ,mtu huota anachokiexperience akiwa macho..sasa kichaa kama anaona fisi badala ya watu hata kuota ataota fisi tu..

Na kuhusu kufa kisayansi ukifa umekufa brain inaoza moyo unaoza kwahio hakuna kichaa baada ya kufa wala genius wote ni uozo tu

Ahsante mkuu kwa kunijuza
 
*Kifuatacho*

Kwa yule ambae hafahamu jina sahihi la mlemavu sasa naomba afahamu hivi

Kipofu............ *asiyeona*

Zeruzeru, mlemavu wa ngozi........ *albino*

Asiyesikia........... *kiziwi*

Kichaa............. *mwenye ugonjwa wa akili*

Zezeta,taahira............................... *mwenye ulemavu wa akili*

Kifafa................ *mwenye kifafa*

Mbilikimo......... *mwenye umbile fupi*

Kilema............ *mlemavu*
Kiwete.......... *mlemavu wa viungo*

Tukumbushane kutumia majina sahihi
 
Kisayansi zaidi ukichaa ni akili..hakuna cha nafsi wala nini
Mtu kuwa kichaa nati zinakuwa zimelegea tu kichwani..

na kuhusu ndoto ,mtu huota anachokiexperience akiwa macho..sasa kichaa kama anaona fisi badala ya watu hata kuota ataota fisi tu..

Na kuhusu kufa kisayansi ukifa umekufa brain inaoza moyo unaoza kwahio hakuna kichaa baada ya kufa wala genius wote ni uozo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Na mtu akiota ndoto za kutisha kwenye mazingira ya ajabu ajabu au ameota amekufa anakuwa ame experience hicho kitu akiwa macho?
 
Kila siku tunaona watu wanakufa mkuu.
Sio lazima unachokiota uwe umekiexperience wewe hata kama uliona tu au una hio idea...huwezi kuota (never) kitu ambacho huna idea kabisa..

Mfano hata ukiota umekufa umeenda mbinguni basi mbingu itakuwa na watu unaowafahamu au mazingira yske yatakuwa ya kibinadamu mf kutakuwa na nyumba labda treni n.k

Lakini huwezi kupaota mbinguni halafu ukaanza kuona vitu ambavyo hujawahi kuviskia wala kuimagine ukiwa macho..hio ni impossible.

Sometimes ndotonk unaweza kuona sura mpya kabisa ya mtu..lkn jiulize ni watu wangapi ulishaona sura zao tangu unazaliwa?? Kwahio hio sura mpya ni moja ya sura ulizoziona lkn ukasahau but the brain has a place for such memories

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom