Ukibembeleza kidonda hakiponi, UKAWA/CHADEMA hawasikii ushauri

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Hivi sasa Nimeudhika sana na Mwenendo wa Siasa Nchini, Kiasi Kwamba Nafikiri Kabisa Kuacha Kutoa mawazo na Malalamiko ya Jumla jumla. Ni bora nifanye Siasa za Behind the Scene kwa lengo la Kusaidia Nchi. Na kuondokana Kabisa na Kuegemea Kwa Vyama.

Nilikuwa Nimekaa na Siri yangu Moyoni, Lakini Ukweli Ni Kuwa Mimi Sio Mwanachama wa Vyama vya Ukawa wala CCM, Wakati wa Uchaguzi Mimi Nilitaka CCM iondoke Madarakani Sio tu kwa Mawazo Narrow ya Kudhani CCM ni Mafisadi, ila kwa Kutaka Kuwe na equilibrium ya Kisiasa na Kusiwepo na Chama Kinachojiaminisha vyovyote iwavyo watashinda tu. Sikutamani, na Sitamani CCM ife, haitakuwa Jambo zuri Kisiasa wala Kimaendeleo kwa Taifa Letu. Ila Nilitaka CCM baada ya Kuwa Madarakani Miaka hamsini wakae pembeni. Na bado Nataka Hivyo.

Ikatokea Jinsi ilivyokuwa Process ya Kupata Mgombea wa CCM, Mara tu Baada ya Kukatwa Lowassa Nikaona UKAWA wanaweza Kutumia Mwanya huo kwa advantage yao na ya Kutimiza Lengo la Kuitoa CCM.

Nilijua Wabunge na Viongozi wa CCM hawatakuwa Kamakazi wa Kuacha Mustakabali Binafsi Kumfuata Lowassa Kwani Kwa Wengi siasa ndio Maisha. Sikujua Magufuli angepita ingawa Nilimpenda sana. alipopita Nikawa Njia Panda, Lakini Nikaamua CCM hata angekuwa Ni nani Ni bora Ikae pembeni Kwanza. Hivyo Nikaamua Nisaidie Niwezavyo Kuleta Mabadiliko ya Kisiasa. Nilimjua Player mmoja tu, lakini wengine wote hawanijui, Sio Mbowe wala Lowassa anayenijua.

Nikajitahidi Kuwatafuta Ikawa Vigumu. Nilikuwa Na Michango ya Policy na Approach ya Kampeni. Nikawatafuta Mbowe kwa Simu sikumpata, Nishauriwa na Secretary wake Nitume Proposal Zangu Nikafanya Hivyo, Lakini hakukuwa na feed back. Nikajiamulia Mwenyewe Kuwa Nitajitolea Hivyo Hivyo Kusaidia Niwezavyo ila dharau zao Ziliniudhi sana. Proposal zangu Zilikuwa Ni Nini?

1) Kupiga kampeni ambayo Inagusa Matatizo ambayo yalikuwa Ni kero sana Kwa Wanachi Mfano (a) Wagonjwa Kulala chini (b) Wajawazito kukosa Dawa (c) Wanafunzi Kukaa chini na Kukosa vifaa vya Elimu (d) Kukosa ajira kwa Vijana (e) Polisi Kunyanyasa Raia na Rushwa Mahakamani etc. (f) Kutilia Mkazo Viwanda vya Kusindika Mazao (g) Kuzidisha Ununuzi wa ndani Katika Miradi na Mahitaji yanayohudumiwa Moja kwa moja na serikali kuu mfano, Kutoagiza Nguo, Viatu na silaha ndogo za Majeshi yetu Kutoka Nje, Mfano wa Pili Ni Kutumia Malighafi na Nishati zetu Katika Miradi Mikubwa, eg Barabara za Zege badala ya lami, Na Kutumia zaidi Gesi ya songosongo katika Magari na Vifaa vya Ujenzi na Kilimo badala ya Kutegemea Diesel kutoka nje. Na Mengine Mengi ambayo Naweka siri kwa sasa.

2) Proposal ya Jinsi ya Kupata mapato ya Kugharimia Elimu Bure. Mfumo ambao Ungekuwa Ni Practical na Usiogusa Kabisa Vianzio Vingine vya mapato. Hilo naliweka Siri, Ila Nitalifikisha kwa Mhusika Mwingine. The progress of our children cannot be put on hold for political reasons.

3) Kisiasa Niliwashauri Wafanye Mawasiliano Ya Siri Na wale Wabunge wote wa CCM ambao walikuwa Na Lengo la Mabadiliko lakini wanahofia Kupoteza Ubunge wao. Wangewaahidi Kuwa Wangewapitisha Kwenye Majimbo yao na Wasingewawekea Mpinzani Mwingine.

3) Kuchangisha fedha na Kusitumia Katika Kulipa watu au Mtu Mwenye Taarifa za Siri za Hujuma Dhidi ya Ukawa Kabla hazijatokea. Hata Polisi mataifa ya nje wanalipa Kupata tips za Uhalifu unaotaka Kufanyika au uliokwisha kufanyika kumpata suspect.

Mwisho Nilisisitiza sana Kuwa Lowassa aandaliwe Speech ya Kusoma wakati wote kwa Kuwa Pamoja na Kuwa Ni Kiongozi Mzuri, na Makini sio Msemaji na Ndio Maana alipokuwa hawezi kusema mengi dhana ya Kuwa alikuwa ni Mgojwa mahututi iliaminiwa kwa makosa ya Ukawa na Lowassa Mwenyewe Kwa Kiasi Kikubwa. Ikumbukwe Lowassa Katika Hotuba ya Kufunga Kampeni alisoma hutuba, ilikuwa the best of the best, lakini Niliamini ni too little too late.

Na sasa Niliwatafuta Kuwashauri, Watoe fedha Katika Mfuko wao na Pia Wachangishe Fedha kwa Wanachama, wapate Kama Bilioni 5 Kutoa Mtaji kwa OCD yeyote atakayejiuzulu Kupinga Kutumiwa na CCM. Hawasikii

Nikirudi Nyuma baada ya Kuona Hakuna Feed back nikaamua Nisaidie Kivyangu Kusema yale Niliyoyaamini Katika Kampeni. Na Muda wote Nilijitahidi Kuonyesha heshima kwa Magufuli na wote ila tu pale Nilipotumia Makosa yao ya Kimatamshi au kimkakati kuwapunguza Makali yao. Hii ni mbinu safi Kisiasa inatumika kote Duniani Tofauti na Matusi.

Huu Ni Mfano wa Kampeni zangu wakati Ule.





Nimeweka Video Hizi Ili wajuwe anayewasema sio Adui yao ila Ni anayewatakia Mema. Hata Mh Magufuli sio adui yangu, Ni Mtu mwema sana kwa asilimia 90% When it comes kutaka kubadilisha nchi yetu. Ila Namtaka Akamilishe asilimia 90% ya Uchapakazi wake, na Ukali wake, kwa Kuweka hiyo asilimia 10% ya Kutenda haki za Kisiasa, Atatisha Dunia Nzima!
 
Back
Top Bottom