Ukibahatika kukutana na Rais Samia utamuuliza swali gani la msingi?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamiiforums

Ukibahatika kukutana na Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

fgthbv.jpg


Rais wa sasa wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu ni mwanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapa nchini Tanzania. Alikuwa mbunge wa jimbo la Makunduchi visiwani Zanzibar kuanzia 2010 hadi 2015, na alikuwa waziri wa nchi anaeshughulikia muungano katika muda huo.

Samia Suluhu Hassan ndiye makamu wa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania. Kabla ya kuwa Rais kutokana na kifo cha Rais John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, Suluhu alikuwa makamu wa Rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo hicho, akarudia baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2020.

SWALI: Ukibahatika kukutana na Rais Samia "face to face" utamuuliza swali gani la msingi?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Sioni kama kuna swali lolote la maana anaweza kulijibu sasa, sana sana baada ya siku 100 wangalau anaweza kuulizwa swali la maana. Hii mada yako ni nzuri, ila imewahi sana maana yuko kwenye hatua za awali za kuishape serikali yake.
 
Kwani kazi ya Rais ni kuulizwa tu Maswali? acheni uzwazwa... Mwambieni atekeleze tu Majukumu yake ipasavyo na asimamie haki ikiwemo ya Masheikh wa Uhamisho... na aunde tume ya kuchunguza watu walipotea au kupotelewa na ndugu zao bila kufahamika
 
Maswali matano
1. Bunge lini unavunja?
2. Katiba mpya lini na tume huru?
3. Why wakwapuzi wa fedha baada ya msiba wasinyongwe kama uthibitisho upo wazi?
4. Katiba na vyama vya siasa iko vipi?
5. Anajisikiaje kuwa Rais wa kwanza mwanamke tz, na vipi genge lile lataka yeye pitia njia za mtangulizi wake anaona wako sawa?
 
Nitasema

Nitamwambia Mheshimiwa Rais ! Ulivyoanza ndo tunakuombea umalize 2030 kwa mwendo huo huo. Inawezekana kuongoza bila kuwa mkorofi na kurekebisha bila kutoka mapovu.
Kaisome katiba vizuri ndio uje uandike hapa.
 
1. Ni lini wabadhirifu wa mali za Umma waliotajwa na ripoti ya CAG watafikishwa mahakamani na kurudisha kodi zetu ?
2. Mchakato wa katiba mpya utaanza lini ?
 
Zanzibar ina changia shilingi ngapi kwenye kuendesha serikali ya muungano? ikiwemo Mshahara, Per diem, Statutory payments anazopata yeye mheshimiwa Rais na wasaidizi wake
 
1. Atafanyaje kuifanya Tanzania iwe imejaa vijana wenye maarifa ya kisasa ya ufundi, ufugaji na kilimo na hivyo kuweza kujiajiri au kuajirika kirahisi?

2. Atafanyaje kuhakikisha anaweka mazingira bora kwa biashara kuanzishwa na kuboresha ukusanyaji wa kodi?

3. Atafanyaje kuhakikisha wala rushwa, wahujumu uchumi na nk. hawastawi kipindi cha uongozi wake na kuchukuliwa hatua zinasostahili ili iwe funzo kwa wengine?

4. Atafanyaje kuhakikisha wazembe, wavivu na wasaidizi wake wasio wabunifu, ambao wapo wapo tu wanashughulikiwa?
 
Mimi binafsi kwa sasa naomba nikiri kwa uhakika kabisa kuwa ninayo mengi mno na ya msingi sana ya kumweleza, mengi tu na ikitokea nikabatika kupata nafasi hiyo ya kukutana naye nitafurahi sana. Aliyepita nilikuwa nasita kidogo kutafuta nafasi ya kukutana naye kutokana na ukweli kuwa origin yake na yangu vina uhusiano wa karibu kidogo.

Kwa hiyo mimi nikibahatika kukutana naye sitamuuliza maswali, bali nitamweleza mambo kadhaa ya msingi niliyonayo moyoni
Ubarikiwe sana kwa wazo zuri mno
 
Back
Top Bottom