Ukibahatika kukutana na IGP utamshauri nini kuhusu jeshi la Polisi?

  1. Kikosi chake cha usalama barabarani kimekithiri kwa rushwa na yeye hayupo tayari kuamini hilo kwakuwa siyo mhanga wa mambo yanayotokea barabarani
  2. Kitengo cha cyber crime na hasa kwa simu za wanaoibiwa na kufikisha taarifa police, hakuna msaada wowote, zaidi ya kuzungushwa makoridoni na kuombwa rushwa kwa kisingizio cha uchunguzi kutokamilika




Word!!!
 
Traffic waache kuonea watu barabarani.Mbona enzi za Kikwete tulikuwa hatusumbuliwi barabarani?
Wewe mtu una driving licence, una kadi ya gari, unafunga mkanda,una bima,una triangle na kila siku lazima ukamatwe na upigwe faini.
 
Dah! Trafiki wanaonekana kuongoza kwa kukera watu.
 
Asaidie mabadiliko katika utaratibu wa jeshi la polisi kukamata wezi wa simu kwa kutumia teknolojia waliyonayo,uweledi na utashi.
Kwa sasa utashi wa Cybercrime unit kukamata mtu aliyeiiba simu na kuiflash na kuiuza au kuweka simcatd ingine hakuna kabisa labda awe ni muheshimiwa, ahonge.

Na inabidi kampuni za simu zisaidie hili suala wapo watalii na wawekezaji wanaibiwa simu zao ambazo unakuta mtu amehifadhi documents zake zote anaporwa na pikipiki njianj halafu akiripoti inageuka cold case. Tunatia aibu kama taifa na jeshi letu likikamata wezi wa simu na laptops basi tutapunguza hamu ya vibaka kuiba bidhaa hizi
 
Kitengo Cyber walau ngazi ya mkoa viboreshwe, wapewe vitendea kazi na access wahusika TCRA na makampuni ya simu.Ni aibu na ajabu inakuwa ni hisani na juhudi binafsi CID cyber,afanye mawasiliano binasfsi( Kwa ahadi malipo ,tip) na mdau wake TCRA ama kampuni ya simu,kupata taarifa!
 
Nitamshauri awafundishe adabu hawa polisi watoto wamekua wasumbufu sana vinginevyo wataendelea kupigika sana juzi wengine huku wamelia kama watt wanakataa sisi sio polisi jamaa wakauliza na hizi pingu mmetoa wapi wakabaki wanalia tu, sasa weekend hii mtaani hatujahema
 
Back
Top Bottom