Ukibahatika kukutana na IGP utamshauri nini kuhusu jeshi la Polisi?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Pengine haya mambo huwa hayamfikii Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi lakini kiukweli kumekuwa na chuki kubwa sana ya wananchi kwa
Jeshi hilo.

Siku ukibahatika kukutana na Mkuu huyo Utamweleza au kumshauri
nini kuhusu Jeshi la Polisi kwa kuzingatia eneo ulilopo na mengine
unayoyafahamu kwa Ujumla?

Je! Kuna afisa yeyote wa Jeshi la polisi au Polisi wa kawaida ambaye
amekuwa anafanya mambo kinyume na utaratibu na umeamua kumfikishia IGP?

Wakuu hebu tufunguke pengine Mkuu huyo anaweza kupita huku baadhi ya
mambo yakakaa sawa.
 
Ningemshauri aanzishe vitengo vifuatavyo:

1. baby police- watoto wa kipolisi waandaliwe kwa kufundwa tangu wakiwa wadogo kuhusu usalama wa raia na mali zao.
Watoto hawa wachaguliwe kwa ustadi mkubwa wa kiusalama,

faida zake ni kuwa watakuja kuwa askari polisi wanaoipenda sana kazi yao maana wameizoea toka utotoni.

2. Cyber and Economical police, hawa watokane na baby police, yaani wakishakuwa wakubwa wakuweza kuanza elimu ya msingi bhasi waelekezwe na kusaidiwa kusoma zaidi masomo ya sayansi na uchumi kwa ajili ya kuja kukabiliana na uhalifu wa kimtandao na kiuchumi hasa ule unaofanyika ktk mabenki na taasisi mbalimbali za kifedha.

NI HAYO TU KWA LEO.
 
  1. Kikosi chake cha usalama barabarani kimekithiri kwa rushwa na yeye hayupo tayari kuamini hilo kwakuwa siyo mhanga wa mambo yanayotokea barabarani
  2. Kitengo cha cyber crime na hasa kwa simu za wanaoibiwa na kufikisha taarifa police, hakuna msaada wowote, zaidi ya kuzungushwa makoridoni na kuombwa rushwa kwa kisingizio cha uchunguzi kutokamilika
 
Polis waongezewe uwezo wa Martial art's manake wapo kizembe sana na wanadharaulika sana
 
Tamshauri Aboreshe mafunzo ya polisi,aboreshe vyuo viwe vya kisasa,Tamshauri suala la upandishaji vyeo uzingatie elimu na utumishi uliotukuza,tamshauri aboreshe maslahi ya Polisi,tamshauri kuwe na subdivions ambazo zitaongozwa na task team ambayo iundwe na idara mbali mbali,pili tamshauri suala la maboresho ya PGO(Police General Order)
 
Namshauri atumie nguvu kupota kiasi kwenye uchaguzi wa Kinondoni kinyume na hapo Jumbo linabaki lilipokua
 
Pengine haya mambo huwa hayamfikii Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi lakini kiukweli kumekuwa na chuki kubwa sana ya wananchi kwa
Jeshi hilo.

Siku ukibahatika kukutana na Mkuu huyo Utamweleza au kumshauri
nini kuhusu Jeshi la Polisi kwa kuzingatia eneo ulilopo na mengine
unayoyafahamu kwa Ujumla?

Je! Kuna afisa yeyote wa Jeshi la polisi au Polisi wa kawaida ambaye
amekuwa anafanya mambo kinyume na utaratibu na umeamua kumfikishia IGP?

Wakuu hebu tufunguke pengine Mkuu huyo anaweza kupita huku baadhi ya
mambo yakakaa sawa.

Askari wake wa Kiume waache kuvaa Nguo zinazowabana, halafiu njiwa ( namaanisha fupi miguuni ) na zilizopauka. Askari wa Kike ajitahidi awashauri waache kuwa wepesi ' kutongozeka ' na ' Kubaiolojika ' humu mitaani. Haya ndiyo ambayo ningeonana na IGP Sirro ningemfungukia mbele yake mubashara na mujarab kabisa.
 
Yeye ndio abahatike kukutana na mini ......alaf ndo ntamshauri watafute njia nyingine ya kuwapata vijana wanao jiunga na jeshi polisi maana saiz wengi wanao jiunga ni kwaajili ya ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira na sio kwa mapenzi ya dhati katika kulinda mali za raia na usalama wao ndomana rushwa haita isha na polis maadili yanashuka askari masharo baro askar anavaa nguo inayo mbana mara askar anatumia nguvu nyingi pasipo hitaji nguvu na mengine meeeengiiii. ....nikikumbuka zamani tulikua tukimuona pilisi tunakimbia hatakama hatunakosa ila saiz watoto wakimuona polisi wanaona kama mwanafuzi wa sekondali katoka shule
 
Back
Top Bottom