Ukiachwa unajisikiaje?Acha kabla ya kuachwa

Ambition plus

JF-Expert Member
Feb 23, 2018
4,198
2,000
Angalizo sizungumzii wana ndoa.

jamani swalamaaaaa?
Kheri ya kuzaliwa Yesu kristo na mwaka mpya....

Leo yamenikuta.Hua nina katabia flani ka kuacha kabla sijawachwa.
Nikiona binti kaanza kubadilika labda vitabia vya ajabu .Naaza uchunguzi wangu mara moja.Nikiona vigezo vimekamilika naachia mzigo kwa amani tu.Wako mabinti ambao nimewahi kuwaacha lakini bado nilikua nawapenda sana."Unajua ile unampenda mtu alafu unamwacha"INAUMA SANA ila inabidi.

Na binti "akiniacha" haijalishi ni muda gani nitabembeleza turudiane ili na mimi "nikubwage".Hakuna faida ninayopata kwa kufanya hivo zaidi ya kujisikia "aman ndani ya nafsi"

Nilikua na binti mwenye asili ya Zanzibar+oman.Mwislam swafi.Tulidumu kwenye mapenzi.Tokana na mapenzi na kupenda.Nikawa namwadithia kwamba ikitokea amebadilika nitamwacha mimi kwanza.Akasema haiwezekani.Ukiniacha wewe nitakubembeleza tutarudiana nitakuacha.Masiharamasihara ikaisha.

Mwaka jana akaanza dharau baada ya kupata warabu wenzie.
Sikuchukua round nikampiga chini.Tukawa kama maadui.

Baadae akarudi oman.Kakaa kama miezi sita naona namba sielewi whatsap.Tukawasiliana sana.Akanza kujirudisha.Kanibembeleza sana.Siku karudi tukaonana.Tukafanya yetu.
Baada ya hapo hahaha kanibwaga.

Inauma sana...kanikomesha

Ukiachwa ama ukiacha unajisikiaje?
Tupeane uzoefu.
Ila kuachwa hakuna uzoefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,573
2,000
Aki kublock kwenye social media badilisha user name muombe urafiki aki accept tu na wewe unamblok hapo tuliozoea jiji tunasema ngoma droo na tunaset mambo mengine yaende kwenye mtandao
 

Ezekiel Mbaga

JF-Expert Member
May 28, 2018
9,401
2,000
me hua nna principle ya ku-balance shobo zangu.

nshawahi kuwa na demu, kila kitu namfanyia lkn hakuwahi kurudisha shukrani hata kwa neno asante.

nkajisemea mwenyewe, bora nkae pembeni japokuwa nilikuwa naumia sana baada ya kujiweka pembeni lkn ilikuwa afadhali kwangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom