Ukiachana na Mbowe, Wanachama wengine wa CHADEMA wenye siasa za Kistarabu ni Mchungaji Msigwa na John Mnyika

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,160
1,493
Mheshimiwa Mbowe ni Mwanasiasa mkongwe wa Siasa za Upinzani, hakuna ubisihi kwa sasa anaamini kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mh. Samia Suluhu Hassan inawapeleka Watanzania kwenye ile nchi ya ahadi yenye Asali na Maziwa.

Mchungaji Msigwa na Mh John Mnyika ni Wapinzani wanaoamini siasa sio kupinga tu au kutukana matusi, mara nyingi Mchungaji Msigwa amekuwa akipongeza Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo unaofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, japo kila akiongea ukweli na kupongeza amekuwa akiambulia matusi na kubezwa na vijana walioingia Chadema juzi ambao wao Siasa ni kukukana tu.

Ndugu yangu Mchungaji Msigwa, Siasa ni Sayansi, na Kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye Mwanasayansi bora kabisa wa siasa, ameweza kuwatuliza Wapinzani kisayansi kwa kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa kiwango cha juu, Watanzania wamekubali mziki wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mchungaji Msigwa, Karibu CCM, tuijenge Iringa yetu, njoo tuunge juhudi za Mwanasayans wa Siasa bora kabisa, Chadema sio mama yako wala baba yako, Umetukanwa vya kutosha na watoto wadogo kwa misimamo yako ya kusimamia ukweli .

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Ungekuwa una akili ungejua kuwa wanachadema wote ni watu wastaarabu kabisa. Vinginevyo kwa hali ilivyo kwa miaka hii michache iliyopita na matendo mnayo watendea mngekuwa mnaambulia vipigo kutoka kwao huko mitaani maana Chadema ina vijana wengi wenye afya timamu kabisa tofauti na CCM iliyo jaa mateja na wazee
 
Nakubaliana kuwa mchungaji Msigwa ni mwanasiasa mzuri na mstaarabu, na mimi namwomba aendelee hivyo hivyo. Sikubaliani na wazo la kumtaka ajiunge ccm, hasa ccm hii ya akina mzee ndovu. Aendelee kubaki huko huko chadema, kama itaendelea kuwa hai. Vyama vya upinzani vinahitaji wanasiasa logical kama mchungaji Msigwa ili kuvilea na kuvikuza. Kwenye upinzani wanahitajika wanasiasa wanaoweza kujenga hoja na zikakubalika na wanachama wao, independents, na hata wanaccm wasio wahafidhina. Mch Msigwa ndiye hope pekee iliyobaki ya kuiokoa chadema kwa sasa.
 
Mkuu UmkhontoweSizwe unataka abaki huko aendeleee kutukanwa matusi na vijana ambao hawajui hata Chadema imetoka wapi, my brother Msigwa ushauri huu sio sahihi, ukishindwa kurudi CCM, nenda hata kwa mdogo wako ZZK mkaendeleze siasa za kistaraabu.
 
..sasa kwanini Polisi wa Ccm wanawasumbua Msigwa na Mnyika wanapofanya shughuli au kazi za kisiasa?

Mkuu JokaKuu mbona Jeshi la Polisi limetoa sababu ni nini? Ukiomba upite njia A then baadaye hutaki kupita njia hiyo lazima utoe taarifa. Lazima tuendeshe mambo kwa utaratibu
 
Ungekuwa una akili ungejua kuwa wanachadema wote ni watu wastaarabu kabisa. Vinginevyo kwa hali ilivyo kwa miaka hii michache iliyopita na matendo mnayo watendea mngekuwa mnaambulia vipigo kutoka kwao huko mitaani maana Chadema ina vijana wengi wenye afya timamu kabisa tofauti na CCM iliyo jaa mateja na wazee

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Mkuu Chakaza Kama kutukana matusi na kupinga kila hata lililo jema ni ustaarabu, basi bado hujajua maana ya ustarabu.
 
Mkuu UmkhontoweSizwe unataka abaki huko aendeleee kutukanwa matusi na vijana ambao hawajui hata Chadema imetoka wapi, my brother Msigwa ushauri huu sio sahihi, ukishindwa kurudi CCM, nenda hata kwa mdogo wako ZZK mkaendeleze siasa za kistaraabu.
Mkuu, sidhani kama itakuwa sahihi kwa yeye mwanachama mkongwe wa chadema kukimbia chama chake eti kwa sababu anakimbia matusi. Strong leaders ni wale wanaoweza kusimama hata wakati mambo hayaendi vizuri.
Hao vijana watukanaji wengi wao ni wa kuja ndani ya chadema, naamini ni wimbi tu la muda ambalo litapita. Chadema asilia siyo chama kilichojengwa kwenye matusi, chadema ninayoijua mimi ni chama cha hoja. Inahitaji viongozi kama mch Msigwa kusimama na kuirejesha kwenye misingi yake ya mwanzo.
Kama unamshauri aondoke ili chadema iendelee kuporomoka kwa urahisi na hatimaye kuwa kama nccr na cuf, basi afuate ushauri wako.
 
Mkuu JokaKuu mbona Jeshi la Polisi limetoa sababu ni nini? Ukiomba upite njia A then baadaye hutaki kupita njia hiyo lazima utoe taarifa. Lazima tuendeshe mambo kwa utaratibu

..inawezekana Polisi wanasema ukweli lakini kuna HISTORIA mbaya na ya muda mrefu ya wapinzani kuonewa na kudhulumiwa ktk nchi yao.

..hivi toka uzaliwe au nchi hii iasisiwe umewahi kusikia mwana-Ccm au Tanu amefanyiwa dhuluma wanazofanyiwa wapinzani na tume ya uchaguzi, polisi, au mahakama?

..umewahi kusoma kiongozi wa Tanu kudhalilishwa na polisi wa mkoloni? Umewahi kusikia mkutano au msafara wa Ccm ukapigwa mabomu na Polisi?

..itachukua muda mrefu sana kuwaamini Polisi, mahakama, au tume, wanapotenda jambo fulani dhidi ya wapinzani.
 
Acha kuwaamini wanasiaaa wamini Zaid mungu
IMG-20221018-WA0002.jpg
View attachment 2391491
 
Mheshimiwa Mbowe ni Mwanasiasa mkongwe wa Siasa za Upinzani, hakuna ubisihi kwa sasa anaamini kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mh. Samia Suluhu Hassan inawapeleka Watanzania kwenye ile nchi ya ahadi yenye Asali na Maziwa.

Mchungaji Msigwa na Mh John Mnyika ni Wapinzani wanaoamini siasa sio kupinga tu au kutukana matusi, mara nyingi Mchungaji Msigwa amekuwa akipongeza Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo unaofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, japo kila akiongea ukweli na kupongeza amekuwa akiambulia matusi na kubezwa na vijana walioingia Chadema juzi ambao wao Siasa ni kukukana tu.

Ndugu yangu Mchungaji Msigwa, Siasa ni Sayansi, na Kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye Mwanasayansi bora kabisa wa siasa, ameweza kuwatuliza Wapinzani kisayansi kwa kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa kiwango cha juu, Watanzania wamekubali mziki wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mchungaji Msigwa, Karibu CCM, tuijenge Iringa yetu, njoo tuunge juhudi za Mwanasayans wa Siasa bora kabisa, Chadema sio mama yako wala baba yako, Umetukanwa vya kutosha na watoto wadogo kwa misimamo yako ya kusimamia ukweli .

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chawa kazini ili apate koneksheni !
 
Back
Top Bottom