Ukiacha waliokuwepo yaani Sugu na Prof. Jay, msanii mwingine anayefaa kuungana nao ni Judith Wambura peke yake

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,744
2,000
Hivi hawa wasanii wanaojitokeza eti wanataka kuwania ubunge wanajipima kweli? Kwakuwa wameona wanaweza kupata dezo kutokana na upuuzi unaoendelea ndani ya CCM kwa sasa basi wameona sehemu ya wao kupata mpunga wa laini laini ni kwenye ubunge! Hovyo kabisa kabisa

Sasa wamegeuka watu wa kusifia mpaka akili zimewaruka kabisa, wamewehuka kuliko kuwehuka kwenyewe. Yani wanaona sehemu sahihi ya wao kukimbia kutafuta kwa jasho ni kwenye ubunge. Ushenzi huu kiuhalisia umesababishwa na hii CCM ya leo ambayo imepoteza kabisa hata ule uhalisia waliokuwa nao

Eti Steve Nyerere anataka Ubunge, sijui kina Shilole eti wanataka na wao kuitwa waheshimiwa! Kweli! Kwanza ili uwe mbunge ni lazima kwanza ujitambue, hawa hakuna anayejitambua

Warudi nyuma wamuangalie Sugu alivyokuja na uthubutu mwaka 2010 akiwa katikati ya fitina za CCM akapenya tena kutokea upinzani. Huyu ukimuangalia tu na mazingira aliyokuwepo ni mtu anayejua maana ya Ubunge! Alithubutu kwa kutumia akili na utashi.

Mwenzake Prof. Jay ambaye walianza wote mziki akajiandaa kwa miaka mitano ya ziada kutengeneza mazingira naye akapenya tena ndani ya mkoa wenye kila aina ya figisu dhidi ya upinzani. Huyu anajielewa na alijipima kwa kina ikiwemo kujijenga kwa muda si chini ya miaka 10.

Yupo mwanadada Jay Dee ama Jide ambaye naye ni mkongwe, ameiva na hata ukimtazama unasema yes. Huyu akijitambua akaenda kwao ukuryani akachukua jimbo basi mapema tu anashinda. Amejijenga kwa miaka 15 sasa. Hawa ni watu pekee ambao hawajawahi kutegemea mbeleko ya dola. Walipambana kama walivyoanza kwenye mziki.

Hawa wa sasa eti utasikia anakwambia Rais kasema nigombee jimbo fulani, eti natekeleza maagizo ya Rais. Upuuzi mtupu! Ujinga wa kiwango chake! Unagombea ubunge eti unatekeleza maagizo ya Rais! What a shame! Eti ndiyo wasanii wetu hao.

Karibu sana kamanda mwingine uliyeiva Jide. Nakukubali na unajielewa nakuomba uianze safari uliyoiandaa kwa miaka 10 sasa! Unaweza kusimama pekee na unanikosha zaidi kuwa ni mwanamke unawazidi uwezo kwa mbali sana hawa wasanii uchwara wanapenda eti kugombea kwa kutimiza matakwa ya fulani.

Ukumbi wa bunge siyo sokoni useme eti umetumwa bidhaa fulani!
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,694
2,000
IMG-20200624-WA0054.jpg

Huyu anayetukana bungeni?

Kwa staili hii bora shilole awe mbunge kuliko huyo bwana
 

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
1,995
2,000
Piere liquid
Harmonize
Steve Nyerere
Shilole na wasanii wengine wa sampuli hii eti nao wanataka ubunge kwa kupitia ccm. Maajabu haya na ccm nao walivyo watawapa nafasi na kuwaacha wabunge makini kabisa ndani ya chama.
 

Itoye

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
465
1,000
Ukweli utabaki kuwa ukweli na si kwamba ni dharau kwa mtu yeyote hapana, kila mtu anaweza kupata nafasi flani hata kama ni urais lkn si kila mtu anaweza kuperform vizuri na inavyotakiwa na matokeo mazuri yakapatikana ktk nafasi hiyo.

Kama mleta uzi alivyotanabaisha Bunge lisigeuzwe fursa ya watu kupata fedha kirahisi rahisi.
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
26,018
2,000
Piere liquid
Harmonize
Steve Nyerere
Shilole na wasanii wengine wa sampuli hii eti nao wanataka ubunge kwa kupitia ccm. Maajabu haya na ccm nao walivyo watawapa nafasi na kuwaacha wabunge makini kabisa ndani ya chama.
Na Ambaruty analitaka jimbo la Mtera.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,470
2,000
View attachment 1490104
Huyu anayetukana bungeni?

Kwa staili hii bora shilole awe mbunge kuliko huyo bwana
Kwa taarifa yako matusi yake yaliwastahili hao alio watukana.
Lakini huwezi kumlinganisha Sugu na baadhi ya sio wasanii wenzake tuu bali hata wabunge wengi wa chama tawala walioko bungeni na maPhd yao. Hebu sikiliza mchango wake labda akili yako itafunguka kidogo

 

Bambaleta

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
10,365
2,000
Piere liquid
Harmonize
Steve Nyerere
Shilole na wasanii wengine wa sampuli hii eti nao wanataka ubunge kwa kupitia ccm. Maajabu haya na ccm nao walivyo watawapa nafasi na kuwaacha wabunge makini kabisa ndani ya chama.
Kama mtu Kama msukuma ,kibajaji, wamekuwa wabunge why wao wasipewe ubunge wanajiona Wana fit japo Wana ukakasi .

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom