Ukiacha Tundu Lissu ni Mbunge yupi wa Upinzani aliyewahi tokea Kanda ya Kati?

Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
27,109
39,284
Nimemsikiliza leo Tundu Lissu katika hotuba yake pale Diamond Jubilee haswa katika kipengele cha kutetea ushindi ghafla likanijia wazo kichwani.

Nikakumbuka Mazingira ya kisisiasa na kieneo alikoibukia Tundu Lissu huko singida.

Singida na Dodoma ndiko iliko ngome kuu ya CCM tangu uhuru. Kanda ya kati ndio kitovu kikuu cha umasikini kwa namna zote na ujinga uliopitiliza

Ghafla nikamtafakari Tundu Lissu aliwezaje kusimamia anachokiamini kiasi cha kuwa mpinzani na kushinda Ubunge kwenye jamii iliyolowea kwenye uCCM kiasi kile?

Licha ya kupewa upinzani mzito na Jakaya Kikwete 2010 huko Singida bado alishinda kupitia upinzani hii haiwezi toa alama ya taa nyekundu kwa CCM kuelekea October?

Kwa mnaojua ukimuondoa Lissu ni Mbunge gani wa upinzani aliyewahi shinda Kanda ya Kati?
 
Nimemsikiliza leo mhe. Tundu Lissu ktk hotuba yake pale Diamond Jubilee haswa ktk kipengele cha kutetea ushindi ghafla likanijia wazo kichwani.

Nikakumbuka Mazingira ya kisisiasa na kieneo alikoibukia Tundu Lissu huko singida!

Singida na Dodoma ndiko iliko ngome kuu ya CCM tangu uhuru! Kanda ya kati ndio kitovu kikuu cha umasikini kwa namna zote na ujinga uliopitiliza!

Ghafla nikamtafakari Lissu aliwezaje kusimamia anachokiamini kiasi cha kuwa mpinzani na kushinda ubunge kwenye jamii iliyolowea kwenye uCCM kiasi kile?

Licha ya kupewa upinzani mzito na JK 2010 huko Singida bado alishinda kupitia upinzani hii haiwezi toa alama ya taa nyekundu kwa CCM kuelekea October?

Kwa mnaojua ukimuondoa Lissu ni mbunge gani wa Upinzani aliyewahi shinda kanda ya kati?

..usisahau kwamba aligombea na kushindwa mara ya kwanza mwaka 1995 kupitia NCCR-Mageuzi.
 
Tundu Lisu kabla hajaingia kwenye siasa alikuwa mwanaharakati aliyepigania haki za watu wanaoishi karibu na migodi ya dhahabu.
Ikumbukwe kabla mgodi wa Kahama haujapewa wawekezaji, waliokuwa wanachimba dhahabu hapo ni watanzania.
Serikali ya awamu ya tatu iliwaondoa kwa nguvu wachimbaji hao ili kuwapa nafasi wawekezaji.
Wakati serikali inatekeleza operesheni hiyo ya nguvu ambayo ilitawaliwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, Tundu Lisu na mwenzake Lugemeleza Nshala walihusika sana kuwatetea watanzania hao wanyonge ambao baadhi yao ilidaiwa walifukiwa ndani ya mashimo hayo baada kukaidi amri ya kuondoka eneo hilo.
Tundu Lisu alipata matatizo mengi kwenye harakati zake hizo, hali iliyopelekea watanzania wengi kulisikia jina lake kama mtanzania mwenye uchungu na raslimali za nchi hii.
Baada ya harakati zake kupata changamoto nyingi tena bila ya msaada wa maana toka kwa wanasiasa, akaamua ajitose kwenye siasa ili apate uwanja mpana wa kuwatetea walio wengi.
Kwa sababu hiyo ilikuwa rahisi kwake kulitwaa jimbo la Singida mashariki maana tayari alikuwa na jina.
Vinginevyo umasikini uliotamaliki kanda ya kati imekuwa silaha muhimu kwa CCM kutawala siasa za eneo hilo
 
Upo sahihi mkuu, Singida, Tabora, Dododma, Pwani, Njombe, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Rukwa, Katavi, Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro na Songwe ni aibu tupu? huko CCM imeota mizizi na ndiyo masikini/mafukara wa kupindukia
Mkuu iondoe Morogoro na Mtwara.
Maana mpaka bunge linamalizika tayari Morogoro ilkuwa na wabunge watatu wa upinzani na madiwani wengi.
Mkoa wa Mtwara umetoa wabunge wa Ndanda, Mtwara mjini na Tandahimba
 
Upo sahihi mkuu, Singida, Tabora, Dododma, Pwani, Njombe, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Rukwa, Katavi, Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro na Songwe ni aibu tupu? huko CCM imeota mizizi na ndiyo masikini/mafukara wa kupindukia
Kigoma itoe, hakuna ngome ya ccm. Jimbo gani?
 
Lissu alipita kwa bahatimbaya tu.sijui msimazi wa uchaguzi alikuwaje akasahau kuskoo kama maradona!!.
 
Upo sahihi mkuu, Singida, Tabora, Dododma, Pwani, Njombe, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Rukwa, Katavi, Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro na Songwe ni aibu tupu? huko CCM imeota mizizi na ndiyo masikini/mafukara wa kupindukia

Morogoro, Kigoma, Lindi na Tabora kuna upinzani

Ila Dodoma na Singida walahy duh hadi aibu yaani kule CCM inajidai mnoo
 
Upo sahihi mkuu, Singida, Tabora, Dododma, Pwani, Njombe, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Rukwa, Katavi, Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro na Songwe ni aibu tupu? huko CCM imeota mizizi na ndiyo masikini/mafukara wa kupindukia
Tabora 1995 Abraham Msina.2010 Magdalena Sakaya 2015 Magdalena Sakaya.
Rukwa 1995 Ally Kesi, Said Amour Arfi

Simiyu 1995 -2015 John Momose Cheyo, Dani Makanga.

Shinyanga 2010, John Shibuda, Salum Oporukwa, Sylevester Kasulumbayi.

Kigoma. 1995 Daniel Nsanzugwanko, Aman Warid Kabulu ( RIP) 2010, Felix Mkosamali, David Kafulila, Buyongela Zitto Zuberi Kabwe, Kasuku Bilago (RIP)

Morogoro, 2015 Suzan Kiwanga, Joseph Haule Peter Lijualikali.

Mikoa ya Lindi na Mtwara ni ngome ya CUF toka zamani imagine 2015 CUF walibeba majimbo 10 katka mikoa hiyo.

Hebu tupe data za mkoa wako ????

Leta mkoa wako wewe
 
Back
Top Bottom