Ukerewe yalalamikia bei kubwa ya umeme, wananchi wanalipa 2,500 kwa unit 1 ya umeme

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
2c5c39c9e62c825da300738b0ba21354

Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dk Medard Kalemani ametoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kuhakikisha anafuatilia gharama za umeme zinazotozwa kwa wananchi wa kisiwa cha Ukerewe mkoani humo.

Imeelezwa leo bungeni kuwa Watumiaji wa umeme katika Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza wanatumia nishati hiyo kwa gharama ya Sh2,500 kwa uniti moja badala ya Sh100 inayotozwa kwa maeneo mengine.

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma leo na Mbunge wa Ukerewe (CCM), Joseph Mkundi wakati akiuliza swali la nyongeza akiitaka Serikali kuchukua hatua.

Akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema jambo hilo halikubariki.

Dk Kalemani amesema Mtanzania yeyote anayetumia umeme usiozidi uniti 70 kwa mwezi, anapaswa kulipia kiwango cha Sh100 kwa uniti siyo gharama ya huko.
 
Hiyo bei ya unit kwa sh 100 yeye kaisikia wapi au nyumbani kwake ndo anapewa unit 1 kwa sh. 100 kwa kuwa yy waziri?
 
Wapi wanatoza Unit moja ya umeme kwa shilingi 100

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo bei ya unit kwa sh 100 yy kaisikia wapi au nyumbani kwake ndo anapewa unit 1 kwa sh. 100 kwa kuwa yy waziri?

Chini ya unit 70 ~ 100
Zaidi ya unit 70 ~ 300

Ukiona unatozwa zaidi ya 100 ujue unatumia umeme mwingi.

Na kama unatumia kidogo unaenda Tanesco wanakubadilishia Tariff
 
Kwetu huku buku 5 unapata unit 14

dodge
sio kwenu sema kwako, hilijambo liko wazi.
Ukiona elfu tano ya kibongo unapata unit hizo jua uko ndani ya service charge.
Ukichukua buku ukapata unit 8ni sawa na mizani nane hio mia mbili inaenda kwenye hizo kodi miexer ewura jombaaa
 
Hii nch wiz hautaisha dadek

Kuna hyo sehem mkoan Lind huo umeme ukianza kukata unapta had wk ujarud
Yaan mpaka raha ya umeme inapotea
 
Moja hawaongelei kisiwa cha ukerewe, kinaongelewa kisiwa cha ukara ambapo ndio kuna umeme wa jua na sio miliki ya Tanesco.a

Mbili, umeme unaotumika katika kisiwa cha ukara ni umeme wa jua, gharama za kuuzalisha ni ndogo sana ila initial investmest cost ni kubwa sana, mfano kwa makadirio ya chini hapo ukara kampuni ukute imetumia zaidi ya milioni 500 za kitanzania kumaliza mradi mzima. Pamoja na bei kuwa juu ila naamini kampuni haikusanyi zaidi ya milioni 5 kwa mwezi kwa kisiwa cha ukara pekee.

Ukipiga hesabu za wafanyakazi, faida ni ndogo sana, hata kama baadhi ya fedha ni msaada ila return on investment kuipata ni shughuri.

Kumbuka, kampuni inanunua vifaa vya solar (german standard), transformer, nguzo, nyaya za umeme, na mita za umeme. Mteja analipia gharama ndogo sana anafanyiwa wiring, ambayo gharama hiyo inaanzia elfu 32 za kitanzania.
 
Back
Top Bottom