Ukerewe, Mwanza: Meli Mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 500 yazinduliwa

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
9bf972b85d27808c4ff709ed581c5778.jpg


Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela amezindua rasmi huduma ya usafiri wa meli kati ya Mwanza na mji wa Nansio wilayani Ukerewe katika ziwa Victoria, ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 500 magari madogo 40 na tani 284 za mizigo, hatua itakayosaidia kutatua changamoto ya huduma za usafiri wa abiria kwa wakazi wa kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.

image.jpeg


Meli hiyo MV. Nyehunge II, imejengwa na kampuni ya Songoro Marine Transport kwa gharama ya shilingi milioni 800 na kufanyiwa ukaguzi na maofisa wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA), Makao Makuu Dar es Slaam.

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Ukerewe, akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, George Nyamaha wanaeleza changamoto za usafiri zilizokuwa zinawakabili awali.
 
Na jamaa kajifungia ikulu tu, sijui anashona godoro la hela kwa kutumia hela za misaada ya wahanga wa tetemeko badala ya sufi au bamba?
Mv Serengeti, mv butiama zifia wapi?
Mpaka mtu binafsi anaweka meli?
Watu wanashangilia, je serikali meri zake zilienda wapi?
 
Kero ya usafri wa ukerewe sasa kwisha

Ila watusaidie pia kujua kama na ' maboya ' ya kuogelea nayo yapo 500 ili siku ya siku tusije kurudia kama ya tarehe 21, May mwaka 1996 ambapo kwa muda wa wiki mbili mpaka miezi miwili hivi ulikuwa ukifungulia maji tu unakutana na kucha, kidole gumba, kisigino, ulimi na kucha baada ya abiria kuwepo 1500 na ' maboya ' yaliyokuwepo yalikuwa 13 ndani ya MV TETEMEKO LA ARDHI.
 
Back
Top Bottom