Ukerewe: Mkuu wa wilaya amuweka ndani mwalimu kwa kosa la kuwafungia darasani wanafunzi mpaka usiku

Madihani

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
6,080
6,913
*Breaking news*
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe MH *Francis chang'ah* amuweka ndani mwl wa shule ya msingi *Uhuru* , kwa kosa la kuwafungia Darasani watoto wa shule mpaka saa mbili za usiku kwa kosa la watoto hao kushindwa kusoma Tebo.

DC. Alipata Taarifa kutoka kwa katibu uvccm wilaya ya Ukerewe kwa njia ya simu.
Katibu alieleza amekutana na Tukio ilo muda si mrefu na kuamua kufika shule hiyo ya Uhuru na kukuta ni kweli ndipo alipochukua hatua kumuomba Mh. DC awatume askari wamuweke ndani mwl huyo.

Pia mwenyekiti wa Halmashauri wilaya ya ukerewe MH *George Machela Nyamaha* baada ya kufika eneo la Tukio alisikitishwa sana na hali hiyo , ila alishukuru kitendo cha DC kumuweka ndani mwl huyo ili liwe fundisho na kwa waalimu wengine wenye Tabia kama hizo.

Mama mzazi wa mtoto azimia baada ya kumtafuta mtoto wake kwa muda mrefu na baadae kumkuta shuleni akiwa amefungiwa na kufuli

Akiongea na waandishi wa habari katibu uvccm comrede *Hussein Egobano* alisema kuwa anawaomba waalimu kutumia Taaluma zao vizuri wawapo katika vituo vyao vya kazi .
 
Walimu wanatakiwa kujitambua ,kumfungia Mtoto siyo njia harisi ya kumfundisha, tumia njia mbadala kumwelimisha Mtoto.

Naona watu wanapita kimya kimya toeni mawazo ili Walimu waache kujipendekeza kuwarekebisha wanafunzi.
 
Moja ya tatizo kubwa ya waalimu wa siku hizi ni kukosa mbinu za ufundishaji na ndo maana idadi ya kufeli vijana ni kubwa sana.
 
Huyo mwalimu aliefungia watoto ni kilaza kuliko watoto wenyewe.
 
Mimi nashauri waache kuwa busy na wanafunzi,kama hawaelewi waachane nao watimize wajibu tu.

Moja ya tatizo kubwa ya waalimu wa siku hizi ni kukosa mbinu za ufundishaji na ndo maana idadi ya kufeli vijana ni kubwa sana.
 
WAALIMU WA TANZANIA HAWAJITAMBUI NA HAWAJAWAHI KUJITAMBUA

Wao ni maneno na vitisho vya mdomoni tu ila hawana lolote hao.
 
Watoto ni vilaza jamani acheni tu ninavyoongea na nyinyi kuna wadogo wawili wapo kibarazani wanaandika na kila siku ndiyo maisha yao.
Leo wamenisimamisha wananiuliza majibu ya maswali, nikiangalia maswali yenyewe nyanya mpaka basi.

Hata hivyo na wenyewe wanawalaumu walimu kua ndiyo vilaza ndiyo maana na wao wapo hivyo.
 
Walimu wanatakiwa kujitambua ,kumfungia Mtoto siyo njia harisi ya kumfundisha, tumia njia mbadala kumwelimisha Mtoto.
Wakitumia viboko... Raia wanatokwa na mapovu! Kweli ualimu siyo kazi ila ni wito tu...
 
Nchi hii hatuna walimu. Hao ni watz waliofeli na kushindwa kwenda fani nyingine ndiyo wakajipachika kwenda kwenda kwenye hilo kundi la zoa zoa linaloitwa ualimu.

kila kiongozi anajipatia uzoefu wa kufanya kazi na kupanda daraja kupitia kundi hili.
>kuchapwa viboko na wanafunzi
>kuchapwa viboko na DC
>kutolewa matamko ya kudhalilisha
>kunyimwa/kucheleweshewa Stahiki Zao,
n.k
Yote Hayo Yanafanyika Kwa Kundi Hili. Lkn Huwezi Kusikia Limegoma. Kwakuwa Hawana Vyeti Halali. Vyote Ni Vya Marehemu
 
Sio kweli mkuu nawewe umekariri,wapo waliofaulu kwa kiwango cha division one form four na form six,chuo kikuu wakachagua Education ni walimu.

Chunguza chuo kama UDSM wote wa Bachelor of Arts with Education wamechaguliwa kwa kigezo cha division one.

Labda unaongelea level gani ya elimu.

Back
Top Bottom