Ukereketwa wa dini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,333
Hivi ni kwa nini watu wanaoziacha dini zao za awali na kuingia kwenye dini mpya wanakuwa ni wakereketwa sana kuliko wenye dini haswa.
Mfano mtu akitoka kwenye uislamu akiingia ukristo anakuwa mkereketwa sana kuliko aliowakuta na ukristo wao,
hali kadhalika mtu akitoka kwenye ukristo na kuingia uislamu anakuwa mfurukutwa sana kuliko hata ma sheikh wa mujahidin aliowakuta na wakamfunza dini?
 
Duu Terminology zako zimeniacha hoi!!
Kwani kuna tofauti gani hasa kati ya mkereketwa na mfurukuta?
 
Hivi ni kwa nini watu wanaoziacha dini zao za awali na kuingia kwenye dini mpya wanakuwa ni wakereketwa sana kuliko wenye dini haswa.
Mfano mtu akitoka kwenye uislamu akiingia ukristo anakuwa mkereketwa sana kuliko aliowakuta na ukristo wao,
hali kadhalika mtu akitoka kwenye ukristo na kuingia uislamu anakuwa mfurukutwa sana kuliko hata ma sheikh wa mujahidin aliowakuta na wakamfunza dini?

There is no truth in your words.
 
atakuwa mkereketwa kwa sababu anaona ukweli wa mambo na watu aliowakuta hafuati dini kama ifuatavyo ndio maana anakua mkali wa dini na mfuasi mzuri wa Dini lakini itabidi ajifunze vizuri sio tu kutoka katika dini moja na kujiunga na dini ingine unakuwa mkereketwa mkali itabidi ujifunze dini unayoingia vizuri na uijuwe hiyo dini mpya kwa uzuri zaidi ndio utakuwa mkereketwa mzuri hayo ni mawazo yangu mimi
 
Asante kwa mawazo mazuri.
Je inakuaje pale dini uliyoiingia inapokuwa ina discourage kuuliza uliza maswali ili uijue vizuri?
 
asante kwa mawazo mazuri.
je inakuaje pale dini uliyoiingia inapokuwa ina discourage kuuliza uliza maswali ili uijue vizuri?

kama umefanya uchambuzi yakinifu utatambua huku niendako kukoje.
Lakini ikiwa umekurupuka tu, you are in for it.
 
Asante kwa mawazo mazuri.
Je inakuaje pale dini uliyoiingia inapokuwa ina discourage kuuliza uliza maswali ili uijue vizuri?

Kuna baadhi ya dini hutakiwi kuuliza maswali sensitive ndugu! Watakutishia muda si mrefu! Na ukiamua kuiacha hiyo dini baada ya kugundua ukweli na ikiwa uko Saud Arabia, Northern Nigeria, Darfur-Sudan, Somalia, Pakistan, Iran, Indonesia, nk, utaangamizwa maisha yako kabisa, hata kama ni kwa kujilipua mwangamizaji!
 
Asante kwa mawazo mazuri.
Je inakuaje pale dini uliyoiingia inapokuwa ina discourage kuuliza uliza maswali ili uijue vizuri?

Ukiuliza maswali ya ndani sana UTAAMBIWA HAUNA ROHO MTAKATIFU na hata ukitaka kusoma kwenye kitabu chenyewe unaambiwa huwezi elewa wewe unapewa vile vilivyorahisishwa katekism na chuo kidogo cha Sala
 
kuna baadhi ya dini hutakiwi kuuliza maswali sensitive ndugu! Watakutishia muda si mrefu! Na ukiamua kuiacha hiyo dini baada ya kugundua ukweli na ikiwa uko saud arabia, northern nigeria, darfur-sudan, somalia, pakistan, iran, indonesia, nk, utaangamizwa maisha yako kabisa, hata kama ni kwa kujilipua mwangamizaji!
ukiongea hivyo utapigwa mawe hadi ufe
 
Ukiuliza maswali ya ndani sana UTAAMBIWA HAUNA ROHO MTAKATIFU na hata ukitaka kusoma kwenye kitabu chenyewe unaambiwa huwezi elewa wewe unapewa vile vilivyorahisishwa katekism na chuo kidogo cha Sala

Hivi huyu Roho mtakatifu ni nani? Nini athari yake kama utamkosa?
 
Hilo hata mimi nilikuwa naliwaza kwa muda sana, ila nafikiri mara nyingi mtu akihamia dini nyingine huwa kuna imani fulani imemvuta kuwa kule. na hivyo hujikita sana kiimani ili waumini wengine nao wavutiwe kuelekea huko alikohamia sasa.
 
Hivi ni kwa nini watu wanaoziacha dini zao za awali na kuingia kwenye dini mpya wanakuwa ni wakereketwa sana kuliko wenye dini haswa.
Mfano mtu akitoka kwenye uislamu akiingia ukristo anakuwa mkereketwa sana kuliko aliowakuta na ukristo wao,
hali kadhalika mtu akitoka kwenye ukristo na kuingia uislamu anakuwa mfurukutwa sana kuliko hata ma sheikh wa mujahidin aliowakuta na wakamfunza dini?

swali lako ni zuri ingawa naona wazee wa ligi washaanza kuliteka na kulipeleka kwenye ligi yao.
kuna ukweli hapo, mfano uislam na ukristo umetoka huko kwa wenyewe, lakini ulivyokuja kwetu sisi tuliokua na dini za kijadi ndo tumekuwa wakereketwa na wafurukutwa kushinda wao
mi nafikiri kwa wengi ni kutaka kupata uhalali machoni pa wale alojiunga nao, au kutafuta sifa au ulimbukeni. na mifano sio hiyo tu ya kutoka dini moja kwenda nyingine, ni pamoja na kuhama ndani ya dhehebu moja kwenda lingine.tatizo letu ni kuwa mtazamo wetu umejikita kwamba kuna dini mbili tu yaani uislam na ukristo.
hilo swala haliko kwenye dini tu bali ni maisha kwa ujumla. just imagine ukitoka tanzania na kwenda marekani utakavyotaka uijue USA na kuwaonyesha hata wenyeji kwamba na wewe unaijua tena ikiwezekana hata kushinda wao. ukihama kutoka manzese na kuhamia masaki itakavyokua kwa uliowaacha kule manzese. ukibalehe/vunja ungo utakavyokua na hamu ya ku-do kushinda hata wale walioanza kabla yako etc etc.
nafikiri pia umewahi kuwaona hao wenye dini bora wakiziacha/asi (wakifuata upande wa shetani) huwa wanavyokua wakereketwa na wafurukutwa wa maraha na maasi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom