Ukeketaji ni kitu cha maana sana na humfanya mwanamke kuwa safi na kujisafisha kirahisi. Kuna ukweli wowote kwenye kauli hii?

majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,351
4,028
Wandugu, Katika pita pita zangu nilikutana na Bibi wa umri mkubwa sana tu. Katika maongezi yetu Bibi tulijikuta tunaongelea kuhusu ukeketaji. Bibi alinambia ukeketaji ukifanyika vizuri ni kitu cha maana sana sana, eti kwanza kinamfanya mwanamke kuwa safi, ni rahisi kujisafisha. Pili, kinazuia mwanamke kutoa harufu, waliofanyiwa hivyo hawanuki hata wakati wa tendo kuliko wale wasiofanyiwa. Tatu, hawapati kirahisi fungus, UTI na mengine! nilibaki hoi.

Nikajaribu kumuelezea shida inayowapata wakati wa kujifungua... jamani huyu Bibi akaniambia inategemeana na mkataji, kuna ukataji mzuri ambao hauletagi shida na ndio maana .... akataja kabila la kwao... kwamba wanazaa watoto wengi na bila shida kwa kuwa wanafanyiwa vizuri. mmmmmh nilibaki mdomo wazi aliponambia waulize hata wanaume huwa wanaenjoy sana tu wakiwa na hao walioshughulikiwa!!!!! ha ha haaaa nilipingana naye lakini akanambia mimi nakataa kwa maneno, nitafute wanaojua kwa matendo ndio nibishe...

Jamani nipeni mawazo na mitazamo yenu. Aliyosema bibi ni kweli???
 
Wandugu, Katika pita pita zangu nilikutana na Bibi wa umri mkubwa sana tu. Katika maongezi yetu Bibi tulijikuta tunaongelea kuhusu ukeketaji. Bibi alinambia ukeketaji ukifanyika vizuri ni kitu cha maana sana sana, eti kwanza kinamfanya mwanamke kuwa safi, ni rahisi kujisafisha. Pili, kinazuia mwanamke kutoa harufu, waliofanyiwa hivyo hawanuki hata wakati wa tendo kuliko wale wasiofanyiwa. Tatu, hawapati kirahisi fungus, ITU na mengine! nilibaki hoi.

Nikajaribu kumuelezea shida inayowapata wakati wa kujifungua... jamani huyu Bibi akaniambia inategemeana na mkataji, kuna ukataji mzuri ambao hauletagi shida na ndio maana .... akataja kabila la kwao... kwamba wanazaa watoto wengi na bila shida kwa kuwa wanafanyiwa vizuri. mmmmmh nilibaki mdomo wazi aliponambia waulize hata wanaume huwa wanaenjoy sana tu wakiwa na hao walioshughulikiwa!!!!! ha ha haaaa nilipingana naye lakini akanambia mimi nakataa kwa maneno, nitafute wanaojua kwa matendo ndio nibishe...

Jamani nipeni mawazo na mitazamo yenu. Aliyosema bibi ni kweli???
ITU-hiki ndio nini?
 
Ukeketaji sio sahihi, huyo anatetea mila za kwao ambazo si nzuri, sasa kiungo kimewekwa kwanini wewe ukitoe?
 
Kwa wao kipindi kile na kwa tamaduni zao waliaminishwa kuwa ni kitu kizuri, ila kwa dunia ya sasa sio vizuri. Ata zamani waliamini dunia ipo flat ila kwa maendeleo ya science wakaambiwa dunia ipo kama tufe, .... It's a matter of mind setup, ulisikia nini na kuaminishwa nini.
 
Ukataji wa kisimi ni kupunguza matamanio ya kijinsia tu, na ndio faida yake kubwa. Mwanamke akiwa mchafu atatoa harufu kama kawaida atapata fungus na UTI bila shaka, ataumia tu kwa uchafu wake, visimi havihusika hapo... Bi Mkubwa asianze kupeleka lawama kwenye visimi.
 
Birdman na Lil Wayne wana wimbo unaitwa Believe Dat kiitikio kinasema

'Why would you? Believe dat

Why would you? Believe dat

How could you? Believe dat...
 
Ukeketaji sio sahihi, huyo anatetea mila za kwao ambazo si nzuri, sasa kiungo kimewekwa kwanini wewe ukitoe?

Wanadai eti, Lengo la kukitoa ni usafi, na kupunguza magonjwa.
 
Birdman na Lil Wayne wana wimbo unaitwa Believe Dat kiitikio kinasema

'Why would you? Believe dat

Why would you? Believe dat

How could you? Believe dat...

Hujaeleweka ndugu
 
Ukataji wa kisimi ni kupunguza matamanio ya kijinsia tu, na ndio faida yake kubwa. Mwanamke akiwa mchafu atatoa harufu kama kawaida atapata fungus na UTI bila shaka, ataumia tu kwa uchafu wake, visimi havihusika hapo... Bi Mkubwa asianze kupeleka lawama kwenye visimi.

Nilimwambia hivyo, akadai eti nichunguze kati ya waliotolewa na wenye navyo nani anaathirika zaidi na magonjwa? nani anatoa harufu? nilibaki mdomo wazi
 
Back
Top Bottom