Ukawa waomba dua kwenye kaburi la nyerere

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,222
2,000
Watanzania wametakiwa kuwa makini na watu wanaodaiwa kuwa wanafanya unafiki wa kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa maneno ya jukwaani, huku wakimnanga kwa kufanya vitendo vya kifisadi na ubadhirifu kinyume na mafundisho yake.

Badala yake, hasa wakati huu ambapo taifa linapitia kwenye changamoto za kuandika Katiba Mpya, wananchi wametakiwa kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo, kwa kupigania katiba mpya inayozingatia maoni ya wananchi kwa ajili ya maisha yao na hatma ya taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipoongoza msafara wa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwenda kuzuru kaburi la Baba wa Taifa na kuijulia hali familia ya Mwalimu Nyerere, kijijini Mwitongo, Butima juzi, Jummane.

Viongozi hao walipokelewa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere na mmoja wa watoto wa familia hiyo, Madaraka Nyerere ambaye aliwatembeza katika kaburi la Hayati Baba wa Taifa, ambapo walipata fursa ya kuweka mashada ya maua katika kaburi hilo.

Akiwakaribisha viongozi hao, Madaraka alisema kuwa pamoja na kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa mwanachama wa CCM, lakini familia hiyo inatunza hadhi yake ya kuwa Baba wa Taifa kwa kuwakaribisha watu mbalimbali hata kama ni wanachama au viongozi wa vyama vya upinzani, kutembelea kaburi hilo.

Dkt. Slaa aliyekuwa ameongozana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), Mustapha Wandwi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Hemed Msabaha pamoja na Kiongozi wa Shura ya Maimamu, Suweid Sadiq
 
DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,614
2,000
Ccm wakisikia hili wanatetemeka.

Wanatamani wazuie wapinzani kwenda kule ila familia ya mwalimu haiingiliki.
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,595
2,000
Watanzania wametakiwa kuwa makini na watu wanaodaiwa kuwa wanafanya unafiki wa kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa maneno ya jukwaani, huku wakimnanga kwa kufanya vitendo vya kifisadi na ubadhirifu kinyume na mafundisho yake.

Badala yake, hasa wakati huu ambapo taifa linapitia kwenye changamoto za kuandika Katiba Mpya, wananchi wametakiwa kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo, kwa kupigania katiba mpya inayozingatia maoni ya wananchi kwa ajili ya maisha yao na hatma ya taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipoongoza msafara wa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwenda kuzuru kaburi la Baba wa Taifa na kuijulia hali familia ya Mwalimu Nyerere, kijijini Mwitongo, Butima juzi, Jummane.

Viongozi hao walipokelewa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere na mmoja wa watoto wa familia hiyo, Madaraka Nyerere ambaye aliwatembeza katika kaburi la Hayati Baba wa Taifa, ambapo walipata fursa ya kuweka mashada ya maua katika kaburi hilo.

Akiwakaribisha viongozi hao, Madaraka alisema kuwa pamoja na kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa mwanachama wa CCM, lakini familia hiyo inatunza hadhi yake ya kuwa Baba wa Taifa kwa kuwakaribisha watu mbalimbali hata kama ni wanachama au viongozi wa vyama vya upinzani, kutembelea kaburi hilo.

Dkt. Slaa aliyekuwa ameongozana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), Mustapha Wandwi na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Hemed Msabaha pamoja na Kiongozi wa Shura ya Maimamu, Suweid Sadiq

Sijui wale vijana walioenda kumsanifu Mama Maria na Mabosi wao wanajiskiaje
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom