UKAWA wakubaliana kuwanyima mafuta wakuu wa Wilaya

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameagiza wenyeviti wa halmashauri 18 nchini zinazoongozwa na UKAWA kuacha utaratibu wa kutoa fedha za halmashauri kuwasaidia mafuta ya magari wakuu wa wilaya au kuzitumia kwa ajili ya masuala ya kisiasa ya vyama vyao.

Akizungumza na mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Ukawa katika mkutano uliofanyika juzi mjini Arusha, Mbowe alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa na halmashauri hizo zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema katika kikao hicho cha mameya na wenyeviti wa halmashauri, wametambua kuwa kuna matumizi mabaya ndani ya Serikali, mbali na wafanyakazi hewa ambao wapinzani wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2005.

Mbowe alisema bado kuna halmashauri ambazo zimekuwa zikitumia fedha kufadhili ofisi za wakuu wa wilaya na chama tawala, jambo ambalo sasa kwa halmashauri za UKAWA halitakuwapo.

“Maeneo ambayo wakuu wa wilaya wamezoea kuomba fedha za mafuta na CCM wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kazi zao tunawaambia wasithubutu tena kwenda kwenye halmashauri zinazoongozwa na UKAWA, kwani hatutawapa fedha na tunawaumbua,” alisema.

Mbowe alisema katika halmashauri za UKAWA hawataki kusikia kuna fedha zimetolewa kwa wakuu wa wilaya au chama chochote cha siasa.
Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuanzisha mipango mikakati ambayo itawezesha kubuniwa vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni rafiki kwa wananchi, kupatikana kwa ajira na kuboresha huduma muhimu za Watanzania.

Akizungumza baada ya maelekezo hayo, Mwenyekiti wa Madiwani CHADEMA nchini ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema watatekeleza na hawatakubali kuingiliwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makatibu tawala.

Calist alisema katika halmashauri za UKAWA uamuzi wa mwisho wa uendeshaji wa halmashauri utafanywa na madiwani na siyo mtu kutoka nje ya halmashauri hizo.

“Tutasimama na kutetea mamlaka ya kisheria ya Serikali za mitaa hapa nchini,” alisema.

Katibu wa Madiwani wa UKAWA nchi nzima ambaye ni Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema watahakikisha wanasimamia utendaji mzuri wa halmashauri zote wanazoziongoza ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
 
Hahaha wanataka watembee na miguu ...idea .nzurI ya ukusanyaji wa Kodi .. mpaka Ukawa wameigia..
Tunakisanya kodi huku tunarudi kwnye Primitive life .
 
Kuanza vita ni rahisi, lakini kuimaliza ni shida.

Mbowe be careful what you wish for.

Madiwani ni sawa na wabunge sio waajiriwa wala watendaji wa serikali.Meya ni sawa na spika wa bunge yeye ni spika wa baraza la madiwani si mtendaji wala mwajiriwa wa halmashauri.Naona hicho kikao chao koko wameongelea utendaji AS IF mameya na madiwani ni watendaji na waajiriwa wa Halmashauri.Kwa hiyo yakija malipo watagoma kuidhinisha na kulipa!!!! Hivi wanajua mipaka yao?
 
Pia kodi inakusanywa kwa ajili ya maemdeleo wanyimwe vyama vya siasa ruzuku. Hizi hela zinaenda kufanya siasa na maandamano yasiyo na tija

Kabisa nashauri hata mimi serikali ifute Ruzuku ZA VYAMA VYA SIASA PESA ZIENDE kwenye miradi ya maendeleo.Vyama viendeshwe kwa michango ya wanachama wao kama ambavyo simba na yanga wanafanya.Raisi Magufuli peleka mswada bungeni wa kufuta ruzuku ya vyama haraka iwezekanavyo
 
Madiwani ni sawa na wabunge sio waajiriwa wala watendaji wa serikali.Meya ni sawa na spika wa bunge yeye ni spika wa baraza la madiwani si mtendaji wala mwajiriwa wa halmashauri.Naona hicho kikao chao koko wameongelea utendaji AS IF mameya na madiwani ni watendaji na waajiriwa wa Halmashauri.Kwa hiyo yakija malipo watagoma kuidhinisha na kulipa!!!! Hivi wanajua mipaka yao?
kwani matumizi ya Halmashauri ni akina nani wanadhibiti,si baraza la madiwani au hujui???
 
Mimi ninavyojua, Mkurugenzi wa Halmashauri iwe Wilaya, Mji, Mkoa au Jiji ndiye mwenye fungu la fedha na si mwenyekiti, au huo utaratibu siku hizi umebadilishwa?
Mkurugenzi anaidhinisha matumizi yaliyopitishwa na baraza la madiwani, anapokwenda kinyume atakumbana na rungu la madiwani. Ndio sheria ya fedha za halmashauri.
Huo mtindo wa RCs na DCs kuwa na upungufu wa bajeti ofisi zao na kuagiza mafuta na hata stationery kutoka Halnashauri ulisha ota mizizi na wengine wanapanga safari na kudai mpaka posho wapewe.
Well done Ukawa
 
Mkuu wa Wilaya ndio Mkuu wa wilaya ikiwemo na Halmashauri. Acha ukuda wewe. Kwani wewe hutu,i fedha kumsaidia baba yako eti tu kwa vile umesoma sana na una kipato kizuri ilhali aliyekusomesha ni huyo baba yako Maskini?
kweli Watanzania ni wajinga-Halmashauri itoe fedha kutoka wapi kwa ajili ya kusaidia ofisi ya Mkuu wa wilaya hivi hujui fedha zinabajetiwa-au unadhani kuna fungu limetengwa kwa ajili ya kusaidia kazi za Mkuu wa wilaya au CCM??
 
Hivi mnajuaga DED wa serikali na Meya wa siasa nani zaidi zaidi. Mnajua nani anatoa hela kwa halmashauri?

Mkisikia mbowe kasema manakimbia kuandika huku. Msubiri njaa
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameagiza wenyeviti wa halmashauri 18 nchini zinazoongozwa na Ukawa kuacha utaratibu wa kutoa fedha za halmashauri kuwasaidia mafuta ya magari wakuu wa wilaya au kuzitumia kwa ajili ya masuala ya kisiasa ya vyama vyao.

Akizungumza na mameya na wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na Ukawa katika mkutano uliofanyika juzi mjini Arusha, Mbowe alisema viongozi hao wanapaswa kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa na halmashauri hizo zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema katika kikao hicho cha mameya na wenyeviti wa halmashauri, wametambua kuwa kuna matumizi mabaya ndani ya Serikali, mbali na wafanyakazi hewa ambao wapinzani wamekuwa wakilalamika tangu mwaka 2005.

Mbowe alisema bado kuna halmashauri ambazo zimekuwa zikitumia fedha kufadhili ofisi za wakuu wa wilaya na chama tawala, jambo ambalo sasa kwa halmashauri za Ukawa halitakuwapo.

“Maeneo ambayo wakuu wa wilaya wamezoea kuomba fedha za mafuta na CCM wamekuwa wakiomba fedha kwa ajili ya kazi zao tunawaambia wasithubutu tena kwenda kwenye halmashauri zinazoongozwa na Ukawa, kwani hatutawapa fedha na tunawaumbua,” alisema.

Mbowe alisema katika halmashauri za Ukawa hawataki kusikia kuna fedha zimetolewa kwa wakuu wa wilaya au chama chochote cha siasa.

Alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuanzisha mipango mikakati ambayo itawezesha kubuniwa vyanzo vipya vya mapato ambavyo ni rafiki kwa wananchi, kupatikana kwa ajira na kuboresha huduma muhimu za Watanzania.

Akizungumza baada ya maelekezo hayo, Mwenyekiti wa Madiwani Chadema nchini ambaye pia ni Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema watatekeleza na hawatakubali kuingiliwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na makatibu tawala.

Calist alisema katika halmashauri za Ukawa uamuzi wa mwisho wa uendeshaji wa halmashauri utafanywa na madiwani na siyo mtu kutoka nje ya halmashauri hizo.

“Tutasimama na kutetea mamlaka ya kisheria ya Serikali za mitaa hapa nchini,” alisema.

Katibu wa Madiwani wa Ukawa nchi nzima ambaye ni Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alisema watahakikisha wanasimamia utendaji mzuri wa halmashauri zote wanazoziongoza ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
 
Kabisa nashauri hata mimi serikali ifute Ruzuku ZA VYAMA VYA SIASA PESA ZIENDE kwenye miradi ya maendeleo.Vyama viendeshwe kwa michango ya wanachama wao kama ambavyo simba na yanga wanafanya.Raisi Magufuli peleka mswada bungeni wa kufuta ruzuku ya vyama haraka iwezekanavyo
Mbona kama umepanic...eeeh! Hidaya, huu mchezo hautaki hasira. Cool down tuzungumze kiungwana. Huyu unayemuamrisha kufuta kupeleka muswada ni nani wako?

Madiwani ni sawa na wabunge sio waajiriwa wala watendaji wa serikali.Meya ni sawa na spika wa bunge yeye ni spika wa baraza la madiwani si mtendaji wala mwajiriwa wa halmashauri.Naona hicho kikao chao koko wameongelea utendaji AS IF mameya na madiwani ni watendaji na waajiriwa wa Halmashauri.Kwa hiyo yakija malipo watagoma kuidhinisha na kulipa!!!! Hivi wanajua mipaka yao?
Ni kweli madiwani ni sawa na wabunge, kwa hiyo unapaswa kujua kuwa hakuna bajeti ya halmashauri inapaswa kupita bila idhini yao. Ni vile bunge letu limehodhiwa na mhimili mwingine kiasi hujui kuwa hata bajeti ya nchi na matumizi mengine ya fedha yanapaswa kuamuliwa na bunge.

Mkuu Hidaya, huu mchezo...hauhitaji hasira!
 
Haujaelewa, amesema kwenye kazi za kisiasa
How come kazi ya siasa zifadhiliwe na halmashauri? Au haujamwelewa mwenyekiti wako Mbowe.

Naamini hata Mbowe hafahamu nani ndiye afisa masurufu (accounting officer) wa Halmashauri.

Mkuu wa Wilaya ana bajeti yake, how achukue za halmashauri?
 
Back
Top Bottom