UKAWA Wakubali kuwa Bajeti ya Serikali ni vigumu kuipinga kwa Hoja

Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,793
1,082
Wadau, natumaini kuwa hamjambo.

Leo nimekuja kuwatonya juu ya jambo moja tu. nalo ni juu ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2014/2015. Mtonyaji wangu aliyepo Bungeni Dodoma amenitonya kuwa UKAWA wamethibitisha kuwa mwaka huu bajeti za Wizara zimekuwa realistic na kila wakijaribu kujenga hoja kupingana na Serikali wamekuwa wakishindwa vibaya mno. Wamesema kuwa ndani ya UKAWA wamejitathmini na kubaini kuwa wana kazi kubwa mbeleni ya kushawishi wananchi kuwa bajeti ya mwaka huu haina mashiko. Wamesema kuwa hata mtu ambaye wanamuamini kwa kujenga hoja nzito, John Mnyika safari hii amepwaya sana na sana sana anaishia kuangalia ulinganisho wa fesha zilizotengwa baina ya mwaka jana na mwaka huu. Mtonyaji amesema akinukuu kutoka kwa wana UKAWA wakisema kuwa kwa mwendo huu, Serikali ya CCM ni vigumu kuitoa madarakani.

Mtonyaji ameendelea kunihabarisha kuwa hata Wizara ya Nishati na Madini si kwamba kuna hoja nzito za wapinzani bali Reginald Mengi ameandaa kiasi kikubwa cha fedha kwa wabunge ili Prof Mhongo aonekane kuwa hafai kuwa Waziri wa wizara hiyo. Wanasema kuwa wakati waziri huyo atakapowasilisha bajeti ya Wizara yake, kuna wabunge kadhaa wameandaliwa si tu ndani ya UKAWA bali hata ndani ya CCM ili kumbomoa Prof kwa vile amekuwa kikwazo kwa Reginald Mengi na vibaraka wake.

Wamesema kuwa Mwenyekiti wa Bunge, Azan Zungu amekuwa kikwazo kwao. Wametolea mfano kuwa walipojaribu kujenga hoja juu ya Machinga, yeye aliidandia na akaacha nafasi yake ya Mwenyekiti na kuwa mchangiaji. Halikadhalika ilipokuja hoja ya kuwawezesha vijana. Wanasema kuwa hakika Zungu ni hatari zana katika kuneutralize hoja za upinzani kuliko Spika na Naibu wake. Pia wanasema kuwa Zungu ni mbabe kwa hoja na hakuna mwenye ubavu wa kushindana naye ndani ya UKAWA.

Nawatahadharisha ukawa kuwa msijaribu kuiga kunya mavi ya tembo mwisho wa siku mtapasuka msamba.

CCM HOYEEEEE!
 
UKAWA ni kama shimo la Tewa. Umejaa wahuni na watu waliofilisika kimawazo. Ndani ya UKAWA alili ndogo zimekuwa zikitawala akili kubwa
 
credibility ya jf inashuka kutokana na umbea kama huu eti mtonyaji...kwa hiyo umetonywa?
 
Uharo mtupu! Wote tumeshuhudia bajeti zikipitishwa kishabiki kwa kutumia wingi wa maccm tu,hoja mbadala zimetolewa lakini miccm imeendekeza ushabiki maandazi na kuzipitisha.
 
Punguza ushabiki wewe. Klass wako poa. We hukumckia machali juzi? Afu uselete mambo ambayo hayapo kuhusu mengi na waziri. Huyo waziri haitakii mema taifa hili co Mzalendo kabisa
 
Hii ni story ya isiyo na ukweli wo wote mkuu.Umetudanganya live na hatudanganyiki. Taarifa ni kwamba serikalini kuna hofu ya bajeti kupingwa ndo maana wizara ya maji ilihamishwa kwenye ratiba baada ya kuona hali ya hewa ni mbaya ili watafute mahali pa kuongeza kwenye weizara hiyo. Wizara ya Nishati ni matatizo matupu wala usimsingizie Mengi bila sababu. Wizara ni tabu tupu, kwani mengi aliiba bil 200 za walipa kodi wa Tanzania?
 
UKAWA ni kama shimo la Tewa. Umejaa wahuni na watu waliofilisika kimawazo. Ndani ya UKAWA alili ndogo zimekuwa zikitawala akili kubwa

wewe ni mpuuz tu,huna sifa za kuwa hata m/kiti wa mtaa halafu unajilinganisha na wabunge walioshinda kwa malaki ya kura tena katika mfumo huu wa kipuuzi wa uchaguzi? Nyambafuu
 
Wewe uliyetoa huu uzi kweli empty set aka interahamwe,Najua ungetoa hata data unabaki kushadadia tuu unaaa.
 
Wadau, natumaini kuwa hamjambo.

Leo nimekuja kuwatonya juu ya jambo moja tu. nalo ni juu ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2014/2015. Mtonyaji wangu aliyepo Bungeni Dodoma amenitonya kuwa UKAWA wamethibitisha kuwa mwaka huu bajeti za Wizara zimekuwa realistic na kila wakijaribu kujenga hoja kupingana na Serikali wamekuwa wakishindwa vibaya mno. Wamesema kuwa ndani ya UKAWA wamejitathmini na kubaini kuwa wana kazi kubwa mbeleni ya kushawishi wananchi kuwa bajeti ya mwaka huu haina mashiko. Wamesema kuwa hata mtu ambaye wanamuamini kwa kujenga hoja nzito, John Mnyika safari hii amepwaya sana na sana sana anaishia kuangalia ulinganisho wa fesha zilizotengwa baina ya mwaka jana na mwaka huu. Mtonyaji amesema akinukuu kutoka kwa wana UKAWA wakisema kuwa kwa mwendo huu, Serikali ya CCM ni vigumu kuitoa madarakani.

Mtonyaji ameendelea kunihabarisha kuwa hata Wizara ya Nishati na Madini si kwamba kuna hoja nzito za wapinzani bali Reginald Mengi ameandaa kiasi kikubwa cha fedha kwa wabunge ili Prof Mhongo aonekane kuwa hafai kuwa Waziri wa wizara hiyo. Wanasema kuwa wakati waziri huyo atakapowasilisha bajeti ya Wizara yake, kuna wabunge kadhaa wameandaliwa si tu ndani ya UKAWA bali hata ndani ya CCM ili kumbomoa Prof kwa vile amekuwa kikwazo kwa Reginald Mengi na vibaraka wake.

Wamesema kuwa Mwenyekiti wa Bunge, Azan Zungu amekuwa kikwazo kwao. Wametolea mfano kuwa walipojaribu kujenga hoja juu ya Machinga, yeye aliidandia na akaacha nafasi yake ya Mwenyekiti na kuwa mchangiaji. Halikadhalika ilipokuja hoja ya kuwawezesha vijana. Wanasema kuwa hakika Zungu ni hatari zana katika kuneutralize hoja za upinzani kuliko Spika na Naibu wake. Pia wanasema kuwa Zungu ni mbabe kwa hoja na hakuna mwenye ubavu wa kushindana naye ndani ya UKAWA.

Nawatahadharisha ukawa kuwa msijaribu kuiga kunya mavi ya tembo mwisho wa siku mtapasuka msamba.

CCM HOYEEEEE!

Hivi Bunge Maalum la Katiba bado linaendelea vile?Hizi elimu za viwango ya Mulugo hizi zimevuruga sana akili vijana hasa wasomi wetu.Si ajabu engine mnashindwa ktofautisha kati ya ideology na slogan.Sad but true!!!
 
Lengo la mtoa mada ni kumchambua mzee mengi ili aonekane ni kikwazo chamaendeleo katika kukwamisha bajeti ya wizara,kitu ambacho kwa namna moja ama nyingine hakiwezi kumchafua mzee wetu huyu mzalendo reginald mengi dhidi ya professor uchwara na myafiki sospeter muhongo.
 
Mkuu, ni kweli Mengi ni adui wa maendeleo ya Wizara ya Nishati. Anatumia fedha nyingi kuwarubuni wabunge huku akilipa mishahara kiduchu wafanyakazi wake
 
Hivi Bunge Maalum la Katiba bado linaendelea vile?Hizi elimu za viwango ya Mulugo hizi zimevuruga sana akili vijana hasa wasomi wetu.Si ajabu engine mnashindwa ktofautisha kati ya ideology na slogan.Sad but true!!!
Kwani kuna mahala pameandikwa abunge la Katiba?
 
Hii ni story ya isiyo na ukweli wo wote mkuu.Umetudanganya live na hatudanganyiki. Taarifa ni kwamba serikalini kuna hofu ya bajeti kupingwa ndo maana wizara ya maji ilihamishwa kwenye ratiba baada ya kuona hali ya hewa ni mbaya ili watafute mahali pa kuongeza kwenye weizara hiyo. Wizara ya Nishati ni matatizo matupu wala usimsingizie Mengi bila sababu. Wizara ni tabu tupu, kwani mengi aliiba bil 200 za walipa kodi wa Tanzania?
Mkuu Aweda. Yaelekea kuwa umechangia bila kujua uhalisia wake. Hapa hakuna mvutano baina ya Mengi na Wizara bali ni baina ya Mengi na Mhongo. Prof kakata mirija yao ya kifedhuli na sasa wamebaki kumuandama tu kwa vihoja visivyo vya maana
 
Ni Kweli Ya Kwamba UKAWA Si Rahisi Kuitoa CCM Madarakani!,lakini Madai Ya UKAWA Ni Ya Msingi Na Yanamashiko,kama Lile La Kutaka Muungano Wenye Haki Na Usawa Kwa Pande Zote Mbili Za Muungano!
 
Hivi kumbe.na bunge hili lina ukawa! Nilimskia madam spika akiweka kumbukumbu sawa siku Mbowe anatangaza mawaziri wake kuwa UKAWA ni hukohuko bunge maalum Sio humu kwa bunge lake. Sasa hii ukawa inayozungumzwa hapa ni ipi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom