Sikubaliani na ushabiki usio na mantiki kama wa mtoa mada hii. Kama kweli wewe unaguswa na matatizo yanayowazunguka watanzania kwa mfumo wa bajeti ya nchi yetu hungeweza kufurahia mtu yeyote anayebeza wanaojaribu kuboresha bajeti hizo ili kuweza kutatua matatizo yetu. Kwa mtazamo wangu ninaamini kuwa vikao vya bunge havitakiwi kuendeshwa na mtu mwenye upendeleo wa chama. Anachokifanya Zungu na wewe mtoa mada hapa ni ulimbukeni na huenda pia kwa kutojua hali halisi waliyonayo watanzania kiuchumi. Actually Zungu anatakiwa kukemewa asitafute umaarufu ambao utawaumiza watanzania baadae