Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
KAMBI rasmi ya upinzani bungeni inatilia mashaka uwezo na dhamira ya Benki Kuu (BoT) kufanya ujasusi wa miamala ya fedha.
Ni katika kuzuia utakatishaji wa fedha sambamba na uwezo mdogo wa kitengo kinachoshughulika na masuala hayo-Financial Intelligence Unit (FIU) ambacho kinazuia utakatishaji wa fedha.
Hayo yameainishwa katika Hutuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge iliyosomwa na David Silinde, Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo katika Wizara ya Fedha na Mipango katika hotuba ya mapato na makadirio ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Silinde amesema kuwa, kambi ya upinzani haina imani na kitengo hicho na kuwa (FIU) haina uwezo wa kufanya uchunguzi, wala kuendesha mashitaka dhidi ya utakatishaji wa fedha haramu jambo ambalo ni mwanya unaotumiwa na watu waovu na mafisadi kama ilivyokuwa katika wizi wa Mabilioni ya Rada, wizi wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow na wizi wa fedha katika Mkopo wa Serikali dola milioni 600 kutoka Stanbic Bank.
Amesema kuwa, serikali imeunda kitengo cha FIU ambacho kina mamlaka ya kiutawala pekee na huishia kufanya uchambuzi wa taarifa za miamala ya fedha na kuziwasilisha ama Jeshi la Polisi au PCCB, wakati huo huo PCCB inalazimika kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili atoe ruhusa ya kufungua mashitaka.
Ameleeza kuwa, mfumo wa (FIU) ya Tanzania ni “administrative model” (mfumo wa kiutawala) wakati mfumo imara zaidi ni ule wa “Judicial Model” (mfumo wa kimahakama ) ambao unakiongezea nguvu kitengo hicho cha kuzuia miamala ya biashara haramu za kutakatisha fedha.
Hata hivyo kambi rasmi ya upinzani bungeni inaishauri serikali kuimarisha kitengo cha FIU kwa kukiundia Mfumo wa Judicial Model ili kuepuka aibu ambayo Taifa letu imekuwa ikiipata hasaa aibu kubwa iliyotupata nchini Uingereza , ili kuwana na uwezo wa kurudisha fedha za zilizoibiwa kwa njia ya kifisadi wakati kazi kama hiyo ingeweza kufanywa na vyombo vya hapa nchini endapo vingeimarishwa kama ambavyo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inavyoshauri kuimarisha kitengo cha FIU.