UKAWA wahamasishana kujitokeza kwa wingi Polisi kumuona Lissu

Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
964
2,355
VIONGOZI na wanachama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wameombwa kujitokeza kwa wingi makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es Salaam, kufuatilia hatma ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
Anatuhumiwa “kumtusi rais wa Jamhuri, John Pombe Magufuli.” Anadaiwa kumuita “dikteta uchwara.”

Kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mbunge wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea, viongozi wa UKAWA wanaomba kufika kwa wingi makao makuu ya polisi mchana huu kufuatilia hatma ya kiongozi wao.

Akindika katika mtandao wa wabunge wa UKAWA, mbunge huyo machachari wa Ubungo anaeleza, “…kama ilivyoelezwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Upinzani, Tundu Antiphas Lissu, amekamatwa mkoani Singida na sasa yuko njiani kuletwa Dar es Salaam.

Kubenea anasema, kwa kuwa haijafahamika mahali ambako Lissu atafikishwa, anawaomba wabunge wa UKAWA, madiwani, wachama na mashabiki wengine wa vyama hivyo, kujumuika kwa pamoja ili kuungana naye katika dhahama inayomkabili.

Wahe, wabunge, madiwani, wanachama na viongozi wengine wa vyama vinavyounda UKAWA, kwa kuwa hatufahamu Lissu atapelewa katika kituo gani cha polisi, naomba tujumuike kwa pamoja kuelekea makao makuu ya polisi,” anaeleza Kubenea.

Anasema, “huko ndiko tutakaolezwa na mkuu wa jeshi la polisi, IGP Ernest Mangu, mahali aliko Lissu wetu.”

Kubenea amesema, ameweza kuongea na Lissu na kumthibitishia kuwa yuko njiani analetwa jijini Dar es Salaam kutokea Dodoma.
Amesema, katika mazungumzo yake na Lissu, amemueleza kuwa mpaka sasa hajaelezwa na polisi sababu za kumshikilia.

Lissu aliyekamatwa mkoani Singida alilazwa katika kituo kikuu cha polisi cha Dodoma na amesafirishwa alfajiri ya leo kuelekea Dar es Salaam.
Amenyang’anywa simu zake zote mbili kwa madai kuwa amekuwa akifanya mawasiliano na viongozi wenzake, wanachama na familia, jambo ambalo jeshi la polisi limesema, “halikubaliani nalo.”

1470306618900-jpg.375937
 
IMG-20160804-WA0001-150x150.jpgVIONGOZI na wanachama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wameombwa kujitokeza kwa wingi makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es Salaam, kufuatilia hatma ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
Anatuhumiwa “kumtusi rais wa Jamhuri, John Pombe Magufuli.” Anadaiwa kumuita “dikteta uchwara.”

Kwa mujibu wa ujumbe uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, viongozi wa UKAWA wanaomba kufika kwa wingi makao makuu ya polisi mchana huu kufuatilia hatma ya kiongozi wao.

Akindika katika mtandao wa wabunge wa UKAWA, mbunge huyo machachari wa Ubungo anaeleza, “…kama ilivyoelezwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Upinzani, Tundu Antiphas Lissu, amekamatwa mkoani Singida na sasa yuko njiani kuletwa Dar es Salaam.

Kubenea anasema, kwa kuwa haijafahamika mahali ambako Lissu atafikishwa, anawaomba wabunge wa UKAWA, madiwani, wachama na mashabiki wengine wa vyama hivyo, kujumuika kwa pamoja ili kuungana naye katika dhahama inayomkabili.

Wahe, wabunge, madiwani, wanachama na viongozi wengine wa vyama vinavyounda UKAWA, kwa kuwa hatufahamu Lissu atapelewa katika kituo gani cha polisi, naomba tujumuike kwa pamoja kuelekea makao makuu ya polisi,” anaeleza Kubenea.

Anasema, “huko ndiko tutakaolezwa na mkuu wa jeshi la polisi, IGP Ernest Mangu, mahali aliko Lissu wetu.”

Kubenea amesema, ameweza kuongea na Lissu na kumthibitishia kuwa yuko njiani analetwa jijini Dar es Salaam kutokea Dodoma.

Amesema, katika mazungumzo yake na Lissu, amemueleza kuwa mpaka sasa hajaelezwa na polisi sababu za kumshikilia.

Lissu aliyekamatwa mkoani Singida alilazwa katika kituo kikuu cha polisi cha Dodoma na amesafirishwa alfajiri ya leo kuelekea Dar es Salaam.

Amenyang’anywa simu zake zote mbili kwa madai kuwa amekuwa akifanya mawasiliano na viongozi wenzake, wanachama na familia, jambo ambalo jeshi la polisi limesema, “halikubaliani nalo.”
kama kapokonywa simu alizungumza nae vipi?
 
Kaongea nae kwa njia gani, polisi wamemuruhusi vp kuwasiliana na mtu huku yuko chini ya ulinzi. Hv mnatuona hatuna idea yoyote yan mkisema tu tukubali. Teh! Teh! Na kama alinyanganywa simu zote sasa wamewasiliana vp. Acheni maigizo
 
Kwakweli huyu jamaa asipojitazama anaweza asimalize miaka mitano..watu wameshachoka ubabe wake

Mungu mkubwa naamini lisu atapatikana akiwa salama
 
Kaongea nae kwa njia gani, polisi wamemuruhusi vp kuwasiliana na mtu huku yuko chini ya ulinzi. Hv mnatuona hatuna idea yoyote yan mkisema tu tukubali. Teh! Teh! Na kama alinyanganywa simu zote sasa wamewasiliana vp. Acheni maigizo

Hii akili ya kijinga kweli? Mtu anawekwa rumande na simu zinachukuliwa na anaweza ongea na ndugu itakuwa Lissu?
 
Huu ni uonezi Na unyanyasaji wa hali ya juu....inakera sana.!
 
Naombeni msaada hamna jinsi ya kublock mtu humu! Kuna mtu kama Lizaboni kwangu ni kero anajaza server za JF

Kuna kitu kinaitwa ignore: Kwenye profile yako kuna kitu kinaitwa people you igore, unaclick hapo then unamweka mtu unayetaka kumuignore, ukishasevu changes umemaliza.
 
kama kakamatwa kiutaratibu na tunajua atahojiwa then apelekwe mahakamani ... sisi twaenda kufanya nini ... kushindana na jeshi la polisi ama kuvamia kituo cha polisi ama kumtorosha hapo kituoni ama tunaenda kwa impact zipi kwa mfano... TUACHE SHERIA ZIFANYE KAZI ZAKE ... MIMI BINAFSI NAPENDA WATU TUPIGE KAZI MAMBO YAKAE SAWA MAFISADI WAKAMATWE UCHUMI WA NCHI UWE THABITI ILA UHAMASISHAJI WA KUPAMBANA NA KITU AMBACHO KWANGU KAMA MTANZANIA KITANIYUMBISHA NI BORA NIWAANGALIE KWENYE TV KAMA NINAVYOANGALIA MOVIES NIZIPENDAZO.

TUACHE KUTAFUTA UMAARUFU KWA VURUGU TUTAFUTE UMAARUFU KWA MBINU ZA KULETA MAENDELEO KATIKA TAIFA LETU
 
Back
Top Bottom