YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,995
Gazeti la mwananchi limeandika kuwa UKAWA wamembwagia zigo la swala la uchaguzi wa Zanzibar Magufuli alifanyie kazi.Hivi hawa UKAWA katiba ya nchi wanaisoma au hawaisomi? Swala la uchaguzi wa Zanzibar si jambo la muungano.Utamwagiaje Raisi jambo ambalo si la muungano wakati unajua yule ni Raisi wa muungano.
Huu ndio wakati muafaka wa watanzania bara kuwaonyesha wazanzibari kuwa Zanzibar ni nchi kama wanavyodai na kama walivyopitisha katiba yao ya nchi ya Zanzibar bila kushirikisha serikali ya muungano kwa kuwa walisema wao ni nchi kamili isiyohitaji kuingiliwa kwenye kuunda katiba yake wala uendeshaji wa mambo yake yakiwemo ya uchaguzi.
Ile Katiba ya Zanzibar waliyojipitishia Wazanzibari wakakubaliana sasa ndio inafanya kazi yake.2015 NDIO IMEINGIA KAZINI KISAWA SAWA.
Wabunge wa Tanzania bara wote unganeni kwa hili bila kujali vyama na kutaka swala hilo wakalimalize wanzanibari wenyewe kwenye nchi yao asiweko kibaraka wa kushupalia lijadiliwe.Kumbukeni wazanzibari wanavyokuwa kitu kimoja wakishupalia swala lao la maslahi ya Zanzibar.Seif shariff Hamad anaona Tanzania bara ndiko kuna watu wasiojitambua wakiwemo wabunge hasa wa UKAWA ndio anataka awatumie kama vibaraka wake wa kuingiza hoja ya jambo lisilo la muungano la uchaguzi wa Zanzibar bungeni.Tafadhali bunge liheshimu katiba.
Wao ni nchi wana katiba,raisi,jaji mkuu,tume yao ya uchaguzi, raisi wao mahakama zao nk waende wakamalizane.
Sitegemei Bunge nalo lijitie halisomi katiba ya jamhuri ya muungano kuliingiza hilo swala kwenye mijadala wakati si swala la muungano