UKAWA wa Uganda watoa uzushi kwamba wamarekani wanaondolewa Uganda

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Habari wadau!

Katika hali ya kusikitisha upinzani nchini uganda (ukawa) wametoa propaganda zinazoonyesha barua kutoka ubalozi wa marekani ukiwataka wamarekani na rafiki zao kuondoka mara moja uganda sababu ya fujo japo ubalozi wa marekani umekanusha habari hizo. Huu ni muendelezo wa wafuasi wa upinzani afrika (aka wafuasi wa Donald Triump) kufanya siasa chafu zikifananishwa na zile za Ukawa ya tanzania;
1.Kwamba TB Joshua kaja na ujumbe wa ''Mungu''
2.kikwete kupelekwa ICC,ICJ
3.Tanzania haitakalika.
4.Zanziba damu kumwagika nk

Wito wangu kwa vijana tuwe wazalendo na nchi zetu kwani jumbe kama hizo zinachafua nchi zetu bila kujali itikadi demokrasia sio lazima upinzani kuingia ikulu, UK,US,Urusi, China zote zina demokrasia zao na wako wananchi wao hawaridhiki lakini hawachafui nchi zao kwa maslahi ya tumbo. (nimeweka kiambatanisho kwa ufuatiliaji)
 

Attachments

  • 12744381_10207581492728438_8399710032282210971_n.jpg
    12744381_10207581492728438_8399710032282210971_n.jpg
    18.8 KB · Views: 37
Back
Top Bottom