UKAWA tunaomba ufafanuzi wa kina kuhusu wagombea wa CCM kupita bila kupingwa

mchambuzixx

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
1,292
943
Jamani viongozi wa CHADEMA tunaomba ufafanuzi, tumesikia kuna baadhi ya maeneo CCM wamepita baada ya CHADEMA kushindwa kuweka mgombea au kuwekewa pingamizi la kuhusiana na mihuri, lakini kuna habari tulizisikia kuwa hakuna mgombea wa chama chochote atakayeenguliwa kwa kushindwa kujaza mhuri wa chama.

Naomba mtoe ufafanuzi na kuna maeneo kama Same nasikia katibu alitumia mhuri wake binafsi badala ya chama.

Hivi haya mambo yanatokea kwenye chama kinachojiita chama makini huko Same hakukuwa na mwenyekiti au viongozi wengine hadi huyo katibu anafanya hayo inatia shaka.

Tunaomba ufafanuzi je kushindwa kujaza mhuri wa chama kunasababisha mgombea kutolewa ?
 
Mkuu mchambuzi!
Waziri mkuu alishatoa kauli bungeni kwamba wagombea wote wa mitaa na vijiji, fomu zao zitapitishwa na mihuri ya matawi! hivyo huyo mama wa same, hata kama muhuri usingekuwa na jina lake, bado ungekuwa batili.
Kumbuka mgombea wa udiwani anagongewa mhuri wa kata! na mgombea wa ubunge anagongewa mhuri wa jimbo.
 
CCM ni chama dume. Wengine ni cha mtoto

Chama dume cha Mafisadi... Singasinga kawatia mfukoni kuanzia Mwenyekiti wenu La-profesar mpaka wasakatonge kama wewe!! Chama makini kimealikwa Bunge la Ulaya kuzungumzia mstakabali wa taifa kwa siku zijazo..

Tangu mfumo wa vyama vingi uanze sijawahi kusikia hiki Chama chakavu cha Magamba kialikwe na taasisi kubwa duniani.. Sanasana utasikia kimealikwa kwenye sherehe za kuadhimisha sijui nn ya chama cha kikomunisti china,,, kwenye mabegi mnaweka na meno yetu ya tembo.. Pu....mbavu..
 
Baadhi ya sehemu upinzani haujakubalika sawasawa,sehemu zingine CCM wamewanunua wapinzani,sehemu zingine wapinzani wameondolewa kwa hila na sehemu zingine wapinzani wamejiondoa baada ya kutishiwa kubambikiziwa kesi za mauaji na CCM.
 
Asante Mkuu..!!!

BACK TANGANYIKA
 
haaaaaaa, new colonization style by using Puppet leaders
 
Sehemu nyingine ccm wamekosa wawakilishi...kama sumbawanga mjini,..ccm wanafuata watu kuwaomba wagombee nafasi za uenyekiti...sumbawanga mjini watu hawataki kusikia ccm
 
Baadhi ya sehemu upinzani haujakubalika sawasawa,sehemu zingine CCM wamewanunua wapinzani,sehemu zingine wapinzani wameondolewa kwa hila na sehemu zingine wapinzani wamejiondoa baada ya kutishiwa kubambikiziwa kesi za mauaji na CCM.

Na bado, mtapona tu!
 
Jamani viongozi wa CHADEMA tunaomba ufafanuzi, tumesikia kuna baadhi ya maeneo CCM wamepita baada ya CHADEMA kushindwa kuweka mgombea au kuwekewa pingamizi la kuhusiana na mihuri, lakini kuna habari tulizisikia kuwa hakuna mgombea wa chama chochote atakayeenguliwa kwa kushindwa kujaza mhuri wa chama.

Naomba mtoe ufafanuzi na kuna maeneo kama Same nasikia katibu alitumia mhuri wake binafsi badala ya chama.

Hivi haya mambo yanatokea kwenye chama kinachojiita chama makini huko Same hakukuwa na mwenyekiti au viongozi wengine hadi huyo katibu anafanya hayo inatia shaka.

Tunaomba ufafanuzi je kushindwa kujaza mhuri wa chama kunasababisha mgombea kutolewa ?

Mkuu nilifikiria sana kufungua uzi wangu maalumu lakini kwa vile uzi wako una maudhui yanayofanan na yangu basi naomba nikolezee hapo hapo kwako.

Wakuu wote
Kuna makosa ambayo Chadema au UKAWA kwa ujumla wanayafanya kwa aidha kutokana na uelewa mdogo wa masuala ya uchaguzi au pengine elimu ndogo hasa kwa viongozi wa ngazi ya chini. CCM inatumia makosa madogo madogo kabisa ambayo kimsingi kisheria yana uzito wake. Mfano halisi ni kuengeluwa kwa wagombea wa Chadema katika kijiji cha Nakawale kata ya Muhukuru wilaya ya Songea vijijini. Hawa walifanya makosa ambayo nayaita ya kijinga sana.
Wagombea wetu waliwekewa pingamizi na CCM kwa ujinga wetu wenyewe na hasa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maslahi ya chama. Tazama makosa yafuatayo;
1. La kwanza wagombea watatu walienguliwa baada ya kushindwa kuthibitisha uanachama wao kwa Chadema. Nilimuhoji msimamizi wa uchaguzi. Akaamua kutonijibu bali kunipa karatasi yenye makosa kwa namna walivyojaza. Kwa kweli ilisikitisha sana. CCM walipinga kuwa hakuna mgombea huru hadi sasa. Kila mgombea lazima awe mwanachama wa chama cha siasa. Sasa wagombea wetu walipotakiwa kuthibitisha uanachama wao walishindwa kuonyesha kadi za chama. Siku tatu msimamizi aliwapa kuthibitisha lakini hadi dakika ya mwisho walishindwa. Je kosa hili walionewa?
2. Pili mwingine alishindwa kuthibitisha umri wake. Akawekewa pingamizi na CCM kuwa kadanganya umri. Msimamizi akamwambia athibitishe kwa document yoyote ile juu ya umri wake lakini hadi baada ya siku tatu akashindwa. Akaondolewa.
3. Tatu wagombea wengine wawili walijaza fomu zao kwa majina tofauti. Sehemu nyingine kwa mfano niliona aliandika Mohamed Said Mpanju na pengine akaandika Mohamed Said Njole. Hivi kweli hatujui kuwa majina ni kitu muhimu sana? Kosa dogo sana linakufanya ukose haki yako. Mfano mtu anayeitwa Alois ni tofauti na mtu huyu huyu anayeitwa Aloyse. Hawa ni watu wawili tofauti japo wanapotamkwa huwezi kuona utofauti wao.
4. Wanachama wetu wanapaswa kujua pia kifupi cha chama chetu kinatambulika kisheria. Kinaitwa Chadema na si CDM kama tunavyofupisha sisi humu JF. Sasa kuna watu pia bado kwenye legal document wanataka kuandika CDM. Haya ni makosa madogo lakini ni makubwa sana. Makosa haya yatajirudia tena hata kwenye ngazi ya ubunge na udiwani kama hayatarekebishwa kwa kutolewa elimu.
 
Baadhi ya sehemu upinzani haujakubalika sawasawa,sehemu zingine CCM wamewanunua wapinzani,sehemu zingine wapinzani wameondolewa kwa hila na sehemu zingine wapinzani wamejiondoa baada ya kutishiwa kubambikiziwa kesi za mauaji na CCM.

Haya unayoyaeleza hapa ni woga wa kijinga sana. Binafsi huwa nawaambia ukweli kuwa mtawatisha wajinga wenzenu si kwa mwelewa. Akubambikie kesi atokenayo wapi? Ina maana hiyo kesi unayo ndio maana wanakubambikia? Hata tuache unyonge usio na maana katika hili.
 
Chama dume cha Mafisadi... Singasinga kawatia mfukoni kuanzia Mwenyekiti wenu La-profesar mpaka wasakatonge kama wewe!! Chama makini kimealikwa Bunge la Ulaya kuzungumzia mstakabali wa taifa kwa siku zijazo..

Tangu mfumo wa vyama vingi uanze sijawahi kusikia hiki Chama chakavu cha Magamba kialikwe na taasisi kubwa duniani.. Sanasana utasikia kimealikwa kwenye sherehe za kuadhimisha sijui nn ya chama cha kikomunisti china,,, kwenye mabegi mnaweka na meno yetu ya tembo.. Pu....mbavu..

Chama Dume hiyo
 
Mkuu nilifikiria sana kufungua uzi wangu maalumu lakini kwa vile uzi wako una maudhui yanayofanan na yangu basi naomba nikolezee hapo hapo kwako.

Wakuu wote
Kuna makosa ambayo Chadema au UKAWA kwa ujumla wanayafanya kwa aidha kutokana na uelewa mdogo wa masuala ya uchaguzi au pengine elimu ndogo hasa kwa viongozi wa ngazi ya chini. CCM inatumia makosa madogo madogo kabisa ambayo kimsingi kisheria yana uzito wake. Mfano halisi ni kuengeluwa kwa wagombea wa Chadema katika kijiji cha Nakawale kata ya Muhukuru wilaya ya Songea vijijini. Hawa walifanya makosa ambayo nayaita ya kijinga sana.
Wagombea wetu waliwekewa pingamizi na CCM kwa ujinga wetu wenyewe na hasa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maslahi ya chama. Tazama makosa yafuatayo;
1. La kwanza wagombea watatu walienguliwa baada ya kushindwa kuthibitisha uanachama wao kwa Chadema. Nilimuhoji msimamizi wa uchaguzi. Akaamua kutonijibu bali kunipa karatasi yenye makosa kwa namna walivyojaza. Kwa kweli ilisikitisha sana. CCM walipinga kuwa hakuna mgombea huru hadi sasa. Kila mgombea lazima awe mwanachama wa chama cha siasa. Sasa wagombea wetu walipotakiwa kuthibitisha uanachama wao walishindwa kuonyesha kadi za chama. Siku tatu msimamizi aliwapa kuthibitisha lakini hadi dakika ya mwisho walishindwa. Je kosa hili walionewa?
2. Pili mwingine alishindwa kuthibitisha umri wake. Akawekewa pingamizi na CCM kuwa kadanganya umri. Msimamizi akamwambia athibitishe kwa document yoyote ile juu ya umri wake lakini hadi baada ya siku tatu akashindwa. Akaondolewa.
3. Tatu wagombea wengine wawili walijaza fomu zao kwa majina tofauti. Sehemu nyingine kwa mfano niliona aliandika Mohamed Said Mpanju na pengine akaandika Mohamed Said Njole. Hivi kweli hatujui kuwa majina ni kitu muhimu sana? Kosa dogo sana linakufanya ukose haki yako. Mfano mtu anayeitwa Alois ni tofauti na mtu huyu huyu anayeitwa Aloyse. Hawa ni watu wawili tofauti japo wanapotamkwa huwezi kuona utofauti wao.
4. Wanachama wetu wanapaswa kujua pia kifupi cha chama chetu kinatambulika kisheria. Kinaitwa Chadema na si CDM kama tunavyofupisha sisi humu JF. Sasa kuna watu pia bado kwenye legal document wanataka kuandika CDM. Haya ni makosa madogo lakini ni makubwa sana. Makosa haya yatajirudia tena hata kwenye ngazi ya ubunge na udiwani kama hayatarekebishwa kwa kutolewa elimu.

hapo nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom