UKAWA ni Genge hatari kwa amani, utulivu na maslahi mapana ya Tanzania | Page 9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UKAWA ni Genge hatari kwa amani, utulivu na maslahi mapana ya Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by meningitis, Sep 6, 2015.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2015
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Mimi nilikuwa muumini makini wa Chama makini cha upinzani kilichojijenga taratibu mpaka kuonekana kuwa pengine kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

  CHADEMA ilikuwa taratibu bila misukosuko mingi mpaka pale kilipoanza kuonekana pengine kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

  Wananchi walianza kazi kwa umakini kabisa wa kuipa chadema majimbo ya ubunge kadhaa na serikali za mitaa.

  Wananchi walianza kuitambua na kuisaidia chadema kwa michango ya kadiri mbalimbali.

  Ni maumivu makali kwa CHADEMA kupoteza focus na kutaka kukimbilia kile ambacho wananchi hawakukiandaa au kukipanga kwa ajili yao.

  Hii ina maana Chadema itarudi miaka 20 nyuma na mbaya zaidi kuiacha Tanzania bila mbadala wa Chama bora cha upinzani.

  KUHUSU GENGE LA UKAWA:

  Itoshe kusema kuwa UKAWA ni genge hatari sana kwa usalama na Ustawi wa Taifa letu kwa sababu au chambuzi zifuatazo:

  1 - Edward Lowassa:
  Yuko serious katika kuutaka urais na alipenda kwa udi na uvumba kuupata urais kupitia ccm ingawa ilishindikana iwe kwa fitina au kwa kukosa vigezo. Huyu yuko Ukawa kwa lengo la urais tu na anaitumia chadema kama chombo cha kuupata urais. Anaweza akawa na sababu zake lakini sitajadili kwa leo. Lakini haipendi Chadema au UKAWA.

  2 - Maalim Seif na CUF:
  Huyu naye ni mtaka urais tu lakini anaweza kuwa na ajenda yake ile ile iliyobebwa na CUF Zanzibar yaani kuitaka Zanzibar huru. Alitulizwa baada ya kupewa cheo lakini baada ya vuguvugu la katiba na shinikizo la kichama amejikuta akianza chokochoko upya.

  Pia tusisahau CUF inaungwa mkono na makundi kama yale ya uamsho kiasi cha kumfanya mgombea urais wa UKAWA kutamka hadharani kuwa atawaachia huru watuhumiwa wa ugaidi.

  3 - CHADEMA Asilia na Maslahi:
  Kuna kundi la wanachadema walio serious na kutaka mabadiliko ya kweli.kundi hili limekatishwa tamaa na mambo makubwa mawili yaliyotokea yaani kumpokea lowassa bila maelezo ya kueleweka na kumpa kijiti cha kugombea urais,pili kukatwa kwa Dr Slaa na kutothaminiwa kwa mchango wake ndani ya Chadema.

  Chadema maslahi ni kina Mbowe na washkaji kibao kutoka pande za Arusha na Moshi. Hawa wako kimaslahi zaidi, Issue kwao ni chama kinaingizaje fedha au mikutano inaingizaje fedha au nguo na adverts za chama zinaingizaje fedha. Hawa wanaendesha Chadema kama kamati ya harusi za kichaga.

  4 - Team Lowassa, Ulipo tupo na 4UMovement:
  Hili ni genge ndani ya genge! Katika kundi hili kuna watoto wa kishua wanaosubiri kupiga dili kama za watoto wa vigogo.

  Katika kundi hili kuna waliokosa ajira na fursa na hivyo kujishikiza kwa lowassa ili ikitokea kapata na wao watoke(hawajui uhuni wa mwanasiasa)

  Katika kundi hili kuna watoto ambao wako tu kwenye age yao ya 'fantancy' na kuburudika na maisha.

  5 - WanaCCM viongozi waliomfuata Lowassa:
  Hapa kuna mchanganyiko wa waliokatwa kwa kuwa ni makapi haswa. Pia wako walioshtukia dalili za kukosa wakigombea kupitia CCM(Lembeli).

  Pia wapo wanaojaribu kuibuka upya kwa mgongo wa Lowassa. Humu pia kuna mashushu kutoka CCM.

  6 - NCCR na Mbatia na NLD:
  Hili ni kundi lisilojielewa linahitaji nini. Mbatia anaweza kuwa ni mpiga dili flani hivi na pia baada ya kuonja ubunge wa kuteuliwa anatamani angepata ubunge ili aweke mambo sawa.

  7 - Wanaharakati na waandishi:
  Hawa wako katika kutegemea nafasi za kuteuliwa kama ilivyozoeleka huku wakisahau kuna vijana wengi na wenye weledi. Wengi wao wameumizwa na tendo la CCM kukata na kuvunja makundi na option waliyobakiwa nayo ni kujipendekeza UKAWA.

  8 - Wafanyabiashara:
  Hawana uhakika kabisa wa EL kushinda nje ya CCM na wamebaki kuuma na kupuliza.
  Ingawa kuna wachache bado wanagamble kuendelea kuamini katika EL kuchukua kijiti.

  9 - Wachungaji/Maaskofu:
  Ni wachache na wanajaribu kutumia karata ya zamu ya mlutheri lakini kimsingi wanataka kutetea matumbo yao tu.


  Ukiwa na genge la namna hii na likiwa halina uongozi au miongozo inayoeleweka utakuwa unaongelea nchi iliyoanguka. Ni lazima genge hilo lipate Kiongozi na Muongozo kwanza ndio ufikirie kuwapa nchi.
   
 2. T

  TINGISHAA Member

  #161
  Nov 20, 2015
  Joined: Aug 13, 2015
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa unatetea genge lenu au vp! hii parapata na mdomo mrefu unajipendekeza kwa nani, unamshutumu kila wa ukawa, wewe na genge lenu mnautakatifu gani! ni juzi tu jizi lililokomaa ati ni mwenyekiti ktk kamati ya bunge kwa wakati mrefu nchi hii ni ya maigizo lkn siku kweli itaposimama mtaumbuka wengi na hapo ndio maendeleo yatapokuja lkn kwa mtindo huu wakupinduwa matokeo kwa maslahi binafsi hatwendi popote.
   
 3. luginyo

  luginyo JF-Expert Member

  #162
  Nov 21, 2015
  Joined: May 26, 2013
  Messages: 1,259
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  Sio kweli ni genge hatari huo sema ni mtazamo wako Mtoa mada mi nachojua watanzania wengi hawapendi kuambiwa unwell ndicho ukawa wanachokifanya
   
 4. A

  Angelo007 JF-Expert Member

  #163
  Nov 21, 2015
  Joined: Dec 1, 2013
  Messages: 1,784
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  Mimi nina uhakika tume ingekua huru CCM hisingekua ikulu sasa hv.Dawa yenu katiba ya warioba.
   
 5. M

  MANTONGA JF-Expert Member

  #164
  Nov 21, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 527
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Mliambiwa katiba itayotumika ni ya 1977
   
 6. luginyo

  luginyo JF-Expert Member

  #165
  Nov 22, 2015
  Joined: May 26, 2013
  Messages: 1,259
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  Mi naona hakuna amani hiki ni kisiwa cha uvumilivu
   
 7. Ishmael

  Ishmael JF-Expert Member

  #166
  Nov 24, 2015
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Ukawa Kwisha habari yao.
   
 8. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #167
  Nov 24, 2015
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 19,167
  Likes Received: 1,889
  Trophy Points: 280
  Mchungaji feki , umepata njia ya kula ???
   
 9. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #168
  Nov 24, 2015
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 19,167
  Likes Received: 1,889
  Trophy Points: 280

  HII NDIYO CCM na ugaidi wao   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #169
  Apr 2, 2016
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,608
  Likes Received: 14,669
  Trophy Points: 280
  Muwe mnafikiria kabla ya kupost
   
 11. habari ya hapa

  habari ya hapa JF-Expert Member

  #170
  Apr 2, 2016
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 12,154
  Likes Received: 7,324
  Trophy Points: 280
  Ovyooo kabisa
   
 12. chipaka.com

  chipaka.com JF-Expert Member

  #171
  Apr 2, 2016
  Joined: Dec 5, 2015
  Messages: 2,725
  Likes Received: 1,059
  Trophy Points: 280
  Hatushangazwi na post za wasubiri, buku 7,wa Lumumba
   
 13. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #172
  Apr 2, 2016
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,608
  Likes Received: 14,669
  Trophy Points: 280
  Hutakiwi kushangaa unatakiwa kutafakari....
   
 14. chipaka.com

  chipaka.com JF-Expert Member

  #173
  Apr 2, 2016
  Joined: Dec 5, 2015
  Messages: 2,725
  Likes Received: 1,059
  Trophy Points: 280
  Kutafakari post za Lumumba ni sawa na kucheza pool, table asubuhi
   
 15. K

  Kifoi JF-Expert Member

  #174
  Apr 4, 2016
  Joined: May 12, 2007
  Messages: 863
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 80
  nenda ukatafute bangi uvute
   
 16. georgemwaipungu

  georgemwaipungu JF-Expert Member

  #175
  Apr 5, 2016
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 2,779
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Tatizo bangi zenu mnavutia chooni kichwa kinajaa kinyesi
   
 17. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #176
  Sep 27, 2016
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,608
  Likes Received: 14,669
  Trophy Points: 280
  Genge linavunjika sasa
   
 18. Sharif

  Sharif JF-Expert Member

  #177
  Sep 29, 2016
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 2,466
  Likes Received: 1,660
  Trophy Points: 280
  vipi kuhusu yule jamaa anaeagiza watu watumbukizwe visimani ?
   
 19. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #178
  Feb 25, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,608
  Likes Received: 14,669
  Trophy Points: 280
  grngre grengre Sasa ni dhahiri kuwa Ukawza ni genge la wakwepa kodi na sasa wala ngada
   
 20. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #179
  Dec 3, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,608
  Likes Received: 14,669
  Trophy Points: 280
  Genge linapukutika
   
 21. chizcom

  chizcom JF-Expert Member

  #180
  Dec 3, 2017
  Joined: Jul 31, 2016
  Messages: 1,308
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  pale muembe yanga ndipo ilipo zaliwa ukawa ILIKUWA CCM yote hayo yalitajwa.watanzania ni wepesi kusahau ya nyuma.ndo maana hata historia zetu hatuna
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...