Elections 2015 UKAWA ni Genge hatari kwa amani, utulivu na maslahi mapana ya Tanzania

Mimi nilikuwa muumini makini wa Chama makini cha upinzani kilichojijenga taratibu mpaka kuonekana kuwa pengine kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

CHADEMA ilikuwa taratibu bila misukosuko mingi mpaka pale kilipoanza kuonekana pengine kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

Wananchi walianza kazi kwa umakini kabisa wa kuipa chadema majimbo ya ubunge kadhaa na serikali za mitaa.

Wananchi walianza kuitambua na kuisaidia chadema kwa michango ya kadiri mbalimbali.

Ni maumivu makali kwa CHADEMA kupoteza focus na kutaka kukimbilia kile ambacho wananchi hawakukiandaa au kukipanga kwa ajili yao.

Hii ina maana Chadema itarudi miaka 20 nyuma na mbaya zaidi kuiacha Tanzania bila mbadala wa Chama bora cha upinzani.

KUHUSU GENGE LA UKAWA:

Itoshe kusema kuwa UKAWA ni genge hatari sana kwa usalama na Ustawi wa Taifa letu kwa sababu au chambuzi zifuatazo:

1 - Edward Lowassa:
Yuko serious katika kuutaka urais na alipenda kwa udi na uvumba kuupata urais kupitia ccm ingawa ilishindikana iwe kwa fitina au kwa kukosa vigezo. Huyu yuko Ukawa kwa lengo la urais tu na anaitumia chadema kama chombo cha kuupata urais. Anaweza akawa na sababu zake lakini sitajadili kwa leo. Lakini haipendi Chadema au UKAWA.

2 - Maalim Seif na CUF:
Huyu naye ni mtaka urais tu lakini anaweza kuwa na ajenda yake ile ile iliyobebwa na CUF Zanzibar yaani kuitaka Zanzibar huru. Alitulizwa baada ya kupewa cheo lakini baada ya vuguvugu la katiba na shinikizo la kichama amejikuta akianza chokochoko upya.

Pia tusisahau CUF inaungwa mkono na makundi kama yale ya uamsho kiasi cha kumfanya mgombea urais wa UKAWA kutamka hadharani kuwa atawaachia huru watuhumiwa wa ugaidi.

3 - CHADEMA Asilia na Maslahi:
Kuna kundi la wanachadema walio serious na kutaka mabadiliko ya kweli.kundi hili limekatishwa tamaa na mambo makubwa mawili yaliyotokea yaani kumpokea lowassa bila maelezo ya kueleweka na kumpa kijiti cha kugombea urais,pili kukatwa kwa Dr Slaa na kutothaminiwa kwa mchango wake ndani ya Chadema.

Chadema maslahi ni kina Mbowe na washkaji kibao kutoka pande za Arusha na Moshi. Hawa wako kimaslahi zaidi, Issue kwao ni chama kinaingizaje fedha au mikutano inaingizaje fedha au nguo na adverts za chama zinaingizaje fedha. Hawa wanaendesha Chadema kama kamati ya harusi za kichaga.

4 - Team Lowassa, Ulipo tupo na 4UMovement:
Hili ni genge ndani ya genge! Katika kundi hili kuna watoto wa kishua wanaosubiri kupiga dili kama za watoto wa vigogo.

Katika kundi hili kuna waliokosa ajira na fursa na hivyo kujishikiza kwa lowassa ili ikitokea kapata na wao watoke(hawajui uhuni wa mwanasiasa)

Katika kundi hili kuna watoto ambao wako tu kwenye age yao ya 'fantancy' na kuburudika na maisha.

5 - WanaCCM viongozi waliomfuata Lowassa:
Hapa kuna mchanganyiko wa waliokatwa kwa kuwa ni makapi haswa. Pia wako walioshtukia dalili za kukosa wakigombea kupitia CCM(Lembeli).

Pia wapo wanaojaribu kuibuka upya kwa mgongo wa Lowassa. Humu pia kuna mashushu kutoka CCM.

6 - NCCR na Mbatia na NLD:
Hili ni kundi lisilojielewa linahitaji nini. Mbatia anaweza kuwa ni mpiga dili flani hivi na pia baada ya kuonja ubunge wa kuteuliwa anatamani angepata ubunge ili aweke mambo sawa.

7 - Wanaharakati na waandishi:
Hawa wako katika kutegemea nafasi za kuteuliwa kama ilivyozoeleka huku wakisahau kuna vijana wengi na wenye weledi. Wengi wao wameumizwa na tendo la CCM kukata na kuvunja makundi na option waliyobakiwa nayo ni kujipendekeza UKAWA.

8 - Wafanyabiashara:
Hawana uhakika kabisa wa EL kushinda nje ya CCM na wamebaki kuuma na kupuliza.
Ingawa kuna wachache bado wanagamble kuendelea kuamini katika EL kuchukua kijiti.

9 - Wachungaji/Maaskofu:
Ni wachache na wanajaribu kutumia karata ya zamu ya mlutheri lakini kimsingi wanataka kutetea matumbo yao tu.


Ukiwa na genge la namna hii na likiwa halina uongozi au miongozo inayoeleweka utakuwa unaongelea nchi iliyoanguka. Ni lazima genge hilo lipate Kiongozi na Muongozo kwanza ndio ufikirie kuwapa nchi.
Sheria ya mitandao inakuhusu dogo
 
FaizaFoxy Jihad John kauliwa na rocket za Marekani muda mfupi uliopita. Kama utaenda Syria safari njema.
 
Last edited by a moderator:
Acheni kutuzingua porojo zenu andika vitu vyenye tija.Sio unaposti utumbo we unafikiri ukawa wasingekua na busara hii nchi ingekalika.We tulia kula ugali wako ----- we Lowasa Lowasa kuna mwenye hekma kama Lowasa
 
Quiet strange with ur words
These are justification of what discuss now
Every person in tanzania under world are multicasting something weird

Election election election campaign at last to face families
Ukawa supporters and fans be amuted faintest
 
Acheni kutuzingua porojo zenu andika vitu vyenye tija.Sio unaposti utumbo we unafikiri ukawa wasingekua na busara hii nchi ingekalika.We tulia kula ugali wako ----- we Lowasa Lowasa kuna mwenye hekma kama Lowasa

Acha maneno ya upenzi usio na tija ndugu yangu,ungekua kanda ya ziwa na ukachunguza vzr kwa nini Magufuli kashinda usingelaumu ccm,ungeenda kutoa ushauli cdm waje na kasi mpya ya umoja wa kimakabila na siyo uongozi ulojaa watu wote wenye vinasaba vya ukanda m1.kisha wape ushauli wa kuwapoza na wengine walioumia kwa sababu ya Dr Slaa..hawakupata elimu ya kutosha kwa nini kafukuzwa mtu walomuamini na kwa nini wamemleta mtu walosema hafai,hili halihitaji degree kujua,huku kanda ya ziwa tulipiga kura na watu wengi tu wakilipa kisasi cha Dr Slaa kwa kumpa kura Magufuli na wengine kwa kuwalalamikieni na jambo la ukanda.mahala pengine siyo lazima utukane au utoe kauli mbovu,ni vzr kufanya uchunguzi.
 
Ndugu yangu waheshimu sana ukawa,acha kabisa ushabiki usio na maslahi kwa taifa,ukawa wametufanya tuelewe wizi mwingi unafanywa na viongozi,angalia aliyosema magufuri mengi niyale waliyokuwa wakiyapigia kelele ukawa
 
Ndugu yangu waheshimu sana ukawa,acha kabisa ushabiki usio na maslahi kwa taifa,ukawa wametufanya tuelewe wizi mwingi unafanywa na viongozi,angalia aliyosema magufuri mengi niyale waliyokuwa wakiyapigia kelele ukawa

Siyo waliyokua wakiyapigia kelele ukawa,kweni mambo yanayoendelea yeye alikua hayaoni ameyasikilia kwa ukawa?kuweni wapole Magu afanye kazi,keshashinda na yeye ndo rais,kaeni kimya na mpige kazi pia.ni kweli upinzani unaiweka serikali mguu sawa ndiyo lakini siyo kitu cha sifa ni kufanya kazi,haupo muda wa kulaumu au kujisifia sifia ni kazi tu..wanayosema ukawa hayo ndo tunataka waseme japo upinzani bado haujafit kuiweza nchi kuongoza
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom