Ukawa kwenda IKULU-Thubutu-Ukumbusho!!

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Katika siku za hivi karibuni tumeaminishwa kwamba CCM itaondoka madarakani Oktoba 25 mwaka huu. Hata kama nitaonekana kuwa mmojawapo wa wanaopinga na wasioamini katika kile kinachoitwa 'UKOMBOZI WA PILI' lakini mtu mwenye akili anajua kwamba ndoto hizo niza ALINACHA kwa sababu:

(a) UCHAGUZI WA SEIKALI ZA MITAA 2014

Ukweli ni takwimu na kwa msomi yeyote anakubaliana na hilo. CCM ilishinda 67% kwenye Mitaa, 80% kwenye vijiji na 78% kwenye Vitongoji wakati CHADEMA na CUF kwa pamoja walipata 33% wenye Mitaa, 20% kwenye vijiji na 20% kwenye Vitongoji. Huu ndio UDHAIFU wa kwanza wa UKAWA ambao ni dhahiri nguvu yao iko Mijini tu.

(b) KOSA LA DAKIKA ZA MWISHO

Kitendo cha Dr Slaa aliyepata 28% mwaka 2010 kama niko sahihi kujiweka kando na CHADEMA ni pigo kubwa kwa UKAWA. Vivyo hivyo kwa Profesa Lipumba mwenye 11% mwaka 2010. Wenye imani na watu hao hawezi kuwapa kura UKAWA.

(c) WAFUASI WA UKAWA BADALA YA WAPIGA KURA
Vijana wengi wanaozungumzia kuiondoa CCM madarakani ni Wafuasi tu ambao kwa sehemu kubwa hawatakwenda Vituoni kupiga kura. Hii ni tofauti na CCM wenye Mkakati wa mtu kwa mtu na nyumba wa nyumba.

(d) TAASISI VS MTU BINAFSI

Mwaka 1995 NCCR MAGEUZI walimtegemea sana Lyatonga MREMA kuleta ushindi badala ya miundombinu ya Chama ambayo ilikuwa DHAIFU kama UKAWA mwaka huu!

IKULU HAPO UNAINGIAJE?

ACHENI KUJIPA MATUMAINI AMBAYO HAYAPO.
MWISHO MTASEMA MATOKEO YAMECHAKACHULIWA KUMBE WAPI!!!!!
 
CCM imepigwa Dar es salaam. Huo ndo uhalisia na ndo maumivu ambayo yatadumu kwa muda mrefu ndani ya nafsi za wana CCM. Hizo nyingine ni MBWEMBWE tu.
 
CCM imepigwa Dar es salaam. Huo ndo uhalisia na ndo maumivu ambayo yatadumu kwa muda mrefu ndani ya nafsi za wana CCM. Hizo nyingine ni MBWEMBWE tu.
mwisho wa siku serikali ni ya ccm na hao Madiwani wa UKAWA hawana sera za kutekeleza zaidi ya zile za Chama Tawala!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom