Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
WanaJF,
Ikumbukwe kumekuwa na tetesi za sintofahamu na mstakabali wa UKAWA katika siku za hivi karibuni. Taarifa zilizozagaa mitaani wiki mbili zilizopita, ilikuwa juu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuwatelekeza wabunge wa upande wa CUF katika ziara zao za mikoani.
Ziara hizo zilizopewa jina la vuguvugu la kudai Demokrasia, hazikuzingatia makubaliano ya UKAWA. Ijulikane kuwa kwa sasa UKAWA ndo inabeba sura ya upinzani bungeni chini ya Mh. Mbowe. Lakini, baada ya Mbowe kushawishi UKAWA kususia bunge, walipanga ziara za kichama kwenda mikoani na si UKAWA tena.
Wabunge wa CUF walikuja juu ya hili. Wakauliza maana ya Mbowe kusimama na chama chake na si UKAWA.
Taarifa hizi zimefanya CUF wajipange jinsi ya kukabiliana na nguvu ya Mbowe kuimeza na kuitumia CUF. Wiki iliyopita, baadhi ya wabunge wa CUF wamesikika wakisema wanatafuta jinsi ya kuokoa chama chao. Kwa mjibu wa vikao vya siri vilivyokuwa vinaendelea hapa mjini Dodoma na Dar es Salaam, mipango ya CUF kujiondoa UKAWA imejulikana. Baadhi ya Wabunge wa CUF na wajumbe wamesikika wakitoa maoni mbalimbali.
Moja ya makubaliano ya CUF kwasasa ni kumrudisha Prof. Lipumba kushika nafasi yake kama Mwenyekiti wa CUF taifa. Hatua hii ni kupunguza shinikizo la CHADEMA na ushawishi wake ndani ya CUF. Pia, imeonekana wamekosa mshauri wa ndani atakayesimamia maslahi yao ndani ya UKAWA.
Ikumbukwe kuwa Prof. Lipumba aliondoka UKAWA kwasababu ya Mbowe kumleta Lowassa kugombea urais kwa mwavuli wa UKAWA.
Prof. Lipumba amesikika akesema mpaka sasa, hakuna mwenye uwezo wa kugombea Urais ndani ya UKAWA zaidi yake. Ameeleza wasfu wake na uzoefu wa kiuongozi kwa miaka zaidi ya 20. Hii ni kulingana na maelezo yake leo alasiri katika Luninga ya AZAM katika kipindi cha Alasiri Lounge.
Hivyo, kuwepo kwa Prof. Lipumba kama mwamuzi wa mwisho ndani ya chama, kutazidi kudhofisha UKAWA na kupunguza muonekano wa Lowassa ndani ya UKAWA. Lowassa ambaye ametangaza kugombea urais kwa tiketi ya UKAWA 2020 atakuwa amepata pigo kubwa kuingia kwa Lipumba.Inajulikana kuwa Lowassa kwa sasa hawezi kusimama kama mgombea tena kupitia UKAWA kwa vile walimwandama katika kashfa zake za za muda mrefu za ufisadi.
Pia imejulikana kuwa, mbinu zilizokuwa zinatumiwa na Mbowe kuwatumia wabunge wa UKAWA kukuza CHADEMA zitapata upinzani mkubwa. Hii inatokana na Prof. Lipumba anamtuhumu Mbowe kumleta Lowassa ndani ya UKAWA na kuanchana na tuhuma walizotuhumu kwa miaka mingi.
Hii ni njia moja tu ya kudhofisha UKAWA. Na inaweza kuiua ndani ya muda mfupi.
Hebu tusubiri.
Updates