UKAWA inaweza kuleta mabadiliko?

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,919
2,000
Nimefuatilia kwa umakini kampeni za UKAWA, ninatambua yafuatayo:

1) UKAWA siyo chama cha siasa na hivyo sera na ilani ya uchaguzi inatumika ile ya CHADEMA.

2) Kwa sababu kuu hiyo, yafuatayo yanajitokeza:

i) Vyama vya CUF, NCCR na NLD, hawajapewa au hawa nafasi ya kutangaza sera na ilani zao
za uchaguzi.
ii) Kiongozi mkuu wa CHADEMA anahusisha mabadiliko na mgombea wao wa Urais. Hii siyo
maana halisi ya mabadiliko Watanzania wanahitaji, labda mabadiliko ya chama kwa kuteua
watu nje ya chama kugombea nafasi za kuingia Ikulu.
iii) Kwa kauli ya Sumaye, ambaye sasa ni mpiga debe mkuu wa mgombea wa Urais na mshauri
mkuu wa UKAWA) UKAWA hawana watu wenye uwezo wa kuongoza nchi, wakishinda
uchaguzi. Hivyo yeye anajiunga nao kuongeza nguvu.
iv) Matatizo ya nchi hii hajaletwa na sera za CCM (ni kama mparaganyo unaoendelea ndani ya
UKAWA, si wa sera za vyama), ila mapungufu ya viongozi ambao wananchi (wewe na mimi)
tuliwaweka madarakani.

Kwa hayo machache, na mengi yamejadiliwa humu jamvini, mabadiliko ya kweli yataletwa na wananchi wenyewe (mimi na wewe) chini ya usimamizi imara wa viongozi wenye hulka hiyo. Kati ya wagombea 8 wa Urais, Wabunge, na Madiwani, ni nani mwenye sifa za kuongoza. Sifa kuu ya usimamizi mzuri wa kazi, uadilifu na uwajibikaji.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195

Tulia, tafakari upya.

Mpaka hapa naona mabadiliko ya msingi. Moja la msingi (linalonisikitisha na kunifurahisha at the same time), ni kufikia hatua ya kumbadilisha mpaka mgombea wa CCM, kiasi cha kuacha kunadi sera dira na mtazamo wa CCM mpka sasa ananadi sera za Wana UKAWA! Imekuwa worse mpaka tumefikia kwa M4C! hayo nimabadiliko tosha kwa sasa. Labda nikutafsirie maana ya maneno hayo hapo juu. Maana yake ni kuwa CCM imeshakubali na kuona kuwa sera na ilani yake:

1.Haikubaliki
2.Haitekelezeki
3.Wananchi hawako interested kuvisikia tena!
Kwa hiyo wamebadilika kwa kubeba vinavyotakiwa na kukubalika na wananchi.

Kuhusu sera na ilani, kimsingi kama umefuatilia, wapinzani wote wanataka mambo yanayofanana. Wanatofautiana mkazo wa chama gani uko wapi. Ila wote wako common katika imani ya kwamba hayo yote wanayotaka ni MABADILIKO AMBAYO HAYATAKUWA KAMA CCM HAITATOLEWA MADARAKANI! Kwa hiyo kwa ninavyoona wako kwenye right lane so far.

Kuhusu kuwa au kutokuwa na watu wa kuongoza, hiyo ni hoja hafifu. Nchi hii aliwahi kuiongoza mwananchi asiye na uzoefu kabisa, akiwa kijana kabisa, kutoka kufundisha sekondari, bila hata kuwa Headmaster mpaka kuongoza nchi, tena kutoka kwa mkoloni huku akiwa hana watu wazoefu wa kumsaidia kazi! Miaka hiyo hatukuwa na viongozi wala watendaji. Tuliajiri form fours na six'! Na kwa mtazamo wangu, alifanya kazi nzuri kabisa kulinganisha na waliomfuatia, wakiwa na elimu bora kuliko yeye, wakiwa na bahati ya kufundishwa uongozi na nafasi ya kuamua na kujipanga! Leo tuna hazina kubwa ya viongozi na wataalamu, tuache upuuzi wa kudanganyana. Labda kama tuna akili mgando za kufikiri nchi hii ni ya chama! Napenda tuanze kuamini kuwa katika wananchi milioni 45 kuna hazina kubwa ya viongozi na watendaji, tena kuliko tulionao!

Mwisho siyo sahihi kuwa matatizo ya nchi hii hayakuletwa na chama au sera. Ni chama kilichokuwa na ilani ambayo serikali yake iliitengenezea sera ambazo watumishi wa serikali hiyo ambao pia ni wanachama wa chama hicho waliamua kuzipuuza na chama hicho kikawaacha hivyo kwa sababu ndivyo walivyoona vema! vinginevyo chama makini ni zaidi ya viongozi wachache. Kama chama kingekuwa sawa kisingevumilia wanachama wake ndani ya serikali kupuuza utekelezaji wa sera ambazo ni zao la ilani ya chama hicho. TATIZO NI CHAMA. TATIZO NI MFUMO WA CHAMA HICHO na TATIZO NI TABIA NA DESTURI ZA CHAMA HICHO! Chama ni watu. PAmoja nao, viongozi na watumishi wake. Swala la chama kuharibika siyo la viongozi tu, nila wote, na wanachama pia!

Nilikwambia tulia tafakari, namalizia kwa kuwambia chukua hatua!
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Hii mada ilishawekwa hapa jamvini(every word of the thread) kitambo.

Ukawa ni ikawa hivyo hawana Uwezo wowote

Mchango wenu ni nini kuhusu mada hiyo? Tunapenda kusikia hoja zenu wakuuu. Mpaka hapa naona kama mnalalamika tu! Kuna mtu amedhulumiwa kwa kuwekwa mada hii tena na tena? (kama imewekwa). UKAWA ikawa....hawawezi...weka hoja , toa sababu. ipe maana kauli yako!
 
kasinge

JF-Expert Member
May 22, 2011
1,258
1,500
Nimefuatilia kwa umakini kampeni za UKAWA, ninatambua yafuatayo:

1) UKAWA siyo chama cha siasa na hivyo sera na ilani ya uchaguzi inatumika ile ya CHADEMA.

2) Kwa sababu kuu hiyo, yafuatayo yanajitokeza:

i) Vyama vya CUF, NCCR na NLD, hawajapewa au hawa nafasi ya kutangaza sera na ilani zao
za uchaguzi.
ii) Kiongozi mkuu wa CHADEMA anahusisha mabadiliko na mgombea wao wa Urais. Hii siyo
maana halisi ya mabadiliko Watanzania wanahitaji, labda mabadiliko ya chama kwa kuteua
watu nje ya chama kugombea nafasi za kuingia Ikulu.
iii) Kwa kauli ya Sumaye, ambaye sasa ni mpiga debe mkuu wa mgombea wa Urais na mshauri
mkuu wa UKAWA) UKAWA hawana watu wenye uwezo wa kuongoza nchi, wakishinda
uchaguzi. Hivyo yeye anajiunga nao kuongeza nguvu.
iv) Matatizo ya nchi hii hajaletwa na sera za CCM (ni kama mparaganyo unaoendelea ndani ya
UKAWA, si wa sera za vyama), ila mapungufu ya viongozi ambao wananchi (wewe na mimi)
tuliwaweka madarakani.

Kwa hayo machache, na mengi yamejadiliwa humu jamvini, mabadiliko ya kweli yataletwa na wananchi wenyewe (mimi na wewe) chini ya usimamizi imara wa viongozi wenye hulka hiyo. Kati ya wagombea 8 wa Urais, Wabunge, na Madiwani, ni nani mwenye sifa za kuongoza. Sifa kuu ya usimamizi mzuri wa kazi, uadilifu na uwajibikaji.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Mapovu yote ya nini? Mpaka muige sera zao, Logo zao, muwazushie, kama havitekelezeki watu wataamua Oct 25.
Tafuta mengine ya kuiga, UKAWA ndo habari ya watanzania.
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,601
2,000
Mchango wenu ni nini kuhusu mada hiyo? Tunapenda kusikia hoja zenu wakuuu. Mpaka hapa naona kama mnalalamika tu! Kuna mtu amedhulumiwa kwa kuwekwa mada hii tena na tena? (kama imewekwa). UKAWA ikawa....hawawezi...weka hoja , toa sababu. ipe maana kauli yako!

Ndiyo maana Invisible anasisitiza kutumia 'Search button' kabla ya kupost kitu.

Kama unahitaji mchango wangu kuhusu hilo tafuta hiyo topic/thread utaikuta huko.
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Ndiyo maana Invisible anasisitiza kutumia 'Search button' kabla ya kupost kitu.

Kama unahitaji mchango wangu kuhusu hilo tafuta hiyo topic/thread utaikuta huko.

Again, inakupunguzia kitu ikiwekwa tena? Inakupa shida ukijiridhisha tu kuwa ulishachangia mwaka juzi, leo ukapita tu bila kusema lolote? Au unahisi wote waliiona siku hizo? Au je ni wote waliochangia leo walishachangia kabla?

Kwamba wewe uliingia hotelini ukapewa wali ukala ukashiba, haitoshi kufanya wengine wakiingia wasipewe wali. Wala haimaanishi hoteli isipike wali tena! Kulazimisha hilo itakuwa kumpora mwenye hoteli haki yake ya kupika anachoona kinamletea faida na wakati huohuo unawakosesha wengine haki ya kula wali hasa ambao hawakula juzi na ambao kwao it's ok kurudia kula wali na leo tena!! Kwamba wewe unaona ni vema mtu akiingia hotelini aulize kama kulipikwa wali tena juzi kabla haagiza, hiyo amua wewe.

Nasisitiza, nivema ukiona mada ukachangia hoja kama una la kuchangia. Au ukapita tu kama uliridhika na mchango wako wa majuzi na mwaka jana! Haitakupunguzia kitu na haina haja ya kulalamika.
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,919
2,000
Hoja katika mada ya msingi ni "Je, UKAWA wanao uwezo wa kupewa madara ya nchi hii, kwa sasa?"
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom