UKAWA imepotelea wapi? Siku hizi ni nadra sana kusikia neno UKAWA

Mkuu,
Usicheze na Dr. JK ,,, Alisema hawatafika popote.

Tatizo, upinzani wanadhania kuwa siasa ni kama kukaanga na kula popcorns ....
 
Wana bodi!
Bila kurefusha maneno, naenda kwenye mada straight.

Tulianza kuzoea kila kunapokuwa na suala la uchaguzi hapa nchini katika ngazi za kitaifa, jimbo na hata ngazi ya udiwani.
Basi vyama vya upinzani hususan, chadema, nccr mageuzi na cuf, kwa pamoja na mwamvuli wa UKAWA basi wangetoa tamko la pamoja katika kuelezea jinsi ya kupata wagombea au kuachiana majimbo husika.

Hii ilikuwa ni pamoja na kuelezea mikakati yao katika ushirika huo wa ukawa, katika kukabiliana na chama tawala CCM.
Pia tulizowea kuona press conference nyingi WAKAWA wakiwa pamoja na kutoa matamko ya pamoja. Tena yenye msisitizo mkubwa kutokana na jambo husika.

Hii kwa kiwango Fulani ilikuwa imeanza kuleta mabadiliko na hamasa kubwa katika nyanja za siasa hapa nchini, ikiashiria kuimarika kwa upinzani nchini na hasa ikiashiria kutoweka kwa tamaa binafsi za uongozi ndani ya nafsi za viongozi wa vyama vya upinzani nchini.

Lakini hivi karibuni hali hiyo imetoweka ghafla,tena kwa kasi ya ajabu na sasa hatusikii tena neno UKAWA na imebaki chadema ndio inasikika peke yake katika kutoa matamko ya maamuzi yao mbalimbali katika matukio ya siasa za nchi hii.
JE? Ndio kwamba ukawa bye bye!
Kulikoni UKAWA ??
Kuna "Kabila" mmoja kasema "wanyamaze kimya mpaka utawala wake upite. Amesema, katika kipindi chake cha utawala, hii nchi haitaendeshwa kidemokrasia(ingawa hajasema itaendeshwaje)"!
 
Mkuu,
Usicheze na Dr. JK ,,, Alisema hawatafika popote.

Tatizo, upinzani wanadhania kuwa siasa ni kama kukaanga na kula popcorns ....
Maneno ya ukweli toka twitter-ni.

20180121_223058.png


20180121_223041.png
 
Back
Top Bottom