UKAWA ifumuliwe iundwe upya na malengo mapya.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,467
2,000
Madhumuni hasa ya UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) hayakuwa kushinda uchaguzi wa 2015 bali kushinikiza maoni ya wananchi kwenye rasimu ya Warioba kuheshimiwa. Kwahiyo Msingi mkuu wa UKAWA haukuwa kushinda uchaguzi bali katiba.

Kwa vile ushirikiano ule ulikuja 'by chance' bila wao kutegemea na kujipanga, ni muda mwafaka sasa kwa vyama vinavyounda UKAWA na vyama vingine vitakavyojiunga kuja na a strong 'Alliance' itakayokuwa na lengo la kushinda uchaguzi na kuunda serikali. Umoja huu uje na 'Memorandum Of Understanding' (MOU) ambao kila chama kitabidi kuuheshimu.

Lengo kuu liwe kushinda na kushika dola. Inawezekana, mbona Kenya, Ghana, Gambia wameweza kwani wao wana nini.

Mchakato uanze mapema mjuane tabia ili mamluki wajulikane mapema kuliko kusubiri dakika za mwisho mkajikuta mnazoa na visivyozoleka. UKAWA mnatakiwa kutambua kuwa uchaguzi sio lelemama hasa unapotaka kumtoa mtu aliyepo madarakani kwa muda mrefu.

Umoja uwe na strategies za ushindi, kila chama kipewe malengo yake mahususi, kama ni kwenye stronghold yake mfano at least kishinde 50% kwenye serikali za mitaa.

Siyo vibaya hata jina la UKAWA likabadilishwa, lakini vilevile siyo mbaya likaendelea kwa vile limezoeleka.

Naomba kuwasilisha.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,032
2,000
Kwa sasa imebaki chadema tu,nayo wafuasi wameanza kulalamika chini kwa chini mzee anawaletea usiku
 

Migomba

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
946
1,000
Uko sahihi mno Kaka hata kushindwa uchaguzi wa 2015 ilichangiwa na kutokuwa na mipango ya mapema. Hadi dakika za mwisho kwa mfano bado hawakuwa na uhakika nani awe presidential candidate. Akatokea Edo basi wakaona tuweke huyo huyo... Wakijipanga mapema wanashika dola
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,467
2,000
Uko sahihi mno Kaka hata kushindwa uchaguzi wa 2015 ilichangiwa na kutokuwa na mipango ya mapema. Hadi dakika za mwisho kwa mfano bado hawakuwa na uhakika nani awe presidential candidate. Akatokea Edo basi wakaona tuweke huyo huyo... Wakijipanga mapema wanashika dola
Unaona, kama mgombea urais mnayetegemea aongoze jahazi hadi wiki ya mwisho hajulikani atatokea chama gani na mbaya zaidi akatoka upande wa wapinzani wenu, ilikuwa risk sana.
 

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Kama mafisadi Sumaye na Lowasa wana majina ya shule, Nini cha ajabu kwa shujaa Hapi kupewa jina la shule??


Kitendo cha kukomboa shamba la fisadi Sumaye na kuwagawia wanyonge ni cha kupongezwa sana.
 

Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Hapana jamani mbona hata mwaka jana kila kitu kilikwenda vizuri ila shida ikawa yule berbou? Wataweza tu as long as mchumi ouchwerer hawamshirikishi
 

stigajemwa

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
449
500
Uko sahihi lakini hiyo kitu inaitwa ukawa ina maadui wengi na inasababisha wenye mamlaka kutolala vizuri hivyo sijui kama hao ukawa wataachwa wajipange
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,467
2,000
Kama mafisadi Sumaye na Lowasa wana majina ya shule, Nini cha ajabu kwa shujaa Hapi kupewa jina la shule??


Kitendo cha kukomboa shamba la fisadi Sumaye na kuwagawia wanyonge ni cha kupongezwa sana.
Out of context, hata hivyo Tanzania haina mafisadi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom