UKAWA: Huu ni udhalilishaji na insurbodination kwa waheshimiwa hawa

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Nimeshtushwa na taarifa eti UPINZANI wamegoma kuchagua wanyeviti wa kamati ya LAAC na PAC eti kwa sababu waabunge walioteuliwa katika hizo kamati hawawezi hizo nafasi, Really ???

Tuanze hapa. Wabunge wa UKAWA katika LAAC ni
  1. Dr. Suleiman Ally Yusuph - cuf
  2. Rose Kamili -CDM
  3. Conchesta Rwamkaza -cdm
  4. Grace Kiwelu -CDM
  5. Joseph Mkundi -CDM
  6. Vedasto Ngombale -Cuf
Na PAC ni
  1. Nagenjwa Kabuyoka -CDM
  2. Musa Mbarouk -Cuf
  3. Raisa Mussa- Cuf
  4. Yoseph komba -CDM
  5. Tunza Malapo- CDM
  6. Ali Khamis-Cuf
naomba mnijibu yafuatayo.
  • je katika hao wabunge wote ina maana hakuna hata mmmoja anayefaa kwa nafasi hizo??
  • Na kama hawafai, je mnataka kutuaminisha kuwa mmechagua wagombea vilaza, wajinga na msiowaamini hata kwa kuwapa uenyekiti wa kamati??
  • Je mngeshinda urais, mawaziri na manaibu ambao jumla yao ni zaidi ya 40 mngewatoa wapi, kama hamuwaamini wabunge wenu mliowapitisha wenyewe ili wagombee kuwa wenyeviti tu wa kamati???
  • Je kama hamuwataki hawa, twambieni leo mnamtaka nani?? na huyo mnaemtaka alisomea wapi degree ya kuwa mwenyekiti wa PAC/LAAC kiasi cha kufanya wenzie wote waonekane hawafai???
  • Je ndo mnataka kutwambia kuwa UKAWA ni ka kikundi ka baadhi ya wabunge tu na hivyo hakuna usawa kati ya mbunge na mbunge,???
  • hivi kumbe ukawa kuna watu ambao nafasi Fulani zimekuwa reserved kwa ajili yao, na wasipopata nafasi hizo by default basi wanalazimisha?? i.e. uenyekiti PAC/LAAC
  • Ukawa tumekuwa tunapinga watu kuzeekea ofisini na kusisitiza damu mpya, je falsafa hii imeishia wapi, kiasi cha kulazimisha eti lazima Fulani ndo awe mwenyekiti PAC/LAAC kisa tu eti kazoea huko???
  • Je msipowawezesha hao ambao hamuwataki, huo uzoefu watautoa wapi?
Kwa kweli huu ni udhalilishaji, Insubordination , dharau na matusi kwa waheshimiwa wabunge niliowataja hapo juu, na KAMA WANANISKIA NI MUDA MZURI WA WAO KUJIHOJI KAMA WANAFAA KUENDELEA KUWA UKAWA ikiwa hawaaminiki kiasi hiki, hata katika kupewa majukumu ya uenyekiti.
 
Wanawajua wabunge wao, kama majukumu ni mazito zaidi wana haki ya kulalamika na kugoma.
Nani kawateua hap wabunge? Ni wana ukawa wenyewe au? Au sijaelewa kitu.
 
Ishu sio hao ...ishu ni composition nzima ya kamati..kutokuwa fair
 
Hahahahahahhaaaah...mkuu ww subiri jamaa wakija hapa wakumwagie matusi tu...ila hawatakupa majibu yenye kuridhisha kwa hayo maswali yote uliyouliza
 
  • Thanks
Reactions: nao
Nimeshtushwa na taarifa eti UPINZANI wamegoma kuchagua wanyeviti wa kamati ya LAAC na PAC eti kwa sababu waabunge walioteuliwa katika hizo kamati hawawezi hizo nafasi, Really ???

Hakuna mbunge mwanaume mmasai wala mwanaume mchaga hata mmoja.Lowasa atawakilishwa na nani na Mbowe atawakilishwa na nani? Hao wote nadhani ndio maana wanaonekana hawafai.

Hivi mtu kachaguliwa na wananchi wakampa kura au chama kikamwamini kikampa ubunge viti maalumu mtu kweli unaweza simama kusema hawafai nafasi fulani? Hawajawatendea haki
 
Protocol lazima izingatiwe yaani elites wanakula kwanza na wacheza shoo baadae, sasa kamati hizi hazina elites a.k.a wenye bendi. Ni insurbordination Zaidi kuchagua kati ya hawa kuwa wenyeviti kwenye kamati hii na kuacha elites wajumbe kwenye kamati za maendeleo ya jamii. Haiwezekani Tundu Lissu kuwa mjumbe katika kamati ya maendeleo ya jamii na Yoseph ndio mwenyekiti PAC come on ndio wenzio wanapigania hii kitu isitokee, huwezi mweka Messi benchi aanze Mascherano striker.

Imenikumbusha Enzi zile tuko Tambaza, katika zawadi za waliofanya vizuri Mock kimkoa DSM Kiswahili, civics, English watu walikuwa wanazuiliwa wasipande kuchukua zawadi. Yaani Phyisics, Chemistry, Biology na Number ndio msingi wa taaluma. wakati ule ilikuwa mchizi mmoja alikuwa kipanga wetu anaitwa Phabby anaitwa kuchukua history wababe tulipiga kelele manake Shaban Robert, Almuntazir masista duu walitunyoosha katika Phyisics, chemistry, biology na Math O level ilikuwa.
 
Nimeshtushwa na taarifa eti UPINZANI wamegoma kuchagua wanyeviti wa kamati ya LAAC na PAC eti kwa sababu waabunge walioteuliwa katika hizo kamati hawawezi hizo nafasi, Really ???

Kwa kweli huu ni udhalilishaji, Insubordination , dharau na matusi kwa waheshimiwa wabunge niliowataja hapo juu, na KAMA WANANISKIA NI MUDA MZURI WA WAO KUJIHOJI KAMA WANAFAA KUENDELEA KUWA UKAWA ikiwa hawaaminiki kiasi hiki, hata katika kupewa majukumu ya uenyekiti.

Kwanza uchaguzi wa Wabunge Tz - haswa wale wa viti maalum hauna ushindani wa kutosha na hili ni tatizo kwa vyama vyote. Ndio maana tumekuwa na wah WabUnge wa ajabu ajabu amabao wengi tumewajua. Hili limepelekea Chama fulani kujaza watu amabao kazi yao ni kwenda kupiga debe tu.
Kwa upande wa upinzani ie UKAWA, viti hivi vimetumika zaidi kurudisha fadhila na kuwatia moyo wananchi kuwa upo uwiano mzuri wa uwakilishi wao Bungeni.
Pili Dhamira ya UKAWA sio mbaya lakini ukweli upo palepale kwamba kuna kutofautiana sana kati ya uwezo wa wawakilishi waliopo Bungeni.
Tatu, kwa ufahamu wa kawaida tu, (labda kama una malengo yako mwenyewe), ni wazi uongozi wa Bunge hauwezi kutoa nafasi kwa upinzani kuwa na nguvu kubwa katika Kamati nyeti kama hizo, ukirejea majeraha yaliowapata wa serikali iliyopita.
NNE, hakuna sababu ya kuuliza kwa hasira hivyo..... as if hili moja linaondoa makubwa mengine yenye tija yoote yanayofanywa na upinzani. Think again.
 
SONGOKA

Tupe full details na sio habari nusu nusu
Ni nani amewateu ama kuwapendekeza hao Waheshimiwa
Tuanzie hapo
 
Songoka hata kwenye familia yako inawajua watoto wako tabia zao na ukiwapa majukumu kila mtoto anauwezo tofauti.SIjaona kosa la UKAWA kusema kwamba hao waliowaweka majukumu hayo hawayawezi.Jamani wana sabbau za msingi sababu ndiyo waliowafanyia upbringing kwenye SIASA na MAJUKUMU yake.Wakikua watapewa majukumu hayo mazito.Kumbuka issue ni kuwa na uwezo ili kuifanyia haki TAIFA letu
 
Yani hata huyo DR hapo hajui kitu??? hii dharau sasa
 
Nimeshtushwa na taarifa eti UPINZANI wamegoma kuchagua wanyeviti wa kamati ya LAAC na PAC eti kwa sababu waabunge walioteuliwa katika hizo kamati hawawezi hizo nafasi, Really ???

Tuanze hapa. Wabunge wa UKAWA katika LAAC ni
  1. Dr. Suleiman Ally Yusuph - cuf
  2. Rose Kamili -CDM
  3. Conchesta Rwamkaza -cdm
  4. Grace Kiwelu -CDM
  5. Joseph Mkundi -CDM
  6. Vedasto Ngombale -Cuf
Na PAC ni
  1. Nagenjwa Kabuyoka -CDM
  2. Musa Mbarouk -Cuf
  3. Raisa Mussa- Cuf
  4. Yoseph komba -CDM
  5. Tunza Malapo- CDM
  6. Ali Khamis-Cuf
naomba mnijibu yafuatayo.
  • je katika hao wabunge wote ina maana hakuna hata mmmoja anayefaa kwa nafasi hizo??
  • Na kama hawafai, je mnataka kutuaminisha kuwa mmechagua wagombea vilaza, wajinga na msiowaamini hata kwa kuwapa uenyekiti wa kamati??
  • Je mngeshinda urais, mawaziri na manaibu ambao jumla yao ni zaidi ya 40 mngewatoa wapi, kama hamuwaamini wabunge wenu mliowapitisha wenyewe ili wagombee kuwa wenyeviti tu wa kamati???
  • Je kama hamuwataki hawa, twambieni leo mnamtaka nani?? na huyo mnaemtaka alisomea wapi degree ya kuwa mwenyekiti wa PAC/LAAC kiasi cha kufanya wenzie wote waonekane hawafai???
  • Je ndo mnataka kutwambia kuwa UKAWA ni ka kikundi ka baadhi ya wabunge tu na hivyo hakuna usawa kati ya mbunge na mbunge,???
  • hivi kumbe ukawa kuna watu ambao nafasi Fulani zimekuwa reserved kwa ajili yao, na wasipopata nafasi hizo by default basi wanalazimisha?? i.e. uenyekiti PAC/LAAC
  • Ukawa tumekuwa tunapinga watu kuzeekea ofisini na kusisitiza damu mpya, je falsafa hii imeishia wapi, kiasi cha kulazimisha eti lazima Fulani ndo awe mwenyekiti PAC/LAAC kisa tu eti kazoea huko???
  • Je msipowawezesha hao ambao hamuwataki, huo uzoefu watautoa wapi?
Kwa kweli huu ni udhalilishaji, Insubordination , dharau na matusi kwa waheshimiwa wabunge niliowataja hapo juu, na KAMA WANANISKIA NI MUDA MZURI WA WAO KUJIHOJI KAMA WANAFAA KUENDELEA KUWA UKAWA ikiwa hawaaminiki kiasi hiki, hata katika kupewa majukumu ya uenyekiti.
Ccm mwaka huu lazima muombe pooo,hakuna habari ya ndiyo ndiyo hapa
 
Songoka hata kwenye familia yako inawajua watoto wako tabia zao na ukiwapa majukumu kila mtoto anauwezo tofauti.SIjaona kosa la UKAWA kusema kwamba hao waliowaweka majukumu hayo hawayawezi.Jamani wana sabbau za msingi sababu ndiyo waliowafanyia upbringing kwenye SIASA na MAJUKUMU yake.Wakikua watapewa majukumu hayo mazito.Kumbuka issue ni kuwa na uwezo ili kuifanyia haki TAIFA letu
Ccm wanataka mteremko,lkn safari hii wamekutana na mlima kitonga
 
Hata hao wanaojitia wazoefu wakumbuke walipoingia mara ya kwanza walikuwa hawajui kitu walijua baada ya kupewa nafasi .Walijulia humo humo.Huo ni uonezi kudsharau watu wengine.Mtu mpe nafasi asindwe mwenyewe.UKAWA ni jipu la kutumbua pia.
Maccm mwaka huu lazima muisome namba
 
Back
Top Bottom