Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Mwaka Jana tuliona vituko sana. Watu walidai mabadiliko kwa kutuaminisha kwamba yatapatikana UKawa na kwamba tatizo la CCM ni mfumo. Ajabu Watu Hawa sijui walipofushwa na nini, wakakubali Mgombea aliyekatwa CCM wakiamini ataleta mabadiliko ya kweli Hali wakijua kwamba alijiandaa miaka 10 kuwa Rais kupitia CCM na kwamba hakuwa na mawazo mapya Bali alitafuta Kwao nafasi tu ya kutimiza ndoto zake.
Basi barabara zikadekiwa, mikono ikazungushwa, mbwembwe za Mita 200 zikaanza eti kulinda kura!! Ajabu sana hii. Wanaikataa CCM lakini makapi yake wanayakubali! Enyi Wagalatia! Ni nani aliwaroga?
Basi barabara zikadekiwa, mikono ikazungushwa, mbwembwe za Mita 200 zikaanza eti kulinda kura!! Ajabu sana hii. Wanaikataa CCM lakini makapi yake wanayakubali! Enyi Wagalatia! Ni nani aliwaroga?