UKAWA hatuna wa kumlilia

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,449
WanaJf habari zenu,

Naendelea kusisitiza kwamba mimi ni mwanaukawa japo wengi wanaamini kwamba mi ni CCM//lumumba, lakini ukweli utabaki kwamba mi ni mkawa,na nasisitiza kwamba mi ni mwanaukawa kwa sababu watu wa UKAWA baadhi wana tabia ya ajabu sana au siasa za hovyo sana, mtu akikosoa chama wao wanahisi ni mamluki au msaliti na ndio sababu tunaitwa nyumbu.

Nirejee kwenye mada sasa,ni hivi:viongozi wetu wote wa UKAWA ni mapopora kabisa,walijua kabisa kwamba katiba tuliyo nayo ya 1977ambayo imefanyiwa amendment mara 14 ni mbovu na kuna vipengere vinahitaji marekebisho ila waliuchuna kimya, mwisho wa siku tunaanza kumtafuta mchawi nani,hivi kama wangeweka vipengere vifuatavyo mnadhani hizi kelele zingekwepo?

Tume huru yauchaguzi, matokeo ya raisi kuhojiwa mahakamani,raisi ashinde kwa 50 najua wapo wataosema mbona viongozi walipiga kelele sana lakini je baada ya kupiga kelele ni nini kilifanyika?

Hawa viongozi wetu wa ukawa ni mapopora sana kwa sababu hata huko Zanzibar walishindwa kuweka tume huru ya uchaguzi japo wana katiba yao mpya ya juzi tu 2010.

Sasa ni vipi tutawaamini hawa viongozi wetu? Na pia kuthibisha ujuha na uzwazwa walio nao eti leo kingunge,Lowassa, Medeye, Lembeli,nao wanataka katiba mpya ma tunawaita majembe, hivi hao majamaa si ndii walikuwa kwenye bunge la katiba jaman? Na wameipitisha katiba pendekezwa? Sasa ni vipi wanataka katiba mpya au labda mpya ipi? Kosa la sisi wafuasi wa ukawa ni kwamba hatujui kupima hoja ila tuna siasa za kufuata mkumbo na upepo kama bendera, ndio maana tunaitwa nyumbu, yaani viongozi wetu hata wakikosea sisi hatutaki kuwahoji na kuwakosoa.

Kifupi hatuna wa kumlilia na tukiendelea hivi tutaendelea kuwa wasindikizaji tu kwenye chaguzi, mwisho wa siku tutachanganyikiwa na kuanza ujuha kama wa juzi wa kugombana na maiti na kupeleka kesi mahakamani na maiti,utadhani asipozikwa ndio hao wauaji watakamatwa(kamanda alphonse mawazo wa geita),japp kajiunga na CHADEMA 2012 ila anaitwa shujaa, kamanda, yaani two years tu ukiwa CHADEMA utaitwa kamanda,ila ukihama na kukosoa utaitwa msaliti, mamluki, huna hasara, n.k
 
''.......Viongozi wenu wakikosea hata hamhitaji kuwahoji wala kuwakosoa....''

ukihoji au kuwakosoa utaitwa msaliti....
 
ndio maana tulishituka chadema kuachana na mtu aliyekijenga chama na kumkumbatia mtu ambaye siku zote walikuwa wanamshambulia wakimwita fisadi hata kwenye uchaguzi huu walibaki kujibu hoja kwamba wao sio mafisadi badala ya kuwaeleza wananchi ni nini watafanya
 
Back
Top Bottom