UKAWA hatukutaka katiba mpya

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,334
21,429
Kama walivyotuaminisha kuwa wanapigania mabadiliko ya katiba mpya ndani ya bunge la katiba, lakini ghafla wakatuonyesha tabia zao halisi kuwa hawakuwa na dhamira ya kweli.

Povu liliwatoka sana lakini bila ya aibu mwisho wa siku tukampokea mtu aliekuwa anapinga katiba mpya kwa nguvu zake zote na chama na serikali yake, nasi tukamuona ndie mtu sahihi kumpa nafasi ya kugombea urais bila kujua kule aliitetea katiba mbovu kwa kujua atachaguliwa na chama chake ili ile katiba itambeba vyema ndivyo na huku chadema alitegemea hilo.

Hongera mzee Lipumba na Dr. Slaa kwa kuliona hilo na pia pongezi kwa wapinga katiba mpya waliomfuata Kingunge na Sumaye.

Tunatakiwa kujua kule alikotoka ndio kwenye rafiki zake wa kweli ambao hakukutana nao barabarani, hana wasiwasi anajua mali zake zitalindwa na mfumo alioutengeneza hapo kabla na katiba mbovu alioitetea.

CCM si mama yangu!
 
Ilikuwa kosa kubwa kumchukua Lowassa. Wanatamani wautue mzigo ila wanashindwa
 
Ilikuwa kosa kubwa kumchukua Lowassa. Wanatamani wautue mzigo ila wanashindwa
Wanashindwa kwa vile biashara imeshafanyika. Mkuu uliwahi kutapeliwa na wale wahuni pale Kariakoo ama Ubungo. Pale Kariakoo wanakuonesha kiatu kizuri. Mkifikia bei wanajifanya wanakuwekea kwenye mfuko. Ukienda mbele na kukagua tena mali uliyofungua unakuta sole za viatu chakavu. Basi hapo utahangaika sana wapi pa kutupa huo uchafu. Utajiuliza mara mbili mbili je uendelee kuubeba ama uutupe? Vivyo hivyo na pale Ubungo hasa kwenye biashara ya simu. Ndo hali wanakutana nayo CHADEMA kwa sasa
 
Haya yameshapita tangu ulipomalizika uchaguzi.....sasa tunajenga nchi na kusafisha uchafu ,uozo na bila kusahau kukamua majipu na mabusha yaliyosababishwa na uongozi mbovu wa chama twawala.........

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.....
 
Back
Top Bottom