• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

UKAWA chonde msisahau haya katika kampeni zenu kama ahadi kwa watanzania na dunia

K

KKESHOM

Member
Joined
Jul 12, 2015
Messages
24
Points
0
K

KKESHOM

Member
Joined Jul 12, 2015
24 0
1. Nimekua nikifuatilia mikutano ya kampeni za UKAWA na CCM, sijaona au kusikia mgombea hasa wa urais anayezungumzia kutumia lugha yetu ya Kiswahili ktk matukio/ mikutano ya kiserikali ndani na nje ya nchi.

Kimsingi mimi nasikitika sana ninapoona Rais wa Tanzania anapotumia lugha ya kigeni anapohutubia mikutano baadhi ya mikutano ya ndani na mingi au yote ya nje. Lakini sijaona Mfn. Rais wa China, au viongozi wa nchi nyingine wakitumia lugha zisizo zao kuhutubia wakiwa nje ya nchi zao isipokuwa Rais au viongozi waTanzania. Kwa hilo CCM ilichemsha.

Hivi ni lini viongozi wa Tanzania hasa RAIS wataheshimu na kutukuza lugha yetu ya kiswahili hasa wakiwa nje ya TZ?
Naombeni UKAWA chukueni suala hili kama fursa pekee. Waambieni watanzania kuwa mtaenzi Lugha yetu ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania. Kokote atakakoenda Rais wetu atatumia lugha ya kiswahili ili kukuza lugha na ni fahari ya utanzania wetu.

2. Jambo lingine naombeni UKAWA, msikike katika kuboresha maslahi ya watumishi wa umma pamoja na Majeshi yetu. Watumishi wa umma wanaelekea kutoa kura kwa UKAWA ila hawasikii sana maslahi yao kuongelewa vizuri. Hivyo kuhisi kama wakitoa kura UKAWA sijui nini kitawatokea. Naomba UKAWA na LOWASA msisahau kuzungumzia maslahi kwa MAJESHI yetu na watumishi wa umma. UKAWA na Lowassa mmekuwa na kigugumizi sana katika hilo. Sipendi kuamini kuwa mna nia mbaya. Naamini mnajisahau au muda unakuwa mchache kuzungumza mambo yote. Najua yapo ktk ilani lakini ni vema wananchi wakayasikia mikutanani kama wafanyavyo ccm. Huo ni ushauri tu. Ukifaa ufanyiwe kazi. usipofaa uachwe. Asante
 

Forum statistics

Threads 1,406,198
Members 532,237
Posts 34,508,287
Top