UKAWA, 2020 njooni na sera ya kuruhusu TBC na vyombo binafsi kurusha live vikao vya bunge

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,679
149,864
Hakuna kosa kubwa lililowaudhi wananchi wengi kama kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge.Hili jambo halijawauzi wanachama na wapenzi wa UKAWA tu, bali hata wanachama na wapenzi wa CCM na hata wale wasio na vyama.

Hivyo basi, nawashauri viongozi wa UKAWA mwaka 2020 swala la matangazo ya Bunge kuwa live liwe ni sera ya vyama yenu na liingizwe kwenye Ilani ya vyama.

NB: Msije kushangaa serikali hii ikalamba matapishi yake kwa kuruhusu tena shughuli za Bunge ziwe live baada ya kugundua wamefanya kosa. Hawatakosa cha kujitetea ili kupata justification ya kubadili uamuzi wao.
 
Sasa kama wananchi hawatawaona UKAWA mpaka kampeni za 2020 kweli watawachagua???Hili ni la kupiganiwa sasa hvi..likiachwa kuja kuwa mtaji wa kampeni itakuwa too late!!!
 
Sasa kama wananchi hawatawaona UKAWA mpaka kampeni za 2020 kweli watawachagua???Hili ni la kupiganiwa sasa hvi..likiachwa kuja kuwa mtaji wa kampeni itakuwa too late!!!
Hili jambo ni kama Escrow haliwezi kutoka vichwani mwa watanzania kirahisi hivyo bali watabaki na machungu mioyini mwao na Nape atakuwa na kibarua kigumu sana jimboni kwake mwaka 2020.
 
Sera hiyo itapigiwa kampeni mjini tu. Sehemu nyingi vijijini itakuwa watu hawaelewi kitu gani kinaongelewa!
 
Wajinga nchi hii wanapungua mwaka hadi mwaka na ndio maana hata kura za wagombea uraisi wa CCM zimekuwa zikishuka mwaka hadi mwaka na idadi ya wabunge wa upinzani nayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Ila wakifanikiwa kuzima Tv -Bunge miaka 5..amini hata mijini watu watasahau UKAWA na harakati zao.Na wajinga pia wataongezeka,bora hata Bunge la 10 walisikia kuhusu Escrow!!
 
Mwenyekiti wa Escrow ndiyo Mwenyekiti wa Bunge..Muhongo ana wizara,Tibaijuka ubunge kapeta..sijui escrow ilikuwa na matunda mpk hapo???Labda ya kuanguka kwa Kafulila!!!WaTz ni kichwa cha mwendawazimu asee

Mbona huwasemi viongozi wa UKAWA waliotorosha fedha kwenda nchi za nje...
 
Haina sababu ya kung'ang'ania Tbc kama wenye mamlaka wanagoma.Hapo swala ni kuja na mbinu mpya!Waingie mkataba na kituo cha television ambacho kama hakitaruhusiwa kuonesha live basi kirekodi ili watuoneshe baadaye kitu ambacho ni halisi! Nawasilisha.
 
Sasa kama wananchi hawatawaona UKAWA mpaka kampeni za 2020 kweli watawachagua???Hili ni la kupiganiwa sasa hvi..likiachwa kuja kuwa mtaji wa kampeni itakuwa too late!!!

Ni kweli 2020 ni mbali sana. wanatakiwa wapeleke hoja binafsi kuilazimisha TBC irushe majadaliano yote ya bunge.
 
Walichofanya hawa ccm ni ujuma dhidi ya ukawa wanajua wanawakomoa kwa wananchi wake lakn wajue wanajizika wenyewe mda ukifika wakiona cha moto machungu wataendelea kuwa nayo wananchi
 
Hili jambo ni kama Escrow haliwezi kutoka vichwani mwa watanzania kirahisi hivyo bali watabaki na machungu mioyini mwao na Nape atakuwa na kibarua kigumu sana jimboni kwake mwaka 2020.
Nasikitika tu hili halitakuwa kikwazo kwa elimu ya watanzania wengi, kama Muhongo, Chenge na Tiba wamerudi basi watanzania wote wafike chuo ndio itakuwa rahisi. Kama watanzania wakioichagua ccm wamegoma kuelewa sakata la escrow basi mimi nimewanyooshea mikono. Kama Kafulila walishindwa kumpigia kura nyingi sana ili hata zile chache walizoiba zisiwezekane hapo ndio utajua watanzania si watu wa kushikia dhamana
 
...ccm na maamuzi yao hakika wanata kinyaa.....yaani watu wasione bunge live alafu lionyeshwe recorded saa nne usiku!!...muda huo nani huko vijijini wanaangalia tv??...ama ccm wanataka kuwaambia watanzania kwamba huko vijijini watu hawastahili kuona tv??...yaani hili bunge ni kwa manufaa ya nani??....ccm wanadhihirisha tena unafiki wa ajabu...kwa kuwanyima wapiga kura wao haki ya kuangalia wabunge wao wanafanyaje kazi waliyowatuma....i mean cmon nani kijijini anaangaklia tv kwa umakini saa nne usiku???..kwanza saa mbili tu vijijini wengi wamelala...hawa ccm wana lengo gani??
 
Back
Top Bottom