Ukatili wa Serikali na Jeshi la Polisi Kinondoni

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kwa sasa kuna zaidi ya askari 500 wanapita na bomoa bomoa cha ajabu zaidi baada ya greda kuvunja nyumba askari wa jeshi la polisi wanachoma mabaki ya mali zilizobomolewa ndo nini hii jamani ?????
 
Na mkuu wa wilaya yupo hapo hapo anadai ni wavamizi

Wabongo bana! hadi raha! yaani hamna jambo jema kwenu! watu wamejenga holela kwa hela za kifisadi,serikali yetu sikivu inawaondoa ki sheria wanagoma! Jeshi la polisi linawajibika kuhakikisha sheria zinafuatwa mna complain! so mnatakaje?! yani wabishi kama****!
 
Wabongo kutokuwa na jema wewe unajisikia rahaa!
 
Wabongo bana! hadi raha! yaani hamna jambo jema kwenu! watu wamejenga holela kwa hela za kifisadi,serikali yetu sikivu inawaondoa ki sheria wanagoma! Jeshi la polisi linawajibika kuhakikisha sheria zinafuatwa mna complain! so mnatakaje?! yani wabishi kama****!

njoo na hoja vizuri acha kulalama kwani hizo nyumba serikali imeamka tu asubuhi na kukuta zimeota kama uyoga kwa usiku mmoja walikuwa wapi siku zote mpaka kuja leo na kufanya unyama maanake kwingine huwa naona wanapewa muda kuchukuwa chao imekuwaje leo wachome mabaki?

kumbuka kuna watu serikalini kazi zao kila siku ni kuongoza watu wapi wajenge wapi wafanye nini je wako wapi

Ni vizuri kusema ni ukatili wa serikali, lakini ni vigumu kuamini serikali imefanya uamuzi wa kutudhuru baada ya kudhulika hivyo na hiyo kazi yao.

1. Zimekua LRover 7 zimejaza FFU na kufyatua mabomu ya machozi. Haya mabomu yamewaathiri watu na hasa watoto

2. Mgambo wamebomoa milango ya nyumba yangu wamepekua vyumba na kuiba 42 inchi TV na hela.

3. Unatoa taarfa polisi unaambiwa wewe nawe mvamizi

Naomba kama mtu ana simu ya mbunge Mdee atuwekee hapa au kama mbunge mwenyewe anasoma hapa afuatilie hili kwa sababu limevka mstari mwekundu.
 
njoo na hoja
vizuri acha kulalama kwani hizo nyumba serikali imeamka tu asubuhi na
kukuta zimeota kama uyoga kwa usiku mmoja walikuwa wapi siku zote mpaka
kuja leo na kufanya unyama maanake kwingine huwa naona wanapewa muda
kuchukuwa chao imekuwaje leo wachome mabaki?

kumbuka kuna watu serikalini kazi zao kila siku ni kuongoza watu wapi
wajenge wapi wafanye nini je wako wapi

Mi nakwambia ki ukweli ukiwabana hao walojenga hapo,wengi utakuta vibali vyao vya magumashi! kama ni swala la serikali kuwaona wakijenga au kutowaona haijalishi,kama wangekuwa right mahakama isingeamuru waondolewe!
 
Mkuu nina wasiwasi na lengo lako. Mimi niko mbali na hilo eneo sihusiki na hayo unayoyasema ya uvamizi na ufisadi. Kwa sababu niko njiani kuelekea kwenye eneo hilo linalogombaniwa kwa nini mgambo wavunje mlango wa nyumba yangu na kuniibia. Halafu hao unaoita mafisadi ndio hao ho serikalini, mimi sipo serikalini.

Mgambo wameingia kwenye nyumba za watu (mbali na eneo husika) wamewapiga na kuondoka HAPA KUNA KITU SI SAHIHI NA SI CHA KAWAIDA KINACHOFANYWA NA SERIKALI KWA UKATILI.
 
Si ni mtu aweke picha basi tuzitumie wengine kufikisha hiki Kilio cha uonevu Level nyingine since

"Judiciary" wamehusika kwa kutoa hukumu.

"Executive" wako hapo on field RC or DC ndio mwakilishi wao.

Na wote hao hawawezi kujihukumu. Mihimili ilobaki

"Legislature" hawaturuhusiwa kujadili kwa kisingizio kuwa jambo liko mahakamani.

And The Fourth Estate "Media" yetu haina nguvu, wakiongea wanafungiwa, Refer MwanaHalisi.

Kilichobaki ni the Emerging Sixth Estate "Social Networks and Forums" kitusemee.

Mwenye kuweza kuleta picha, Tafadhali fanya hivyo
 
Mi nakwambia ki ukweli ukiwabana hao walojenga hapo,wengi utakuta vibali vyao vya magumashi! kama ni swala la serikali kuwaona wakijenga au kutowaona haijalishi,kama wangekuwa right mahakama isingeamuru waondolewe!

Mkuu hapa nadhani unachanganya mada,
Kimsingi ni kweli lengo mahsusi ni kuwaondoa wavamizi wa mashamba, ambao kwakweli naishukuru serikali kwa moyo wa dhati kwa kulifanyia kazi jambo hili!

Yaani ni kama walisha unda jeshi dogo na himaya yao, mtu alipokuwa akisogelea eneo lao anaulizwa maswali na wasipo rizika na majibu wanakupa mkong'oto haswa! Na usilogwe ukasogea na gari, na kama lina namba za serikali ama SU ndo kiama yako imekukuta! KWA KWELI KWA HILI NAIPONGEZA SANA SERIKALI KUKOMESHA UHUNI HUU,

Angalizo:
Kuna askari wasiokuwa waaminifu ambao wametumia mwanya huu kudhulumu mali za wananchi wasio kuwa na hatia. Na pia kumekuwa na tatizo la kubomoa hadi nyumba zisiziko husika. Nawasihi waongeze umakini kwa haya mambo mawili yasiharibu nia njema ya kukomesha uharamia huu.

hakina asikali mwaminifu kama si mwizi basi mla rushwa.
 
Back
Top Bottom