Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,566
Huu ni ukatili na unyanyasi dhidi ya watoto, tena kitoto kichanga cha miezi miwili!
Wana Jf kama mnavyokumbuka jana Mbunge Joyce Mukya alikamatwa na polisi katika vurugu zilizotokea jana, akiwa pamoja na wabunge wengine watatu Tundu Lissu, Said Arfi na Mustapha Akonaay.
Joyce Mukya aliletewa mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili ili akamnyonyeshe, Polisi wakakataa wakasema hatamnyonyesha, na kweli mtoto hakunyonyeshwa mpaka hivi tunavyoongea, tokea Mh. Joyce akamtwe jana na polisi!
Inasikitisha, inasononesha kwa kila binadamu mwenye moyo wa utu kuona haya yanatokea. Sijui kwanini jeshi letu linatumika kunyanyasa raia hasa watoto.
Polisi wanamnyima mtoto mdogo asinyonye maziwa ya mama, kana kwamba wao hawakuzaliwa na mama na hawajawahi kunyonya.
Mambo mengine ndugu zangu tuweke siasa pembeni, polisi wetu watangulize utu mbele.
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums