Ukatili wa kijinsia ni uvunjigu wa haki za Binadamu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,297
Dunia, mataifa makubwa na mataifa madogo, ulimwengu mzima unakubali kuwa haki za binadamu ni jambo lolote ambalo binadamu anastahili kuwa nalo tangu anapozaliwa bila ya kujali jinsi ya mtu.

Kiimani na kiutamaduni pia, inatambulika kuwa haki za binadamu zitaendelea kuwepo hadi pale binadamu atakapokuwa ameaga Dunia na hata kuzikwa, ndio maana dini zetu zimeelekeza mambo ambayo ni lazima afanyiwe binadamu pindi anapokufa na asipofanyiwa hivyo basio haki yake haitokuwepo.

Haki za binadamu zipo nyingi sana lakini tunapokuja kutazama Katika mikataba na sheria mbalimbali zinazohusu haki za binadamu, kuna haki za msingi ambazo mara nyingi ndizo zinazoonyeshwa ama kutajwa na haki hizo ni zile ambazo ni lazima kila binadamu awe nazo, mfano haki ya kuishi, haki ya faragha, haki ya kutoa maoni, na haki nyinginezo na Tanzania ni moja ya nchi inayoamini kuwa Binadamu wote ni sawa, Mwanaume na Mwanamke wote ni sawa.

Mila yeyote kandamizi, mila ambayo inakuwa inambana Mwanamke na kumuona siyo sehemu ya binadamu anayostahili kupata haki Fulani, mila hiyo itakuwa inavunja haki za Kibinadamu, na taifa ama mtu yeyote atakaeshiriki katika kuvunja haki za kibinadamu, mtu huyo atatakiwa kupata adhabu kulingana na maelekezo ya mikataba ya kimataifa Pamoja na sheria za nchi husika.

Katika maadhimisho haya ya siku kumi na sita za kupinga Ukatili wa Kijinsia, Dunia inapaswa kuambiwa kwa sauti kubwa, kuwa, Ukatili wa Kijinsia ni uvunjivu wa haki za binadamu, hakuna sheria yeyote inayoruhusu mtu kudhulumiwa au kuteswa, ama kuumizwa Kimwili, Kisaikolojia, kiuchumi na aina nyingine ya matesho ambayo ni sehemu ya Uvunjifu wa Haki za binadamu.

Pamoja na kuwa sheria zipo na zinafanya kazi, lakini bado Jamii zetu zinachukulia kama Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia dhidi ya Wanawake ni jambo la kawaida na jambo la kuchukulia kama mzaha.

Mzaha huo unatokana na kuonekana kama Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia ni jambo la kawaida kwa sababu tu limezoeleweka, ila ukweli unabaki palepale kuwa Maumivu yeyote yanayoingia Katika mwili wa binadamu, yanaleta madhara hadi Katika akili.

Mkataba wa kimataifa wa kupinga Ukatili, unazitaka nchi zote kulaani kila aina ya ama kitendo cha Ukatili dhidi ya Mwanamke na pia mkataba huo unazitaka nchi husika kuchukua hatua za kisheria na kisera kwa ajili ya kumlinda Mwanamke, na hata tukirejea Katika makubaliano ya Azimio la Beijing, tunaweza kuona kuwa Haki ya Mwanamke ni haki ya Binadamu, kama ni hivyo basi, jambo lolote ambalo ni la kikatili na Unyanyasaji dhidi ya Mwanamke, jambo hilo ni sehemu ya uvunjifu wa haki za binadamu.

Katika kuhubiri kwetu usawa na kupinga Ukatili wa kijinisia kwa Wanawake, sasa ni wakati wa kusema kwa sauti kubwa kuwa Jamii haipaswi kushiriki Katika jambo lolote kwa kigezo cha umwanamke wala umwanaume, Mwanamke hapaswi kuwa Katika nyadhifa fulani kwa sababu ni Mwanamke na mwanaume hapaswi kuwa Katika nyadhifa fulani kwa sababu ni mwanaume, ila kila mtu anastahili kuwa mtu Fulani, mwenye cheo na mamlaka Fulani kwa sababu ni binadamu na ni haki yake.

Idd Ninga
Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom