Ukatili wa kijinsia Arusha bado upo juu, wasichana ni waathirika wakubwa

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto Mkoani Arusha bado vipo juu, hivyo elimu zaidi inatakiwa kutolewa kuhakikisha jamii inaepukana na vitendo hivyo.

Aidha, takwimu za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa kwa Mkoa wa Arusha jumla ya wanawake 4,510 walifanyiwa ukatili wa kijinsia, huku kati ya hao mabinti wakiwa ni zaidi ya 1,000 wenye umri chini ya miaka 18.

Hayo yalisemwa na Mratibu wa Mpango wa Taita wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Arusha, Helena Materu wakati akizungumza katika tamasha la uelimishaji katika ngazi ya jamii kuhusu ndoa za utotoni na kupinga ukatili wa kijinsia na ukeketaji lililoandaliwa na Shirika la DSW Tanzania lililofanyıka katika Kata ya Musa, Halmashauri ya Arusha DC.

Materu alisema kuwa, takwimu hizo kwa mkoa wa Arusha bado ZIpo juu kutokana na jamii kuendelea kufanya vitendo hivyo ikiwemo ukeketaji kwa watoto ambao unaranywa Kwa siri pindi watoto wanapozaliwa ambapo aliitaka jamii kuungana kwa pamoja katika kupinga vitendo hivyo na hatimaye takwimu hizo Ziweze kushuka ifikapo 2023.

“Tunashukuru sana shirika hili la DSW kwa namna ambayo limekuwa likitoa elimu kwa jamii na wasichana wadogo kuhusu masuala ya ndoa za utotoni na ukeketaji ambapo kupitia watoto hao waliopata elimu hiyo wameweza kuwa mabalozi wazuri wa kuwarundisha wenzao ambao wamekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo katıka jamii zao kwa kweli huo ni mtano mzuri wa kuigwa kwani wanaisaidia serikali kwa kiasi kikubwa," amesema Materu.

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo na Afya kwa Vijana DSW lanzania, Peter Owaga aliséma shirika hilo linatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo wa Binti na maendeleo ambao unatekelezwa katika Halmashauri ya Arusha katika kata tano Ikiwemo ya Musa.

AMesema jamii imeweza kujengewa uwezo kuhusu masuala ya ukatili, ndoa za utotoni na ukeketaji lengo likiwa ni kuhakikisha jamii na mabinti wanakuwa na uelewa wa kutosha na kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo hivyo.

Alisema kuwa, kata hiyo imekuwa mfano wa kuigwa ambapo wataendelea kuwasaidia katika shughuli mbalimbali za vijana ikiwemo ukarabati wa maktaba ndogo iliyotolewa na halmashauri hiyo wakishirikiana na kata kwa lengo la kusaidia vijana na mabinti kupata sehemu ya kujifunzia.

Chanzo: Majira

Ukatili wa kijinsia Arusha, miaka ya Nyuma ilikuwa kama Ifuatavyo; 2017 Kesi zilizolipotiwa za Ukatili wa Kijinsia ni 2,790, 2018 Kesi zilizolipotiwa za Ukatili wa Kijinsia ni 3,904, Mwaka 2019 Kesi zilizolipotiwa za Ukatili wa Kijinsia ni 4,334, na Mwaka 2020 Kesi zilizolipotiwa za Ukatili wa Kijinsia ni 4,705.

Ukatili wa Kijinsia.jpg
 
Back
Top Bottom