kilagalila
JF-Expert Member
- Nov 8, 2018
- 320
- 154
Na.amiri kilagalila
mc.amiri/mr.mtaani
Mtoto anayekadiliwa kuwa na Umri wa Miaka miwili Ambaye Hajajulikana Jina Lake Amekutwa Akiwa amefariki na kutupwa korongoni karibu na Msitu Uliopo Pembezoni Mwa kanisa la EAGT lililopo katika Mtaa wa Sido Mjini Njombe.
Taarifa za kuonekana Kwa Mwili wa Mtoto huyo zimeanza kusambaa Majira ya asubuhi ya Novemba 16 wakati Wanafunzi wakielekea Shuleni.
Kufuatia kutokea kwa Tukio hilo Mtendaji wa Mtaa huo Rehema Ngailo amesema kuwa alipata taarifa ya kuonekana kwa mwili wa mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili mapema asubuhi hii leo na kuweza kufika katika eneo la tukio sambamba na kulijulisha jeshi la polisi huku akiendelea kushirikiana na wananchi wake ili kumbaini aliyetenda tukio hilo
"sijui kama na wananchi wa mtaa wangu waliofanya hivyo kwa kuwa ametupwa karibu na barabara ninachowaomba wananchi wangu kama wa mama ni vema yanapotokea matatzo ya kifamilia kufika katika ofisi yao kuliko kufanya kitendo kama hiki,matukio kama haya tumeendelea kuyapigia kelele sana katika mikutano yetu na sasa tumeshasambaza taarifa kwa wananchi wangu kuangalia kila nyumba kama kuna mtu aliyekuwa na mtoto na sasa hana tupeane taarifa kama ni wa mtaa wangu wa sido atatambulika tu na sheria itachukuliwa"alisema mtendaji
Vitendo Vya Kutupa Watoto,Kutelekeza na Hata Kuwauwa Vionekana Kuwa Kikwazo Kwa Wakazi wa Njombe Ambao Wamelaani Vikali Tukio Hilo.
"kwa sababu kama kwangu mimi hapa mungu amenijaalia mtoto mmoja nilitamani kupata watoto hadi watano lakini sikupata kwanini afanye kitendo kama hicho huu ni ukatili kwa kweli sisi akina mama tunatia aibu ni bora wangeniletea tu hata mimi hapa yaani sijui nisemaje"walisikika wananchi wakizungumza kwa jaziba
Mara baada ya Taarifa hizo kusambaa Jeshi La Polisi Mkoani Njombe limefika Katika Eneo la Tukio na Kuuondoa Mwili wa Mtoto huyo Ikiwa Wiki Mbili Zilizopita Mtoto Mwingine Mchanga Aliokotwa Katika Dampo la Kipagamo Mjini Makambako Akiwa Hai na Kisha Kupelekwa Katika Kituo Cha Kulelea Watoto Cha Tumaini Ilunda.